< Ezekiel 5 >

1 "You, son of man, take a sharp sword; You shall take it as a barber's razor to you, and shall cause it to pass on your head and on your beard: then take balances to weigh, and divide the hair.
“Mwanadamu, sasa chukua upanga mkali na uutumie kama wembe wa kinyozi ili kunyolea nywele za kichwa chako na ndevu zako. Kisha uchukue mizani ya kupimia ukazigawanye nywele hizo.
2 A third part you shall burn in the fire in the midst of the city, when the days of the siege are fulfilled; and you shall take a third part, and strike with the sword around it; and a third part you shall scatter to the wind, and I will draw out a sword after them.
Wakati siku zako za kuzingirwa zitakapokwisha, choma theluthi moja ya hizo nywele zako kwa moto ndani ya mji. Chukua theluthi nyingine ya hizo nywele uzipige kwa upanga kuuzunguka mji wote na theluthi nyingine ya mwisho utaitawanya kwa upepo. Kwa kuwa nitawafuatia kwa upanga uliofutwa.
3 You shall take of it a few in number, and bind them in your skirts.
Lakini chukua nywele chache uzifungie ndani ya pindo la vazi lako.
4 Of these again you shall take, and cast them into the midst of the fire, and burn them in the fire; from it shall a fire come forth into all the house of Israel."
Tena chukua nywele nyingine chache uzitupe motoni uziteketeze. Moto utaenea kutoka humo na kufika katika nyumba yote ya Israeli.
5 "Thus says the LORD: 'This is Jerusalem; I have placed her at the center of the nations, and countries are around her.
“Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Huu ndio Yerusalemu ambao nimeuweka katikati ya mataifa ukiwa umezungukwa na nchi pande zote.
6 She has rebelled against my ordinances in doing wickedness more than the nations, and against my statutes more than the countries that are around her; for they have rejected my ordinances, and as for my statutes, they have not walked in them.'
Lakini katika uovu wake umeasi sheria na amri zangu kuliko mataifa na nchi zinazouzunguka. Umeasi sheria zangu wala haukufuata amri zangu.
7 "Therefore thus says the LORD: 'Because you are turbulent more than the nations that are around you, and have not walked in my statutes, neither have kept my ordinances, neither have done after the ordinances of the nations that are around you';
“Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ninyi mmekuwa wakaidi kuliko mataifa yanayowazunguka na hamkufuata amri zangu wala kuzishika sheria zangu. Wala hamkuweza hata kuzifuata kawaida za mataifa yanayowazunguka.
8 therefore thus says the LORD: 'Look, I, even I, am against you; and I will execute judgments in the midst of you in the sight of the nations.
“Kwa hiyo, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo, Mimi mwenyewe, niko kinyume nanyi Yerusalemu, nitawapiga kwa adhabu yangu mbele ya mataifa.
9 I will do in you that which I have not done, and whereunto I will not do any more the like, because of all your abominations.
Kwa ajili ya sanamu zenu zote za machukizo, nitawafanyia kile ambacho kamwe sijawafanyia kabla wala kamwe sitawafanyia tena.
10 Therefore the fathers shall eat the sons in the midst of you, and the sons shall eat their fathers; and I will execute judgments on you; and the whole remnant of you will I scatter to all the winds.'
Kwa hiyo katikati yenu baba watakula watoto wao na watoto watakula baba zao. Nitawapiga kwa adhabu, nami nitawatawanya watu wenu walionusurika pande zote za dunia.
11 "'Therefore as I live,' says the LORD, 'surely, because you have defiled my sanctuary with all your detestable things, and with all your abominations, therefore I will also diminish you; neither shall my eye spare, and I also will have no pity.
Kwa hiyo hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, kwa kuwa mmenajisi mahali pangu patakatifu kwa sanamu zenu mbaya sana na desturi zenu za machukizo, mimi mwenyewe nitaondoa fadhili zangu kwenu.
12 A third part of you shall die with the pestilence, and with famine shall they be consumed in the midst of you; and a third part shall fall by the sword around you; and a third part I will scatter to all the winds, and will draw out a sword after them.
Theluthi ya watu wako watakufa kwa tauni au kwa njaa humu ndani yako, theluthi nyingine itaanguka kwa upanga nje ya kuta zako, nayo theluthi nyingine nitaitawanya kwenye pande nne kuwafuatia kwa upanga uliofutwa.
13 Thus shall my anger be accomplished, and I will cause my wrath toward them to rest, and I shall be comforted; and they shall know that I, the LORD, have spoken in my zeal, when I have accomplished my wrath on them.
“Ndipo hasira yangu itakapokoma na ghadhabu yangu dhidi yao itatulia, nami nitakuwa nimelipiza kisasi. Baada ya kuimaliza ghadhabu yangu juu yao, watajua kuwa mimi Bwana nimenena katika wivu wangu.
14 Moreover I will make you a desolation and a reproach among the nations that are around you, in the sight of all that pass by.
“Nitakuangamiza na kukufanya kitu cha kudharauliwa miongoni mwa mataifa yanayokuzunguka, machoni pa watu wote wapitao karibu nawe.
15 And you shall be a reproach and a taunt, an instruction and an astonishment, to the nations that are around you, when I shall execute judgments on you in anger and in wrath, and in wrathful rebukes; I, the LORD, have spoken;
Utakuwa kitu cha kudharauliwa na cha aibu, cha dhihaka, ovyo na kitu cha kutisha kwa mataifa yanayokuzunguka, nitakapokupiga kwa adhabu yangu katika hasira na ghadhabu yangu kwa kukukemea kwa ukali. Mimi Bwana nimesema.
16 when I shall send on them the evil arrows of famine, that are for destruction, which I will send to destroy you: and I will increase the famine on you, and will break your staff of bread;
Nitakapokupiga kwa mishale yangu ya kufisha na yenye kuharibu ya njaa, nitaipiga ili kukuangamiza. Nitaleta njaa zaidi na zaidi juu yako na kukomesha upatikanaji wa chakula kwako.
17 and I will send on you famine and evil animals, and they shall bereave you; and pestilence and blood shall pass through you; and I will bring the sword on you: I, the LORD, have spoken it.'"
Nitapeleka njaa na wanyama wa mwituni dhidi yenu, navyo vitawaacha bila watoto. Tauni na umwagaji wa damu utapita katikati yenu, nami nitaleta upanga juu yenu. Mimi Bwana nimenena haya.”

< Ezekiel 5 >