< Jezekiel 22 >

1 And the word of the Lord came to me, saying,
Neno la Bwana likanijia kusema:
2 And you, son of man, will you judge the bloody city? yes, declare you to her all her iniquities.
“Mwanadamu, je, wewe utauhukumu? Je, utauhukumu huu mji umwagao damu? Basi uujulishe juu ya matendo yake yote ya machukizo
3 And you shall say, Thus says the Lord God: O city that sheds blood in the midst of her, so that her time should come, and that forms devices against herself, to defile herself;
uuambie: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ee mji ule ujileteao maangamizi wenyewe kwa kumwaga damu ndani yake na kujinajisi wenyewe kwa kutengeneza sanamu,
4 in their blood which you have shed, you have transgressed; and in your devices which you have formed, you have polluted yourself; and you have brought near your days, and have brought on the time of your years: therefore have I made you a reproach to the Gentiles, and a mockery to all the countries,
umekuwa na hatia kwa sababu ya damu uliyomwaga na umetiwa unajisi kwa sanamu ulizotengeneza. Umejiletea mwisho wa siku zako na mwisho wa miaka yako umewadia. Kwa hiyo nitakufanya kitu cha kudharauliwa kwa mataifa na kitu cha mzaha kwa nchi zote.
5 to those near you, and to those far distant from you; and they shall mock you, [you that are] notoriously unclean, and abundant in iniquities.
Wale walio karibu na wale walio mbali watakudhihaki, Ewe mji wenye sifa mbaya, uliyejaa ghasia.
6 Behold, the princes of the house of Israel have conspired in you each one with his kindred, that they might shed blood.
“‘Ona jinsi kila mkuu wa Israeli aliyeko ndani yako anavyotumia nguvu zake kumwaga damu.
7 In you they have reviled father and mother; and in you they have behaved unjustly toward the stranger: they have oppressed the orphan and widow.
Ndani yako wamewadharau baba na mama, ndani yako wamewatendea wageni udhalimu na kuwaonea yatima na wajane.
8 And they have set at nothing my holy things, and in you they have profaned my sabbaths.
Mmedharau vitu vyangu vitakatifu na kuzinajisi Sabato zangu.
9 [There are] robbers in you, to shed blood in you; and in you they have eaten upon the mountains: they have wrought ungodliness in the midst of you.
Ndani yako wako watu wasingiziaji, watu walio tayari kumwaga damu, ndani yako wako wale wanaokula vyakula vilivyotolewa mahali pa ibada za miungu kwenye milima, na kutenda matendo ya uasherati.
10 In you they have uncovered the father's shame; and in you they have humbled her that was set apart for uncleanness.
Ndani yako wako wale wanaovunjia heshima vitanda vya baba zao, ndani yako wamo wale wanaowatendea wanawake jeuri wakiwa katika hedhi, wakati wakiwa si safi.
11 They have dealt unlawfully each one with his neighbor's wife; and each one in ungodliness has defiled his daughter-in-law: and in you they have humbled each one his sister, the daughter of his father.
Ndani yako mtu hufanya mambo ya machukizo na mke wa jirani yake, mwingine kwa aibu kubwa hukutana kimwili na mke wa mwanawe, mwingine humtenda jeuri dada yake, binti wa baba yake hasa.
12 In you they have received gifts to shed blood; they have received in you interest and usurious increase; and by oppression you have brought your wickedness to the full, and have forgotten me, says the Lord.
Ndani yako watu hupokea rushwa ili kumwaga damu, mnapokea riba na faida ya ziada na kupata faida isiyokuwa halali kutoka kwa jirani ili kupata faida kubwa kupita kiasi. Nawe umenisahau mimi, asema Bwana Mwenyezi.
13 And if I shall strike my hand at [your iniquities] which you have accomplished, which you have wrought, and at your blood that has been shed in the midst of you,
“‘Hakika nitapiga makofi kwa ajili ya faida isiyo halali uliyojipatia na kwa damu uliyoimwaga ndani yako.
14 shall your heart endure? shall your hands be strong in the days which I bring upon you? I the Lord have spoken, and will do [it].
Je, ujasiri wako utadumu au mikono yako itakuwa na nguvu siku hiyo nitakapokushughulikia? Mimi Bwana nimesema na nitalifanya.
15 And I will scatter you among the nations, and disperse you in the countries, and your uncleanness shall be removed out of you.
Nitakutawanya miongoni mwa mataifa na kukutapanya katika nchi mbalimbali nami nitakomesha unajisi wako.
16 And I will give heritages in you in the sight of the nations, and you shall know that I am the Lord.
Ukiisha kunajisika mbele ya mataifa, utajua kuwa Mimi ndimi Bwana.’”
17 And the word of the Lord came to me, saying,
Ndipo neno la Bwana likanijia kusema:
18 Son of man, behold, the house of Israel are all become to me [as it were] mixed with brass, and iron, and tin, and lead; they are mixed up in the midst of the silver.
“Mwanadamu, nyumba ya Israeli imekuwa kwangu takataka ya chuma, wote kwangu wamekuwa shaba, bati, chuma na risasi iliyoachwa kalibuni. Wao ni taka ya madini ya fedha tu.
19 Therefore say, Thus says the Lord God; Because you have become one mixture, therefore I will gather you into the midst of Jerusalem.
Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: ‘Kwa kuwa wote mmekuwa takataka ya chuma, nitawakusanya Yerusalemu.
20 As silver, and brass, and iron, and tin, and lead, are gathered into the midst of the furnace, to blow fire into it, that they may be melted: so will I take [you] in my wrath, and I will gather and melt you.
Kama vile watu wakusanyavyo fedha, shaba, chuma, risasi na bati kalibuni ili kuyeyusha kwa moto mkali, ndivyo nitakavyowakusanya katika hasira yangu na ghadhabu yangu kuwaweka ndani ya mji na kuwayeyusha.
21 And I will blow upon you in the fire of my wrath, and you shall be melted in the midst thereof.
Nitawakusanya na kupuliza juu yenu moto wa hasira yangu na ghadhabu yangu nanyi mtayeyushwa ndani ya huo mji.
22 As silver is melted in the midst of a furnace, so shall you be melted in the midst thereof; and you shall know that I the Lord have poured out my wrath upon you.
Kama fedha iyeyukavyo kalibuni, ndivyo mtakavyoyeyuka ndani ya huo mji, nanyi mtajua kuwa Mimi Bwana nimemwaga ghadhabu yangu juu yenu.’”
23 And the word of the Lord came to me, saying,
Neno la Bwana likanijia tena kusema:
24 Son of man, say to her, You are the land that is not rained upon, neither has rain come upon you in the day of wrath;
“Mwanadamu, iambie nchi, ‘Wewe ni nchi ambayo haijapata mvua wala manyunyu katika siku ya ghadhabu.’
25 whose princes in the midst of her are as roaring lions seizing prey, devouring souls by oppression, and taking bribes; and your widows are multiplied in the midst of you.
Kuna hila mbaya ya wakuu ndani yake kama simba angurumaye akirarua mawindo yake, wanakula watu, wanachukua hazina na vitu vya thamani na kuongeza idadi ya wajane ndani yake.
26 Her priests also have set at nothing my law, and profaned my holy things: they have not distinguished between the holy and profane, nor have they distinguished between the unclean and the clean, and have hid their eyes from my sabbaths, and I was profaned in the midst of them.
Makuhani wake wameihalifu sheria yangu na kunajisi vitu vyangu vitakatifu, hawatofautishi kati ya vitu vitakatifu na vitu vya kawaida. Wanafundisha kuwa hakuna tofauti kati ya vitu vilivyo najisi na visivyo najisi, nao wanafumba macho yao katika kutunza Sabato zangu, hivyo katikati yao nimetiwa unajisi.
27 Her princes in the midst of her are as wolves ravening to shed blood, that they may get dishonest gain.
Maafisa wake walioko ndani yake ni kama mbwa mwitu wararuao mawindo yao, wanamwaga damu na kuua watu ili kupata faida ya udhalimu.
28 And her prophets that daub them shall fall, that see vanities, that prophesy falsehoods, saying, Thus says the Lord, when the Lord has not spoken.
Manabii wake wanapaka chokaa matendo haya kwa maono ya uongo na utabiri wa udanganyifu. Wanasema, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo,’ wakati Bwana hajasema.
29 That sorely oppress the people of the land with injustice, and commit robbery; oppressing the poor and needy, and not dealing justly with the stranger.
Watu wa nchi wanatoza kwa nguvu na kufanya unyangʼanyi, wanawatenda jeuri maskini na wahitaji na kuwaonea wageni, wakiwanyima haki.
30 And I sought from among them a man behaving uprightly, and standing before me perfectly in the time of wrath, so that I should not utterly destroy her: but I found [him] not.
“Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, ambaye angejenga ukuta na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka kwa ajili ya watu wa nchi ili nisije nikaiangamiza, lakini sikumwona mtu yeyote.
31 So I have poured out my wrath upon her in the fury of mine anger, to accomplish [it]. I have recompensed their ways on their own heads, says the Lord God.
Hivyo nitaimwaga ghadhabu yangu juu yao na kuwateketeza kwa moto wa hasira yangu, nikiyaleta juu ya vichwa vyao yale yote waliyotenda, asema Bwana Mwenyezi.”

< Jezekiel 22 >