< 1 Corinthians 11 >

1 Be ye followers of me, even as I also [am] of Christ.
Igeni mfano wangu, kama ninavyouiga mfano wa Kristo.
2 Now I praise you, brethren, that ye remember me in all things, and keep the ordinances, as I delivered [them] to you.
Ninawasifu kwa kuwa mnanikumbuka katika kila jambo na kwa kushika mafundisho niliyowapa.
3 But I would have you know, that the head of every man is Christ; and the head of the woman [is] the man; and the head of Christ [is] God.
Napenda mfahamu kwamba kichwa cha kila mwanaume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanaume, nacho kichwa cha Kristo ni Mungu.
4 Every man praying or prophesying, having [his] head covered, dishonoureth his head.
Kila mwanaume anayeomba au kutoa unabii akiwa amefunika kichwa chake, anakiaibisha kichwa chake.
5 But every woman that prayeth or prophesieth with [her] head uncovered dishonoureth her head: for that is even all one as if she were shaven.
Naye kila mwanamke anayeomba au kutoa unabii pasipo kufunika kichwa chake, anakiaibisha kichwa chake, kwani ni sawa na yeye aliyenyoa nywele.
6 For if the woman be not covered, let her also be shorn: but if it be a shame for a woman to be shorn or shaven, let her be covered.
Kama mwanamke hatajifunika kichwa chake, basi inampasa kunyoa nywele zake. Lakini kama ni aibu kwa mwanamke kukata au kunyoa nywele zake, basi afunike kichwa chake.
7 For a man indeed ought not to cover [his] head, forasmuch as he is the image and glory of God: but the woman is the glory of the man.
Haimpasi mwanaume kufunika kichwa chake kwa kuwa yeye ni mfano wa Mungu na utukufu wa Mungu, lakini mwanamke ni utukufu wa mwanaume.
8 For the man is not of the woman; but the woman of the man.
Kwa maana mwanaume hakutoka kwa mwanamke, bali mwanamke alitoka kwa mwanaume.
9 Neither was the man created for the woman; but the woman for the man.
Wala mwanaume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanaume.
10 For this cause ought the woman to have power on [her] head because of the angels.
Kwa sababu hii na kwa sababu ya malaika, inampasa mwanamke awe na ishara ya mamlaka juu yake.
11 Nevertheless neither is the man without the woman, neither the woman without the man, in the Lord.
Lakini katika Bwana, mwanamke hajitegemei pasipo mwanaume na mwanaume hajitegemei pasipo mwanamke.
12 For as the woman [is] of the man, even so [is] the man also by the woman; but all things of God.
Kama vile mwanamke alivyoumbwa kutoka kwa mwanaume, vivyo hivyo mwanaume huzaliwa na mwanamke. Lakini vitu vyote vyatoka kwa Mungu.
13 Judge in yourselves: is it comely that a woman pray unto God uncovered?
Hukumuni ninyi wenyewe: Je, inafaa kwa mwanamke kumwomba Mungu bila kufunika kichwa chake?
14 Doth not even nature itself teach you, that, if a man have long hair, it is a shame unto him?
Je, maumbile ya asili hayatufundishi kuwa ni aibu kwa mwanaume kuwa na nywele ndefu?
15 But if a woman have long hair, it is a glory to her: for [her] hair is given her for a covering.
Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni utukufu kwake? Kwa maana mwanamke amepewa nywele ndefu ili kumfunika.
16 But if any man seem to be contentious, we have no such custom, neither the churches of God.
Kama mtu anataka kubishana juu ya jambo hili, sisi wala makanisa ya Mungu hatutambui desturi nyingine.
17 Now in this that I declare [unto you] I praise [you] not, that ye come together not for the better, but for the worse.
Basi katika maagizo yafuatayo, siwezi kuwasifu, kwa sababu mkutanikapo si kwa ajili ya faida bali kwa hasara.
18 For first of all, when ye come together in the church, I hear that there be divisions among you; and I partly believe it.
Kwanza, mnapokutana kama kanisa, nasikia kwamba kuna mgawanyiko miongoni mwenu, nami kwa kiasi fulani nasadiki kuwa ndivyo ilivyo.
19 For there must be also heresies among you, that they which are approved may be made manifest among you.
Bila shaka lazima pawe na tofauti miongoni mwenu ili kuonyesha ni nani anayekubaliwa na Mungu.
20 When ye come together therefore into one place, [this] is not to eat the Lord’s supper.
Mkutanikapo pamoja si chakula cha Bwana mnachokula,
21 For in eating every one taketh before [other] his own supper: and one is hungry, and another is drunken.
kwa kuwa mnapokula, kila mmoja wenu anakula bila kuwangoja wengine. Mmoja hukaa njaa na mwingine analewa.
22 What? have ye not houses to eat and to drink in? or despise ye the church of God, and shame them that have not? What shall I say to you? shall I praise you in this? I praise [you] not.
Je, hamna nyumbani kwenu ambako mnaweza kula na kunywa? Au mnalidharau kanisa la Mungu na kuwadhalilisha wale wasio na kitu? Niwaambie nini? Je, niwasifu juu ya jambo hili? La, hasha!
23 For I have received of the Lord that which also I delivered unto you, That the Lord Jesus the [same] night in which he was betrayed took bread:
Kwa maana mimi nilipokea kutoka kwa Bwana yale niliyowapa ninyi, kwamba Bwana Yesu, usiku ule aliposalitiwa, alitwaa mkate,
24 And when he had given thanks, he brake [it], and said, Take, eat: this is my body, which is broken for you: this do in remembrance of me.
naye akiisha kushukuru, akaumega, akasema, “Huu ndio mwili wangu, uliotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.”
25 After the same manner also [he took] the cup, when he had supped, saying, This cup is the new testament in my blood: this do ye, as oft as ye drink [it], in remembrance of me.
Vivyo hivyo baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu. Fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu.”
26 For as often as ye eat this bread, and drink this cup, ye do shew the Lord’s death till he come.
Maana kila mlapo mkate huu na kunywea kikombe hiki, mnatangaza mauti ya Bwana mpaka ajapo.
27 Wherefore whosoever shall eat this bread, and drink [this] cup of the Lord, unworthily, shall be guilty of the body and blood of the Lord.
Kwa hiyo, mtu yeyote alaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa na hatia ya dhambi juu ya mwili na damu ya Bwana.
28 But let a man examine himself, and so let him eat of [that] bread, and drink of [that] cup.
Inampasa mtu ajichunguze mwenyewe, kabla ya kula mkate na kukinywea kikombe.
29 For he that eateth and drinketh unworthily, eateth and drinketh damnation to himself, not discerning the Lord’s body.
Kwa maana mtu yeyote alaye na kunywa pasipo kuutambua mwili wa Bwana, hula na kunywa hukumu juu yake mwenyewe.
30 For this cause many [are] weak and sickly among you, and many sleep.
Hii ndiyo sababu wengi miongoni mwenu ni wagonjwa na dhaifu na wengine wenu hata wamekufa.
31 For if we would judge ourselves, we should not be judged.
Lakini kama tungejichunguza wenyewe tusingehukumiwa.
32 But when we are judged, we are chastened of the Lord, that we should not be condemned with the world.
Tunapohukumiwa na Bwana, tunaadibishwa ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu.
33 Wherefore, my brethren, when ye come together to eat, tarry one for another.
Kwa hiyo, ndugu zangu, mkutanikapo pamoja ili kula, mngojane.
34 And if any man hunger, let him eat at home; that ye come not together unto condemnation. And the rest will I set in order when I come.
Kama mtu akiwa na njaa, ale nyumbani kwake ili mkutanapo pamoja msije mkahukumiwa. Nami nitakapokuja nitawapa maelekezo zaidi.

< 1 Corinthians 11 >