< Leviticus 24 >

1 And the LORD spoke unto Moses, saying,
Yahweh akamwambia Musa, akisema,
2 Command the children of Israel, that they bring unto you pure oil olive beaten for the light, to cause the lamps to burn continually.
“Waamru watu wa Israeli wakuletee mafuta halisi yaliyokamliwa kutokana na mizeituni ili yatumike kwenye taa, ili kwamba taa ziweze kuwaka daima na kuleta mwanga.
3 Without the vail of the testimony, in the tabernacle of the congregation, shall Aaron order it from the evening unto the morning before the LORD continually: it shall be a statute for ever in your generations.
Nje ya pazia lililoko mbele ya sanduku la maamzi ndani ya hema la kukutania, Aroni ataiwasha daima taa mbele za Yahweh, tangu asubuhi hata jioni. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu.
4 He shall order the lamps upon the pure candlestick before the LORD continually.
Kuhani mkuu atazifanya taa ziwake daima mbele za Yahweh, taa hizo zilizo kwenye kinara cha dhahabu safi.
5 And you shall take fine flour, and bake twelve cakes thereof: two tenth deals shall be in one cake.
Yawapasa kuchukua unga laini na kuoka kwa huo mikate kumi na miwili. Ni lazima kuwe na mbili za kumi za efa za unga katika kila mkate.
6 And you shall set them in two rows, six on a row, upon the pure table before the LORD.
Kisha mtaipanga juu ya meza ya dhahabu safi mbele za Yahweh katika safu mbili, mikate sita katika kila safu,
7 And you shall put pure frankincense upon each row, that it may be on the bread for a memorial, even an offering made by fire unto the LORD.
Mtaweka uvumba safi kando ya kila safu ya mikata kuwa sadaka ya kuwakilisha. Uvumba huo utachomwa kwa moto kwa ajili ya Yahweh.
8 Every sabbath he shall set it in order before the LORD continually, being taken from the children of Israel by an everlasting covenant.
Kila siku ya Sabato kuhani mkuu sharti aipange kwa utaratibu hiyo mikate mbele za Yahweh kwa niaba ya watu wa Israeli, iwe ishara ya agano la milele.
9 And it shall be Aaron's and his sons'; and they shall eat it in the holy place: for it is most holy unto him of the offerings of the LORD made by fire by a perpetual statute.
Sadaka hii itakuwa kwa ajili ya Aroni na wanawe, na ni lazima waile mahali palipo patakatifu, kwa kuwa ni sehemu ya matoleo kwa Yahweh yaliyofanywa kwa moto.”
10 And the son of an Israelites woman, whose father was an Egyptian, went out among the children of Israel: and this son of the Israelites woman and a man of Israel strove together in the camp;
Sasa ilitokea kwamba mwana wa mwanamke Mwisraeli, ambaye baba yake alikuwa Mmisri, alikwenda miongoni mwa watu wa Israeli. Huyu mwana wa mwanamke Mwisraeli akagombana na mwanume Mwisraeli kambini.
11 And the Israelites woman's son blasphemed the name of the Lord, and cursed. And they brought him unto Moses: (and his mother's name was Shelomith, the daughter of Dibri, of the tribe of Dan: )
Mwana wa mwanamke Mwisraeli akalikufuru jina la Yahweh na kumlaani Mungu, kwa hiyo watu wakamleta kwa Musa. Jina la mama yake aliitwa Shelomithi, binti wa Dibri, kutoka kabila la Dani.
12 And they put him in ward, that the mind of the LORD might be showed them.
Wakamweka kizuizini mpaka Yahweh mwenyewe atakapotangaza mapenzi yake kwao.
13 And the LORD spoke unto Moses, saying,
Kisha Yahweh akamwambia Musa,
14 Bring forth him that has cursed without the camp; and let all that heard him lay their hands upon his head, and let all the congregation stone him.
“Mchukue nje ya kambi huyo aliyemlaani Mungu. Wale wote waliomskia wataweka mikono yao juu ya kichwa chake, na kisha kusanyiko lote watamponda kwa mawe.
15 And you shall speak unto the children of Israel, saying, Whosoever curses his God shall bear his sin.
Ni lazima uwaeleze watu wa Israeli na kusema, 'Yeyote anayemlaani Mungu wake imempasa kubeba hatia yake mwenyewe.
16 And he that blasphemes the name of the LORD, he shall surely be put to death, and all the congregation shall certainly stone him: as well the stranger, as he that is born in the land, when he blasphemes the name of the Lord, shall be put to death.
Yeye anayelikufuru jina la Yahweh kwa hakika ni lazima auawe. Hakika, kusanyiko lote litampiga mawe, ama awe mgeni au Mwisraeli mwenyeji mzaliwa. Ikiwa yeyote analikufuru jina la Yahweh, ni lazima auawe.
17 And he that kills any man shall surely be put to death.
Naye amuuaye mtu mwingine ni lazima kwa hakika auewa.
18 And he that kills a beast shall make it good; beast for beast.
Yeye anayemuua mnyama wa mwingine sharti amfidie, uhai kwa uhai.
19 And if a man cause a blemish in his neighbour; as he has done, so shall it be done to him;
Iwapo mtu anamjeruhi jirani yake, ni lazima atendewe vivyo hivyo alivyomtendea jirani yake:
20 Breach for breach, eye for eye, tooth for tooth: as he has caused a blemish in a man, so shall it be done to him again.
Mvunjiko kwa mvunjiko, jicho kwa jicho, jino kwa jino. Kama amesababisha jeraha kwa mtu, ndivyo ipasavyo kutendwa kwake.
21 And he that kills a beast, he shall restore it: and he that kills a man, he shall be put to death.
Yeyote auaye mnyama ni lazima amfidie, na yeyote auaye mtu ni lazima auawe.
22 All of you shall have one manner of law, as well for the stranger, as for one of your own country: for I am the LORD your God.
Ni lazima mwe na sheria moja kwa wote, mgeni na Mwisraeli mwenyeji mzaliwa, kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh Mungu wanu.”
23 And Moses spoke to the children of Israel, that they should bring forth him that had cursed out of the camp, and stone him with stones. And the children of Israel did as the LORD commanded Moses.
Kwa hiyo Musa akazungumza na watu wa Israeli, nao watu wakamleta mwanaume huyo nje ya kambi, yule ambaye alikuwa amemlaani Yahweh. Wakampiga kwa mawe. Watu waisraeli wakaitekeleza amri ya Yahweh aliyoitoa kupitia Musa.

< Leviticus 24 >