< Jeremiah 50 >

1 The word that the LORD spoke against Babylon and against the land of the Chaldeans by Jeremiah the prophet.
Hili ni neno alilolisema Yahwe juu ya Babeli, nchi ya Wakalidayo, kwa mkono wa Yeremia nabii,
2 Declare all of you among the nations, and publish, and set up a standard; publish, and conceal not: say, Babylon is taken, Bel is confounded, Merodach is broken in pieces; her idols are confounded, her images are broken in pieces.
“Wajulishe mataifa ili wasikie. Toa ishara ili wasikie. Usiiache. Sema, 'Babeli imetwaliwa. Beli ameaibika. Merodaki amefadhaika. Sanamu zake zimeaibishwa; vinyago vyake vimefadhaika
3 For out of the north there comes up a nation against her, which shall make her land desolate, and none shall dwell therein: they shall remove, they shall depart, both man and beast.
Taifa kutoka kaskazini litainuka kinyume chake, ili kuifanya nchi yake ukiwa. Hakuna hata mmoja, awe mtu au mnyama, atakayeishi ndani yake. Wataondoka.
4 In those days, and in that time, says the LORD, the children of Israel shall come, they and the children of Judah together, going and weeping: they shall go, and seek the LORD their God.
Katika siku hizo na wakati huo - hili ni tamko ya Yahwe - watu wa Israeli na watu wa Yuda watakusanyika ili kwenda kwa kulia na kumtafuta Yahwe Mungu wao.
5 They shall ask the way to Zion with their faces in that direction, saying, Come, and let us join ourselves to the LORD in a perpetual covenant that shall not be forgotten.
Watauliza njia ya kwenda Sayuni nao watakwenda huko, wakisema, tutakwenda wenyewe ili kuungana na Yahwe katika agano la milele lisilosahaulikal
6 My people has been lost sheep: their shepherds have caused them to go astray, they have turned them away on the mountains: they have gone from mountain to hill, they have forgotten their resting place.
Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea. Wachungaji wao wamewapoteza milimani; wamewageuza kutoka mlima hata mlima. Walikwenda, wakasahau mahali walipokuwa wanaishi.
7 All that found them have devoured them: and their adversaries said, We offend not, because they have sinned against the LORD, the habitation of justice, even the LORD, the hope of their fathers.
Kila awaendeaye anawararua. Washitaki wao walisema, 'Hatuna hatia, kwa sababu walimtenda dhambi Yahwe, nyumbani kwao halisi - Yahwe, tumaini la mababu zao.'
8 Remove out of the midst of Babylon, and go forth out of the land of the Chaldeans, and be as the he goats before the flocks.
Tokeni kati ya Babeli; tokeni katika nchi ya Wakalidayo; iweni kama wafanyavyo mabeberu mbele ya kundi lote.
9 For, lo, I will raise and cause to come up against Babylon an assembly of great nations from the north country: and they shall set themselves in array against her; from thence she shall be taken: their arrows shall be as of a mighty expert man; none shall return in vain.
Maana tazama, ninaelekea kupeleka na kuinua kinyume cha Babeli kundi la mataifa makubwa kutoka kaskazini. Yatajipanga yenyewe kinyume chake. Kutoka hapo Babeli utatekwa. Mishale yao ni kama shujaa mzoefu asiyerudi mikono tupu.
10 And Chaldea shall be a spoil: all that spoil her shall be satisfied, says the LORD.
Ukaldayo itakuwa mateka. Wate waitekao wataridhika - asema Yahwe.
11 Because all of you were glad, because all of you rejoiced, O all of you destroyers of mine heritage, because all of you are grown fat as the heifer at grass, and bellow as bulls;
Mnafurahi, mnasherehekea kuteka urithi wangu; mnarukaruka kama ndama anayekanyaga katika malisho yake; mnalia kama farasi mwenye nguvu.
12 Your mother shall be sore confounded; she that bare you shall be ashamed: behold, the hindermost of the nations shall be a wilderness, a dry land, and a desert.
Hivyo mama yenu ataaibika sana; aliyewazaa atafadhaika. Tazama, atakuwa wa mwisho katika mataifa, nyika, nchi kame, na jangwa.
13 Because of the wrath of the LORD it shall not be inhabited, but it shall be wholly desolate: every one that goes by Babylon shall be astonished, and hiss at all her plagues.
Kwa sababu ya hasira ya Yahwe, Babeli haitakaliwa, lakini itakuwa ukiwa mtupu. Kila apitaye kando ataogopa kwa sababu ya Babeli na atatoa sauti kwa sababu ya majeraha yake.
14 Put yourselves in array against Babylon round about: all you that bend the bow, shoot at her, spare no arrows: for she has sinned against the LORD.
Jipangeni wenyewe kumzunguka Babeli kinyume chake. Kila apindaye upinde na ampige. Msizuie mshale wenu wowote, maana amemtenda dhambi Yahwe.
15 Shout against her round about: she has given her hand: her foundations are fallen, her walls are thrown down: for it is the vengeance of the LORD: take vengeance upon her; as she has done, do unto her.
Pigeni kelele za ushindi kinyume chake ninyi nyote mmzungukao. Amesalimu mamlaka yake; minara yake imeanguka. Kuta zake zimebomolewa, maana hiki ni kisasi cha Yahwe. Jilipizeni kisasi juu yake! Mtendeeni kama alivyoyatenda mataifa mengine.
16 Cut off the sower from Babylon, and him that handles the sickle in the time of harvest: for fear of the oppressing sword they shall turn every one to his people, and they shall flee every one to his own land.
Waaribuni wote mkulima apandaye mbegu naye atumiaye mundu wakati wa mavuno katika Babeli. Haya kila mtu na arudi kwa watu wake kutoka upanga wa mtesaji; na wakimbilie katika nchi yao wenyewe.
17 Israel is a scattered sheep; the lions have driven him away: first the king of Assyria has devoured him; and last this Nebuchadrezzar king of Babylon has broken his bones.
Israeli ni kondoo aliyetawanywa na kupelekwa na simba mbali. Kwanza mfalme wa Ashuru alimrarua; kisha baadaye, Nebukadneza mfalme wa Babeli akavunja mifupa yake.
18 Therefore thus says the LORD of hosts, the God of Israel; Behold, I will punish the king of Babylon and his land, as I have punished the king of Assyria.
Kwa hiyo Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Tazama, nitamwadhibu mfalme wa Babeli na nchi yake, kama nilivyomwadhibu mfalme wa Ashuru.
19 And I will bring Israel again to his habitation, and he shall feed on Carmel and Bashan, and his soul shall be satisfied upon mount Ephraim and Gilead.
Nitamrudisha Israeli katika nchi yake; atajilisha katika Karmeli na Bashani. Kisha atajishibisha katika nchi ya kilima ya Efraimu na Gileadi.
20 In those days, and in that time, says the LORD, the iniquity of Israel shall be sought for, and there shall be none; and the sins of Judah, and they shall not be found: for I will pardon them whom I reserve.
Siku hizo na wakati huo, asema Yahwe, uovu utatafutwa katika Israeli, lakini hautaonekana. Nitauliza kuhusu dhambi za Yuda, lakini hazitaonekana, maana nitawasamehe mabaki niliowaacha.”
21 Go up against the land of Merathaim, even against it, and against the inhabitants of Pekod: waste and utterly destroy after them, says the LORD, and do according to all that I have commanded you.
Inuka dhidi ya nchi ya Merathaimu, kinyume chake nao waishio Pekodi. Wapigeni kwa makali ya upanga na mwatenge kwa ajili ya maangamizo - asema Yahwe - fanyeni kila ninachowaamru.
22 A sound of battle is in the land, and of great destruction.
Sauti ya vita na maangamizi ya kustaajabisha yamo katika nchi.
23 How is the hammer of the whole earth cut asunder and broken! how is Babylon become a desolation among the nations!
Jinsi gani nyundo ya mataifa yote imekatiliwa mbali na kuharibiwa. Jinsi Babeli amekuwa kitu cha kushangaza kati ya mataifa.
24 I have laid a snare for you, and you are also taken, O Babylon, and you were not aware: you are found, and also caught, because you have striven against the LORD.
Nimetega mtego dhidi yako. Umenaswa, Babeli, nawe haukutambua! Ulionekana na kukamatwa, tangu uliponidhihaki, Yahwe.
25 The LORD has opened his armoury, and has brought forth the weapons of his indignation: for this is the work of the Lord GOD of hosts in the land of the Chaldeans.
Yahwe amefungua ghala lake la silaha na anachukua silaha kwa ajili ya kutekekeleza hasira yake. Kuna kazi kwa ajili ya Yahwe wa majeshi katika nchi ya Wakaldayo.
26 Come against her from the utmost border, open her storehouses: cast her up as heaps, and destroy her utterly: let nothing of her be left.
Mshambulie kutokea mbali. Fungua maghala yake ya chakula na kumrundika kama marundo ya nafaka. Mtenge mbali na maangamizi. Usimbakizie masalia.
27 Slay all her bullocks; let them go down to the slaughter: woe unto them! for their day has come, the time of their visitation.
Ua madume wake wote wa ng'ombe. Washushe sehemu ya machinjio. Ole wao, maana siku yao imefika - wakati wa kuadhibiwa kwao.
28 The voice of them that flee and escape out of the land of Babylon, to declare in Zion the vengeance of the LORD our God, the vengeance of his temple.
Kuna sauti ya wale wanaokimbia, walionusurika, katika nchi ya Babeli. Hawa watatoa taarifa ya kisasi cha Yahwe Mungu wetu kwa Sayuni, kisasi kwa hekalu lake.”
29 Call together the archers against Babylon: all you that bend the bow, camp against it round about; let none thereof escape: recompense her according to her work; according to all that she has done, do unto her: for she has been proud against the LORD, against the Holy One of Israel.
Ita wapiga pinde dhidi ya Babeli - wale wote wapindao pinde zao. Piga kambi kinyume chake, na msimwache yeyote kutoroka. Mlipeni kwa kile alichofanya. Mfanyieni kwa kipimo alichotumia. Maana amemdharau Yahwe, Mtakatifu wa Israeli.
30 Therefore shall her young men fall in the streets, and all her men of war shall be cut off in that day, says the LORD.
Hivyo vijana wake wataanguka katika viwanja vya mji, na wapiganaji wake wote wataangamizwa siku hiyo - hili ni tamko la Yahwe.”
31 Behold, I am against you, O you most proud, says the Lord GOD of hosts: for your day has come, the time that I will visit you.
Tazama, mimi ni kunyume chako, mwenye majivuno - hili ni tamko la Bwana Yahwe wa majeshi - maana siku yako imefika, mwenye kiburi, wakati nitakapokuadhibu.
32 And the most proud shall stumble and fall, and none shall raise him up: and I will kindle a fire in his cities, and it shall devour all round about him.
Hivyo wenye kiburi watajikwaa na kuanguka. Hakuna atakaye wainua. Nitawasha moto katika miji yao; utateketeza kila kitu kati yake.
33 Thus says the LORD of hosts; The children of Israel and the children of Judah were oppressed together: and all that took them captives held them fast; they refused to let them go.
Yahwe wa majeshi asema hivi: watu wa Israeli wamenyanyaswa, pamoja na watu wa Yuda. Wate waliowateka bado wanawashikilia; wanakataa kuwaacha waondoke.
34 Their Redeemer is strong; the LORD of hosts is his name: he shall thoroughly plead their cause, that he may give rest to the land, and trouble the inhabitants of Babylon.
Yeye awaokoaye ni mwenye nguvu. Yahwe wa majeshi ni jina lake. Kwa hakika atalitetea shitaka lao, ili kuleta pumziko katika nchi, na kuwapiga wakaao Babeli.
35 A sword is upon the Chaldeans, says the LORD, and upon the inhabitants of Babylon, and upon her princes, and upon her wise men.
Upanga u juu ya Wakalidayo - asema Yahwe - na juu ya wakaao Babeli, viongozi wake, na wenye hekima wake.
36 A sword is upon the liars; and they shall be foolish: a sword is upon her mighty men; and they shall be dismayed.
Upanga unakuja juu ya waganga, ili wajione kuwa wajinga. Upanga utakuwa juu ya askari wake, hivyo watajaa hofu.
37 A sword is upon their horses, and upon their chariots, and upon all the mingled people that are in the midst of her; and they shall become as women: a sword is upon her treasures; and they shall be robbed.
Upanga utakuwa juu ya farasi wake, vibandawazi vyao na na watu wote waliomo Babeli, hivyo watakuwa kama wanawake. Upanga utakuwa juu ya ghala zake, nazo zitatekwa.
38 A drought is upon her waters; and they shall be dried up: for it is the land of graven images, and they are mad upon their idols.
Ukame unakuja juu ya maji yake, hivyo yatakauka. Maana ni nchi ya miungu wasiofaa, na wanafanya kama watu waliofanywa punguani kwa miungu yao isiyosaidia.
39 Therefore the wild beasts of the desert with the wild beasts of the islands shall dwell there, and the owls shall dwell therein: and it shall be no more inhabited for ever; neither shall it be dwelt in from generation to generation.
Hivyo wanyama wa jangwani wakaishi na mbwea wataishi huko, na watoto wa mbuni wataishi ndani yake. Kwa muda wote, hatakaliwa tena. Kutoka kizazi hata kizazi, hatakaliwa tena na watu.
40 As God overthrew Sodom and Gomorrah and the neighbour cities thereof, says the LORD; so shall no man abide there, neither shall any son of man dwell therein.
Kama vile Mungu alivyoziangamiza Sodoma na Gomora na majirani zake - asema Yahwe - hakuna atakayeishi huko; hakuna mtu atakayekaa ndani yake.”
41 Behold, a people shall come from the north, and a great nation, and many kings shall be raised up from the coasts of the earth.
“Tazama, watu wanakuja kutoka kaskazini, maana taifa kubwa na wafalme wengi wamemtikisa kutokea mbali.
42 They shall hold the bow and the lance: they are cruel, and will not show mercy: their voice shall roar like the sea, and they shall ride upon horses, every one put in array, like a man to the battle, against you, O daughter of Babylon.
Watachukua pinde na mishale. Ni wakatili na hawana huruma. Sauti yao ni kama mngurumo wa bahari, na wamepanda farasi katika mpangilio kama watu wapiganao, dhidi yako, bindi Babeli.
43 The king of Babylon has heard the report of them, and his hands waxed feeble: anguish took hold of him, and pangs as of a woman in travail.
Mfalme wa Babeli amesikia habari yao na mikono yake imelegea kwa huzuni. Mashaka yamemshika kama mwanamke katika utungu.
44 Behold, he shall come up like a lion from the swelling of Jordan unto the habitation of the strong: but I will make them suddenly run away from her: and who is a chosen man, that I may appoint over her? for who is like me? and who will appoint me the time? and who is that shepherd that will stand before me?
Tazama! Anakwenda juu kama simba atokaye katika miinuko ya Yordani kuelekea katika eneo la malisho ya uvumilivu. Maana kwa haraka nitawafanya wakimbie kutoka humo, nami nitamweka mtu aliyechaguliwa kwa uangalizi wake. Maana ni nani aliye kama mimi, na ni nani atakayeniagiza? Mchungaji gani awezaye kunizuia?
45 Therefore hear all of you the counsel of the LORD, that he has taken against Babylon; and his purposes, that he has purposed against the land of the Chaldeans: Surely the least of the flock shall draw them out: surely he shall make their habitation desolate with them.
Sikilizeni mipango ambayo Yahwe ameamua juu ya Babeli, mipango aliyonayo dhidi ya nchi ya Wakaldayo. Kwa hakika wataondolewa, hata kundi dogo zaidi. Eneo lao la malisho litageuzwa kuwa sehemu zenye magofu.
46 At the noise of the taking of Babylon the earth is moved, and the cry is heard among the nations.
Kwa sauti ya kuangushwa kwa Babeli nchi inatikisika, na sauti ya mateso yao inasikiwa kati ya mataifa.”

< Jeremiah 50 >