< 2 Samuel 12 >

1 And the LORD sent Nathan unto David. And he came unto him, and said unto him, There were two men in one city; the one rich, and the other poor.
Kisha Yahwe akamtuma Nathani kwa Daudi. Akaja kwake na kusema, “Kulikuwa na watu wawili katika mji. Mmoja alikuwa tajiri na mwingine alikuwa masikini.
2 The rich man had exceeding many flocks and herds:
Yule tajiri alikuwa na kundi la ng'ombe na kondoo wengi sana,
3 But the poor man had nothing, save one little ewe lamb, which he had bought and nourished up: and it grew up together with him, and with his children; it did eat of his own food, and drank of his own cup, and lay in his bosom, and was unto him as a daughter.
lakini maskini hakuwa na chochote isipokuwa mwanakondoo, aliyekuwa amemnunua na kumlisha na kumlea. Akakua pamoja naye na pamoja na watoto wake. Yule mwanakondoo hata alikula naye na kunywa kutoka katika kikombe chake, naye akalala katika mikono yake na alikuwa kama binti kwake.
4 And there came a traveller unto the rich man, and he spared to take of his own flock and of his own herd, to dress for the travelling man that was come unto him; but took the poor man's lamb, and dressed it for the man that was come to him.
Siku moja tajiri akapata mgeni, lakini yeye hakuwa tiyari kuchukua mnyama kutoka katika kundi lake la ng'ombe au kundi la kondoo ili kumwandalia chakula. Badala yake alichukua mwanakondoo wa masikini na akampika kwa ajili ya mgeni wake.
5 And David's anger was greatly kindled against the man; and he said to Nathan, As the LORD lives, the man that has done this thing shall surely die:
Hasira ya Daudi ikawaka dhidi ya tajiri yule, naye akamwambia Nathani kwa hasira, “Kama Yahwe aishivyo, mtu aliyelitenda jambo hili anastahili kufa.
6 And he shall restore the lamb fourfold, because he did this thing, and because he had no pity.
Ni lazima alipe mwanakondoo mara nne zaidi kwa ajili ya kile alichokifanya, na kwa sababu hakuwa na huruma kwa mtu maskini.
7 And Nathan said to David, You are the man. Thus says the LORD God of Israel, I anointed you king over Israel, and I delivered you out of the hand of Saul;
Ndipo Nathani akamwambia Daudi, “Wewe ndiye yule mtu! Yahweh, Mungu wa Israeli, asema, 'Nilikutia mafuta uwe mfalme juu ya Israeli, na nilikuokoa kutoka katika mkono wa Sauli.
8 And I gave you your master's house, and your master's wives into your bosom, and gave you the house of Israel and of Judah; and if that had been too little, I would moreover have given unto you such and such things.
Nikakupa nyumba ya bwana wako, na wake zake mikononi mwako. Nilikupa pia nyumba ya Israeli na Yuda. Na ikiwa hayo yalikuwa kidogo zaidi kwako, ningeweza kukuongezea mengine zaidi.
9 Wherefore have you despised the commandment of the LORD, to do evil in his sight? you have killed Uriah the Hittite with the sword, and have taken his wife to be your wife, and have slain him with the sword of the children of Ammon.
Hivyo basi kwa nini umedharau maagizo ya Yahwe, hata ukafanya yaliyo maovu mbele zake? Umeua Uria Mhiti kwa upanga na umechukua mkewe kuwa mke wako. Uliua kwa upanga wa jeshi la Amoni.
10 Now therefore the sword shall never depart from your house; because you have despised me, and have taken the wife of Uriah the Hittite to be your wife.
Hivyo basi upanga hautaondoka nyumbani mwako, kwa kuwa umenidharau na umemchukua mke wa Uria mhiti kuwa mke wako.'
11 Thus says the LORD, Behold, I will raise up evil against you out of your own house, and I will take your wives before your eyes, and give them unto your neighbour, and he shall lie with your wives in the sight of this sun.
Yahwe asema, 'Tazama, nitaleta maafa dhidi yako kutoka katika nyumba yako mwenyewe. Nitachukua wake zako, mbele ya macho yako na kumpa jirani yako, naye atalala na wake zako wakati wa mchana.
12 For you did it secretly: but I will do this thing before all Israel, and before the sun.
Kwa maana wewe ulitenda dhambi hii sirini, lakini mimi nitatenda jambo hili wakati wa mchana mbele za Israeli wote.
13 And David said unto Nathan, I have sinned against the LORD. And Nathan said unto David, The LORD also has put away your sin; you shall not die.
Ndipo Daudi alipomwambia Nathani, “Nimemtenda dhambi Yahwe.” Nathani akamjibu Daudi, “Yahwe naye ameiachilia dhambi yako. Hautakufa.
14 Nevertheless, because by this deed you have given great occasion to the enemies of the LORD to blaspheme, the child also that is born unto you shall surely die.
Lakini, kwa kuwa kwa tendo hili umemdharau Yahwe, mtoto aliyezaliwa kwako hakika atakufa.”
15 And Nathan departed unto his house. And the LORD struck the child that Uriah's wife bare unto David, and it was very sick.
Kisha Nathani akaondoka na kwenda kwake. Yahwe akampiga mtoto ambaye mke wa Uria alimzaa kwa Daudi, naye akaugua sana.
16 David therefore besought God for the child; and David fasted, and went in, and lay all night upon the earth.
Kisha Daudi akamwomba Mungu kwa ajili ya kijana. Daudi akafunga naye akaingia ndani na kulala usiku wote juu ya sakafu.
17 And the elders of his house arose, and went to him, to raise him up from the earth: but he would not, neither did he eat bread with them.
Wazee wa nyumba yake wakainuka na kusimama kando yake, ili wamwinue kutoka sakafuni. Lakini hakuinuka, na hakula pamoja nao.
18 And it came to pass on the seventh day, that the child died. And the servants of David feared to tell him that the child was dead: for they said, Behold, while the child was yet alive, we spoke unto him, and he would not hearken unto our voice: how will he then vex himself, if we tell him that the child is dead?
Ikawa siku ya saba mtoto akafa. Watumishi wa Daudi wakaogopa kumwambia kwamba mtoto amekufa, kwa maana walisema, “Tazama, wakati mtoto alipokuwa hai tuliongea naye, lakini hakuisikiliza sauti yetu. Atakuwaje ikiwa tutamwambia kwamba kijana amekufa?!”
19 But when David saw that his servants whispered, David perceived that the child was dead: therefore David said unto his servants, Is the child dead? And they said, He is dead.
Daudi alipoona kwamba watumishi wake walikuwa wakinong'onezana, Akatambua kwamba mtoto amekufa. Akawauliza, “Je mtoto amekufa?” Wakajibu, “Amekufa.”
20 Then David arose from the earth, and washed, and anointed himself, and changed his apparel, and came into the house of the LORD, and worshipped: then he came to his own house; and when he required, they set bread before him, and he did eat.
Kisha Daudi akainuka kutoka sakafuni naye akaoga, akajipaka mafuta, na kubadili mavazi yake. Akaenda katika hema la kukutania na akaabudu pale, kisha akarudu katika kasri lake. Akataka chakula kiletwe, wakamwandalia, naye akala.
21 Then said his servants unto him, What thing is this that you have done? you did fast and weep for the child, while it was alive; but when the child was dead, you did rise and eat bread.
Ndipo watumishi wake walipomwambia, “Kwa nini umefanya jambo hili? Ulifunga na kulia kwa ajili ya mtoto wakati alipokuwa hai, lakini mtoto alipokufa, ukainuka na kula.”
22 And he said, While the child was yet alive, I fasted and wept: for I said, Who can tell whether GOD will be gracious to me, that the child may live?
Daudi akajibu, “Wakati mtoto alipokuwa hai nilifunga na kulia. Nilisema, Ni nani ajuaye kwamba Yahwe angeweza kunihurumia mtoto akaishi au sivyo?
23 But now he is dead, wherefore should I fast? can I bring him back again? I shall go to him, but he shall not return to me.
Lakini sasa amekufa, hivyo nifungie nini? Je naweza kumrudisha tena? Nitakwenda kwake, lakini yeye hawezi kunirudia.”
24 And David comforted Bathsheba his wife, and went in unto her, and lay with her: and she bare a son, and he called his name Solomon: and the LORD loved him.
Daudi akamfariji Bethsheba mkewe, akaingia kwake, na akalala naye. Baadaye akazaa mtoto wa kiume, naye akaitwa Selemani. Yahwe akampenda
25 And he sent by the hand of Nathan the prophet; and he called his name Jedidiah, because of the LORD.
naye akatuma neno kupitia nabii Nathani kumwita Yedidia, kwa sababu Yahwe alimpenda.
26 And Joab fought against Rabbah of the children of Ammon, and took the royal city.
Basi Yoabu akapigana na Raba, mji wa kifalme wa watu wa Amoni, naye akaiteka ngome yake.
27 And Joab sent messengers to David, and said, I have fought against Rabbah, and have taken the city of waters.
Hivyo Yoabu akatuma wajumbe kwa Daudi na kusema, “Nimepigana na Raba, nami nimeshikilia sehemu inayosambaza maji ya mji.
28 Now therefore gather the rest of the people together, and camp against the city, and take it: lest I take the city, and it be called after my name.
Kwa hiyo sasa likusanye jeshi lililosalia uhuzingire mji na kuuteka, kwa maana ikiwa nitauteka, utaitwa kwa jina langu.”
29 And David gathered all the people together, and went to Rabbah, and fought against it, and took it.
Hivyo Daudi akalikusanya jeshi lote na kwenda Raba; akapigana nao na kuuteka.
30 And he took their king's crown from off his head, the weight whereof was a talent of gold with the precious stones: and it was set on David's head. And he brought forth the spoil of the city in great abundance.
Daudi akachukua taji ya dhahabu kutoka katika kichwa cha mfalme wao iliyokuwa na uzito wa talanta, na ilikuwa na jiwe la thamani ndani yake. Taji ikawekwa juu ya kichwa cha Daudi. Kisha akachukua nyara za mji kwa wingi.
31 And he brought forth the people that were therein, and put them under saws, and under harrows of iron, and under axes of iron, and made them pass through the brick-kiln: and thus did he unto all the cities of the children of Ammon. So David and all the people returned unto Jerusalem.
Akawatoa watu waliokuwa mjini naye akawalazimisha kufanya kazi kwa misumeno, sululu na shoka; lakini pia akawalazimisha kutengeneza matofali. Daudi akailazimisha miji yote ya watu wa Amoni kufanya kazi hiyo. Kisha Daudi na jeshi lote wakarudi Yerusalemu

< 2 Samuel 12 >