< Matthew 3 >

1 In those days came John the Baptist, preaching in the wilderness of Judaea,
Katika siku zile Yohana Mbatizaji alikuja akihubiri katika nyika ya Yuda akisema,
2 And saying, Repent you: for the kingdom of heaven is at hand.
“Tubuni kwa maana ufalme wa mbinguni u karibu.”
3 For this is he that was spoken of by the prophet Isaiah, saying, The voice of one crying in the wilderness, Prepare you the way of the Lord, make his paths straight.
Kwa maana huyu ndiye aliyenenwa na nabii Isaya akisema, “sauti ya mtu aitaye kutoka jangwani; 'wekeni tayari njia ya Bwana, yanyoosheni mapito yake.”'
4 And the same John had his raiment of camel’s hair, and a leather girdle about his loins; and his meat was locusts and wild honey.
Sasa Yohana alivaa manyoya ya ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.
5 Then went out to him Jerusalem, and all Judaea, and all the region round about Jordan,
Kisha Yerusalemu, Yuda yote, na eneo lote linalozunguka mto Yorodani wakaenda kwake.
6 And were baptized of him in Jordan, confessing their sins.
Walikuwa wakibatizwa naye katika mto Yorodani huku wakitubu dhambi zao.
7 But when he saw many of the Pharisees and Sadducees come to his baptism, he said to them, O generation of vipers, who has warned you to flee from the wrath to come?
Lakini alipowaona wengi wa mafarisayo na masadukayo wakija kwake kubatizwa, akawaambia, ''Enyi uzao wa nyoka wenye sumu nani aliye waonya kuikimbia ghadhabu inayokuja?
8 Bring forth therefore fruits meet for repentance:
Zaeni matunda yaipasayo toba.
9 And think not to say within yourselves, We have Abraham to our father: for I say to you, that God is able of these stones to raise up children to Abraham.
Na msifikiri na kusemezana miongoni mwenu, 'Tunaye Ibrahimu kama baba yetu.' Kwa kuwa nawaambieni Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto hata kutoka katika mawe haya.
10 And now also the ax is laid to the root of the trees: therefore every tree which brings not forth good fruit is hewn down, and cast into the fire.
Tayari shoka limekwisha kuwekwa kwenye mzizi wa miti. Kwahiyo kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa kwenye moto.
11 I indeed baptize you with water to repentance. but he that comes after me is mightier than I, whose shoes I am not worthy to bear: he shall baptize you with the Holy Ghost, and with fire:
Ninawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba. Lakini yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi nami sistahili hata kubeba viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
12 Whose fan is in his hand, and he will thoroughly purge his floor, and gather his wheat into the garner; but he will burn up the chaff with unquenchable fire.
Na pepeto lake li mkononi mwake kusafisha kabisa uwanda wake na kuikusanya ngano yake ghalani. Lakini atayachoma makapi kwa moto ambao hauwezi kuzimika.
13 Then comes Jesus from Galilee to Jordan to John, to be baptized of him.
Kisha Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka mto Yorodani kubatizwa na Yohana.
14 But John forbade him, saying, I have need to be baptized of you, and come you to me?
Lakini Yohana alitaka kumzuia akisema, “Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?''
15 And Jesus answering said to him, Suffer it to be so now: for thus it becomes us to fulfill all righteousness. Then he suffered him.
Yesu akajibu akasema, ''Ruhusu iwe hivi sasa, kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.'' Kisha Yohana akamruhusu.
16 And Jesus, when he was baptized, went up straightway out of the water: and, see, the heavens were opened to him, and he saw the Spirit of God descending like a dove, and lighting on him:
Baada ya kuwa amebatizwa, mara Yesu alitoka kwenye maji, na tazama, Mbingu zikafunguka kwake. Na alimuona Roho wa Mungu akishuka kwa mfano wa njiwa na kutulia juu yake.
17 And see a voice from heaven, saying, This is my beloved Son, in whom I am well pleased.
Tazama, sauti ilitoka mbinguni ikisema, “Huyu ni mwanangu mpendwa. Ninaye pendezwa sana naye.''

< Matthew 3 >