< Leviticus 2 >

1 And when any one bringeth a meal-offering unto the LORD, his offering shall be of fine flour; and he shall pour oil upon it, and put frankincense thereon.
“‘Mtu yeyote aletapo sadaka ya nafaka kwa Bwana, sadaka yake itakuwa ya unga laini. Atamimina mafuta juu yake, aweke uvumba juu yake,
2 And he shall bring it to Aaron's sons the priests; and he shall take thereout his handful of the fine flour thereof, and of the oil thereof, together with all the frankincense thereof; and the priest shall make the memorial-part thereof smoke upon the altar, an offering made by fire, of a sweet savour unto the LORD.
naye atapeleka kwa makuhani wana wa Aroni. Kuhani atachukua konzi moja iliyojaa unga laini na mafuta pamoja na uvumba wote, na kuuteketeza kama sehemu ya kumbukumbu juu ya madhabahu, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.
3 But that which is left of the meal-offering shall be Aaron's and his sons'; it is a thing most holy of the offerings of the LORD made by fire.
Sadaka ya nafaka iliyobaki ni ya Aroni na wanawe, ni sehemu ya sadaka iliyo takatifu sana iliyotolewa kwa Bwana kwa moto.
4 And when thou bringest a meal-offering baked in the oven, it shall be unleavened cakes of fine flour mingled with oil, or unleavened wafers spread with oil.
“‘Kama utaleta sadaka ya nafaka iliyookwa jikoni, itakuwa ya unga laini: maandazi yaliyotengenezwa bila kutiwa chachu, yaliyochanganywa na mafuta, au mikate myembamba iliyotengenezwa bila kutiwa chachu, na iliyopakwa mafuta.
5 And if thy offering be a meal-offering baked on a griddle, it shall be of fine flour unleavened, mingled with oil.
Iwapo sadaka yako ya nafaka imeandaliwa kwenye kikaango, itakuwa ni ya unga laini uliochanganywa na mafuta, bila chachu.
6 Thou shalt break it in pieces, and pour oil thereon; it is a meal-offering.
Ukande na kumimina mafuta juu yake; hii ni sadaka ya nafaka.
7 And if thy offering be a meal-offering of the stewing-pan, it shall be made of fine flour with oil.
Kama sadaka yako ya nafaka imepikwa kwenye sufuria, itatengenezwa kwa unga laini na mafuta.
8 And thou shalt bring the meal-offering that is made of these things unto the LORD; and it shall be presented unto the priest, and he shall bring it unto the altar.
Ilete hiyo sadaka ya nafaka iliyotengenezwa kwa vitu hivi kwa Bwana; mkabidhi kuhani ambaye ataipeleka madhabahuni.
9 And the priest shall take off from the meal-offering the memorial-part thereof, and shall make it smoke upon the altar — an offering made by fire, of a sweet savour unto the LORD.
Naye atatoa ile sehemu ya kumbukumbu kutoka kwenye hiyo sadaka ya nafaka na kuiteketeza juu ya madhabahu kuwa sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.
10 But that which is left of the meal-offering shall be Aaron's and his sons'; it is a thing most holy of the offerings of the LORD made by fire.
Sadaka ya nafaka iliyobaki ni ya Aroni na wanawe; ni sehemu ya sadaka iliyo takatifu sana ya sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto.
11 No meal-offering, which ye shall bring unto the LORD, shall be made with leaven; for ye shall make no leaven, nor any honey, smoke as an offering made by fire unto the LORD.
“‘Kila sadaka ya nafaka unayoleta kwa Bwana ni lazima ifanywe bila kutiwa chachu, kwa kuwa huna ruhusa kuchoma chachu yoyote au asali katika sadaka itolewayo kwa Bwana kwa moto.
12 As an offering of first-fruits ye may bring them unto the LORD; but they shall not come up for a sweet savour on the altar.
Unaweza kuzileta kwa Bwana kama sadaka ya malimbuko, lakini haziwezi kutolewa juu ya madhabahu kama harufu nzuri ya kupendeza.
13 And every meal-offering of thine shalt thou season with salt; neither shalt thou suffer the salt of the covenant of thy God to be lacking from thy meal-offering; with all thy offerings thou shalt offer salt.
Koleza sadaka zako zote za nafaka kwa chumvi. Usiache kuweka chumvi ya Agano la Mungu wako katika sadaka zako za nafaka; weka chumvi kwenye sadaka zako zote.
14 And if thou bring a meal-offering of first-fruits unto the LORD, thou shalt bring for the meal-offering of thy first-fruits corn in the ear parched with fire, even groats of the fresh ear.
“‘Kama ukileta malimbuko ya sadaka ya nafaka kwa Bwana, utatoa masuke yaliyopondwa ya nafaka mpya iliyookwa kwa moto.
15 And thou shalt put oil upon it, and lay frankincense thereon; it is a meal-offering.
Weka mafuta na uvumba juu yake; ni sadaka ya nafaka.
16 And the priest shall make the memorial-part of it smoke, even of the groats thereof, and of the oil thereof, with all the frankincense thereof; it is an offering made by fire unto the LORD.
Kuhani atateketeza ile sehemu ya kumbukumbu kutoka kwenye hiyo sadaka ya nafaka iliyopondwa kwa mafuta, pamoja na uvumba wote, kama sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto.

< Leviticus 2 >