< Ezekiel 6 >

1 And the word of the LORD came unto me, saying:
Neno la Bwana likanijia kusema,
2 'Son of man, set thy face toward the mountains of Israel, and prophesy against them,
“Mwanadamu, elekeza uso wako kukabili milima ya Israeli, utabiri dhidi yake
3 and say: Ye mountains of Israel, hear the word of the Lord GOD: Thus saith the Lord GOD concerning the mountains and concerning the hills, concerning the ravines and concerning the valleys: Behold, I, even I, will bring a sword upon you, and I will destroy your high places.
na useme: ‘Ee milima ya Israeli, sikia neno la Bwana Mwenyezi. Hili ndilo Bwana Mwenyezi aliambiayo milima na vilima, magenge na mabonde: Ninakaribia kuleta upanga dhidi yenu, nami nitapaharibu mahali penu pote pa juu pa kuabudia miungu.
4 And your altars shall become desolate, and your sun-images shall be broken; and I will cast down your slain men before your idols.
Madhabahu yenu yatabomolewa na madhabahu yenu ya kufukizia uvumba yatavunjavunjwa, nami nitawachinja watu wenu mbele ya sanamu zenu.
5 And I will lay the carcasses of the children of Israel before their idols; and I will scatter your bones round about your altars.
Nitazilaza maiti za Waisraeli mbele ya sanamu zao, nami nitatawanya mifupa yenu kuzunguka madhabahu yenu.
6 In all your dwelling-places the cities shall be laid waste, and the high places shall be desolate; that your altars may be laid waste and made desolate, and your idols may be broken and cease, and your sun-images may be hewn down, and your works may be blotted out.
Popote mnapoishi, miji hiyo itafanywa ukiwa na mahali pa juu pa kuabudia miungu patabomolewa, ili madhabahu yenu ifanywe ukiwa na kuharibiwa, sanamu zenu zitavunjavunjwa na kuharibiwa, madhabahu yenu ya kufukizia uvumba yatabomolewa na kila mlichokifanya kitakatiliwa mbali.
7 And the slain shall fall in the midst of you, and ye shall know that I am the LORD.
Watu wenu watachinjwa katikati yenu, nanyi mtatambua Mimi ndimi Bwana.
8 Yet will I leave a remnant, in that ye shall have some that escape the sword among the nations, when ye shall be scattered through the countries.
“‘Lakini nitawabakiza hai baadhi yenu, kwa kuwa baadhi yenu watanusurika kuuawa watakapokuwa wametawanyika katika nchi na mataifa.
9 And they that escape of you shall remember Me among the nations whither they shall be carried captives, how that I have been anguished with their straying heart, which hath departed from Me, and with their eyes, which are gone astray after their idols; and they shall loathe themselves in their own sight for the evils which they have committed in all their abominations.
Ndipo katika mataifa ambamo watakuwa wamechukuliwa mateka, wale ambao watanusurika watanikumbuka, jinsi ambavyo nimehuzunishwa na mioyo yao ya uzinzi, ambayo imegeukia mbali nami na macho yao ambayo yametamani sanamu zao. Watajichukia wenyewe kwa ajili ya uovu walioutenda na kwa ajili ya desturi zao za kuchukiza.
10 And they shall know that I am the LORD; I have not said in vain that I would do this evil unto them.
Nao watajua kuwa Mimi ndimi Bwana, sikuwaonya bure kuwa nitaleta maafa hayo yote juu yao.
11 Thus saith the Lord GOD: Smite with thy hand, and stamp with thy foot, and say: Alas! because of all the evil abominations of the house of Israel; for they shall fall by the sword, by the famine, and by the pestilence.
“‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Piga makofi, kanyaga chini kwa mguu na upige kelele, “Ole!” kwa sababu ya maovu yote na machukizo yote yanayofanywa na nyumba ya Israeli, kwa kuwa wataanguka kwa upanga, njaa na tauni.
12 He that is far off shall die of the pestilence; and he that is near shall fall by the sword; and he that remaineth and is besieged shall die by the famine; thus will I spend My fury upon them.
Yeye aliye mbali sana atakufa kwa tauni, naye aliye karibu atauawa kwa upanga, naye yule atakayenusurika na kubaki atakufa kwa njaa. Hivyo ndivyo nitakavyotimiza ghadhabu yangu dhidi yao.
13 And ye shall know that I am the LORD, when their slain men shall be among their idols round about their altars, upon every high hill, in all the tops of the mountains, and under every leafy tree, and under every thick terebinth, the place where they did offer sweet savour to all their idols.
Nao watajua kwamba Mimi ndimi Bwana, wakati maiti za watu wao zitakapokuwa zimelala katikati ya sanamu zao kuzunguka madhabahu yao, juu ya kila kilima kilichoinuka na juu ya vilele vyote vya milima, chini ya kila mti uliotanda na kila mwaloni wenye majani, yaani, sehemu walizofukizia uvumba kwa sanamu zao zote.
14 And I will stretch out My hand upon them, and make the land desolate and waste, more than the wilderness of Diblah, throughout all their habitations; and they shall know that I am the LORD.'
Nami nitanyoosha mkono wangu dhidi yao na kuifanya nchi yao ukiwa, kuanzia jangwani hadi Dibla, kila mahali wanapoishi. Ndipo watakapojua ya kwamba Mimi ndimi Bwana.’”

< Ezekiel 6 >