< Isaiah 64 >

1 Oh, that thou wouldest breake the heauens, and come downe, and that the mountaines might melt at thy presence!
''Oh, ikiwa umeigawa kwa kuifungua mbingu na kushuka chini! Milima inetikisika mbele yako,
2 As the melting fire burned, as the fire caused the waters to boyle, (that thou mightest declare thy Name to thy aduersaries) the people did tremble at thy presence.
ni kama vile moto uunguzao vichaka, moto uchemshao maji. Oh, jina lako lingejulikana kwa maadui wako, na ya kwamba mataifa yangetetemeka mbele yako!
3 When thou diddest terrible things, which we looked not for, thou camest downe, and the mountaines melted at thy presence.
Awali, ulipofanya mambo ya ajabu ambayo hatukuyategemea, ulishuka chini, milima ikatetemeka mbele zako.
4 For since the beginning of the world they haue not heard nor vnderstande with the eare, neither hath ye eye seene another God beside thee, which doeth so to him that waiteth for him.
Tangu nyakati za kale hakuna hata mmoja aliyesikia au kujua, wala jicho kuona Mungu yeyote karibu yake, ni nani afanyae mambo haya kwake anayemsubiri yeye.
5 Thou diddest meete him, that reioyced in thee, and did iustly: they remembred thee in thy wayes: beholde, thou art angrie, for we haue sinned: yet in them is continuance, and we shall be saued.
Umekuja kuwasidia wale wanaofurahia kutenda yaliyo ya haki, wale wanaowaita kuwakumbusha njia zake na kumheshimu yeye. Ulipatwa na hasira tulipotenda dhambi. Katika njia zako daima tutakombolewa.
6 But we haue all bene as an vncleane thing, and all our righteousnes is as filthie cloutes, and we all doe fade like a leafe, and our iniquities like the winde haue taken vs away.
Maana sote tumekuwa kama mmoja aliye na unajisi, na matendo yetu ya haki yamekuwa kama hedhi kali. Sote tumenyauka kama majani; maovu yetu, ni kama upepo, unaotupeperusha sisi mbali.
7 And there is none that calleth vpon thy Name, neither that stirreth vp himselfe to take holde of thee: for thou hast hid thy face from vs, and hast consumed vs because of our iniquities.
Hakuna hata mmoja anayeita jina lako, hakuna anayefanya jitihada za kukushika wewe; maana umeuficha uso wako mbali na sisi na kutufanya sisi kuwa takataka katika mkono wa maovu yetu.
8 But now, O Lord, thou art our Father: we are the clay, and thou art our potter, and we all are the worke of thine hands.
Na lakini, Yahwe, wewe ni baba yetu; sisi ni udongo. Wewe ni mfinyanzi wetu; sisi ni kazi ya mkono wako.
9 Be not angry, O Lord, aboue measure, neither remember iniquitie for euer: lo, we beseech thee beholde, we are all thy people.
Usiwe na hasira kubwa, Yahwe, wala daima usikumbuke maovu dhidi yetu, tafadhali sisi sote, watu wako.
10 Thine holy cities lye waste: Zion is a wildernes, and Ierusalem a desart.
Miji yenu mitakatifu imekuwa jangwa; Sayuni imekuwa jangwa, Yerusalemu imekuwa ukiwa.
11 The House of our Sanctuarie and of our glorie, where our fathers praysed thee, is burnt vp with fire and all our pleasant things are wasted.
Hekalu letu takatifu na zuri. mahali ambapo baba zetu walikusifu wewe, limeangamizwa kwa moto, na kila kilichokuwa karibu kiliharibiwa.
12 Wilt thou holde thy selfe still at these things, O Lord? wilt thou holde thy peace and afflict vs aboue measure?
Je unawezaje kuendelea kumshika, Yahwe? Unawezaje kutulia kimya na kuendelea kutufedhehesha sisi?''

< Isaiah 64 >