< Proverbs 15 >

1 A mild answer breaketh wrath: but a harsh word stirreth up fury.
Jawabu la upole hugeuza ghadhabu, bali neno liumizalo huchochea hasira.
2 The tongue of the wise adorneth knowledge: but the mouth of fools bubbleth out folly.
Ulimi wa mwenye hekima husifu maarifa, bali kinywa cha mpumbavu hufoka upumbavu.
3 The eyes of the Lord in every place behold the good and the evil.
Macho ya Bwana yako kila mahali, yakiwaangalia waovu na wema.
4 A peaceable tongue is a tree of life: but that which is immoderate, shall crush the spirit.
Ulimi uletao uponyaji ni mti wa uzima, bali ulimi udanganyao huponda roho.
5 A fool laugheth at the instruction of his father: but he that regardeth reproofs shall become prudent. In abundant justice there is the greatest strength: but the devices of the wicked shall be rooted out.
Mpumbavu hubeza maonyo ya baba yake, bali yeyote akubaliye maonyo huonyesha busara.
6 The house of the just is very much strength: and in the fruits of the wicked is trouble.
Nyumba ya mwenye haki ina hazina kubwa, bali mapato ya waovu huwaletea taabu.
7 The lips of the wise shall disperse knowledge: the heart of fools shall be unlike.
Midomo ya mwenye hekima hueneza maarifa, bali sivyo ilivyo mioyo ya wapumbavu.
8 The victims of the wicked are abominable to the Lord: the vows of the just are acceptable.
Bwana huchukia sana dhabihu za waovu, bali maombi ya wanyofu humfurahisha Mungu.
9 The way of the wicked is an abomination to the Lord: he that followeth justice is beloved by him.
Bwana huchukia sana njia ya waovu, bali huwapenda wale wafuatao haki.
10 Instruction is grievous to him that forsaketh the way of life: he that hateth reproof shall die.
Adhabu kali humngoja yeye aachaye njia; yeye achukiaye maonyo atakufa.
11 Hell and destruction are before the Lord: how much more the hearts of the children of men? (Sheol h7585)
Mauti na Uharibifu viko wazi mbele za Bwana: je, si zaidi sana mioyo ya wanadamu! (Sheol h7585)
12 A corrupt man loveth not one that reproveth him: nor will he go to the wise.
Mwenye mzaha huchukia maonyo; hatataka shauri kwa mwenye hekima.
13 A glad heart maketh a cheerful countenance: but by grief of mind the spirit is cast down.
Moyo wenye furaha hufanya uso uchangamke, bali maumivu ya moyoni huponda roho.
14 The heart of the wise seeketh instruction: and the mouth of fools feedeth on foolishness.
Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa, bali kinywa cha mpumbavu hujilisha upumbavu.
15 All the days of the poor are evil: a secure mind is like a continual feast.
Siku zote za wanaoonewa ni za taabu, bali moyo mchangamfu una karamu ya kudumu.
16 Better is a little with the fear of the Lord, than great treasures without content,
Afadhali kuwa na kidogo pamoja na kumcha Bwana, kuliko mali nyingi pamoja na ghasia.
17 It is better to be invited to herbs with love, than to a fatted calf with hatred.
Afadhali chakula cha mboga mahali palipo na upendo kuliko nyama ya ndama iliyonona pamoja na chuki.
18 A passionate man stirreth up strifes: he that is patient appeaseth those that are stirred up.
Mtu mwepesi wa hasira huchochea ugomvi, bali mtu mvumilivu hutuliza ugomvi.
19 The way of the slothful is as a hedge of thorns; the way of the just is without offence.
Njia ya mvivu imezibwa na miiba, bali njia ya mwenye haki ni barabara kuu.
20 A wise son maketh a father joyful: but the foolish man despiseth his mother.
Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake, bali mtu mpumbavu humdharau mama yake.
21 Folly is joy to the fool: and the wise man maketh straight his steps.
Upumbavu humfurahisha mtu ambaye hana akili, bali mtu mwenye ufahamu hushika njia iliyonyooka.
22 Designs are brought to nothing where there is no counsel: but where there are many counsellors, they are established.
Mipango hushindwa kufanikiwa kwa ajili ya kukosa ushauri, bali kukiwa na washauri wengi hufanikiwa.
23 A man rejoiceth in the sentence of his mouth: and a word in due time is best.
Mtu hupata furaha katika kutoa jibu linalofaa: je, ni zuri namna gani neno lililotoka kwa wakati wake!
24 The path of life is above for the wise, that he may decline from the lowest hell. (Sheol h7585)
Mapito ya uzima huelekea juu kwa ajili ya wenye hekima kumwepusha asiende chini kaburini. (Sheol h7585)
25 The Lord will destroy the house of the proud: and will strengthen the borders of the widow.
Bwana hubomoa nyumba ya mtu mwenye kiburi, bali huilinda mipaka ya mjane isiguswe.
26 Evil thoughts are an abomination to the Lord: and pure words most beautiful shall be confirmed by him.
Bwana huchukia sana mawazo ya mwovu, bali mawazo ya wale walio safi humfurahisha yeye.
27 He that is greedy of gain troubleth his own house: but he that hateth bribes shall live. By mercy and faith sins are purged away: and by the fear of the Lord every one declineth from evil.
Mtu mwenye tamaa huletea jamaa yake taabu, bali yeye achukiaye rushwa ataishi.
28 The mind of the just studieth obedience: the mouth of the wicked over floweth with evils.
Moyo wa mwenye haki hupima majibu yake, bali kinywa cha mwovu hufoka ubaya.
29 The Lord is far from the wicked: and he will hear the prayers of the just.
Bwana yuko mbali na waovu, bali husikia maombi ya wenye haki.
30 The light of the eyes rejoiceth the soul: a good name maketh the bones fat.
Mtazamo wa tabasamu huleta furaha moyoni, nazo habari njema huipa mifupa afya.
31 The ear that heareth the reproofs of life, shall abide in the midst of the wise.
Yeye asikilizaye maonyo yatoayo uzima atakuwa miongoni mwa wenye hekima.
32 He that rejecteth instruction, despiseth his own soul: but he that yieldeth to reproof possesseth understanding.
Yeye anayedharau maonyo hujidharau mwenyewe, bali yeyote anayekubali maonyo hupata ufahamu.
33 The fear of the Lord is the lesson of wisdom: and humility goeth before glory.
Kumcha Bwana humfundisha mtu hekima, nao unyenyekevu huja kabla ya heshima.

< Proverbs 15 >