< Matthew 6 >

1 Take heed that you do not your justice before men, to be seen by them: otherwise you shall not have a reward of your Father who is in heaven.
Zingatia kutotenda matendo ya haki mbele ya watu ili kujionyesha, vinginevyo hutapata thawabu kutoka kwa Baba aliye mbinguni.
2 Therefore when thou dost an almsdeed, sound not a trumpet before thee, as the hypocrites do in the synagogues and in the streets, that they may be honoured by men. Amen I say to you, they have received their reward.
Hivyo basi unapotoa usipige tarumbeta na kujisifu mwenyewe kama wanafiki wanavyofanya katika masinagogi na katika mitaa, ili kwamba watu wawasifu. Kweli nawaambia, wamekwisha kupokea thawabu yao.
3 But when thou dost alms, let not thy left hand know what thy right hand doth.
Lakini wewe unapotoa, mkono wako wa kushoto usijue kinachofanywa na mkono wa kulia,
4 That thy alms may be in secret, and thy Father who seeth in secret will repay thee.
ili kwamba zawadi yako itolewe kwa siri. Ndipo Baba yako aonaye sirini atakupatia thawabu yako.
5 And when ye pray, you shall not be as the hypocrites, that love to stand and pray in the synagogues and corners of the streets, that they may be seen by men: Amen I say to you, they have received their reward.
Na unapokuwa ukiomba, usiwe kama wanafiki, kwa kuwa wanapenda kusimama na kuomba kwenye masinagogi na kwenye kona za mitaani, ili kwamba watu wawatazame. Kweli nawaambia, wamekwishapokea thawabu yao.
6 But thou when thou shalt pray, enter into thy chamber, and having shut the door, pray to thy Father in secret: and thy Father who seeth in secret will repay thee.
Lakini wewe, unapo omba, ingia chumbani. Funga mlango, na uombe kwa kwa Baba yako aliye sirini. Ndipo Baba yako aonaye sirini atakupatia thawabu yako.
7 And when you are praying, speak not much, as the heathens. For they think that in their much speaking they may be heard.
Na unapokuwa ukiomba, usirudie rudie maneno yasiyo na maana kama mataifa wanavyofanya, kwa kuwa wanafikiri kwamba watasikiwa kwa sababu ya maneno mengi wanayosema.
8 Be not you therefore like to them, for your Father knoweth what is needful for you, before you ask him.
Kwa hiyo, usiwe kama wao, kwa kuwa Baba yako anatambua mahitaji yako hata kabla hujaomba kwake.
9 Thus therefore shall you pray: Our Father who art in heaven, hallowed be thy name.
Hivyo basi omba hivi: Baba yetu uliye mbinguni, ulitukuze jina lako.
10 Thy kingdom come. Thy will be done on earth as it is in heaven.
Ufalme wako uje, mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni.
11 Give us this day our supersubstantial bread.
Utupatiye leo mkate wetu wa kila siku.
12 And forgive us our debts, as we also forgive our debtors.
utusamehe deni zetu, kama nasi tunavyowasamehe wadeni wetu.
13 And lead us not into temptation. But deliver us from evil. Amen.
Na usitulete katika majaribu, lakini utuepushe kutoka kwa yule mwovu.'
14 For if you will forgive men their offences, your heavenly Father will forgive you also your offences.
Ikiwa mtawasemehe watu makosa yao, Baba yako aliye mbinguni pia atawasamehe ninyi.
15 But if you will not forgive men, neither will your Father forgive you your offences.
Lakini ikiwa hamtawasamehe makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe makosa yenu.
16 And when you fast, be not as the hypocrites, sad. For they disfigure their faces, that they may appear unto men to fast. Amen I say to you, they have received their reward.
Zaidi ya yote, unapokuwa umefunga, usioneshe sura ya huzuni kama wanafiki wanavyofanya, kwa kuwa wanakunja sura zao ili kwamba watu wawatambue wamefunga. Kweli ninakuambia, wamekwisha kupokea thawabu yao.
17 But thou, when thou fastest anoint thy head, and wash thy face;
Lakini wewe, unapokuwa umefunga, paka mafuta kichwa chako na uoshe uso wako.
18 That thou appear not to men to fast, but to thy Father who is in secret: and thy Father who seeth in secret, will repay thee.
Hivyo haitakuonesha mbele ya watu kuwa umefunga, lakini tu itakuwa kwa Baba yako aliye sirini. Na Baba yako aonaye sirini, atakupa thawabu yako.
19 Lay not up to yourselves treasures on earth: where the rust, and moth consume, and where thieves break through and steal.
Usijitunzie hazina yako mwenyewe hapa duniani, ambapo nondo na kutu huharibu, ambapo wezi huvunja na kuiba.
20 But lay up to yourselves treasures in heaven: where neither the rust nor moth doth consume, and where thieves do not break through, nor steal.
Badala yake, jitunzie hazina yako mwenyewe mbinguni, ambapo wala nondo wala kutu hawezi kuharibu, na ambapo wezi hawawezi kuvunja na kuiba.
21 For where thy treasure is, there is thy heart also.
Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo na moyo wako utakapokuwepo pia.
22 The light of thy body is thy eye. If thy eye be single, thy whole body shall be lightsome.
Jicho ni taa ya mwili. Kwa hiyo, ikiwa jicho lako ni zima, mwili wote utajazwa na nuru.
23 But if thy eye be evil thy whole body shall be darksome. If then the light that is in thee, be darkness: the darkness itself how great shall it be!
Lakini ikiwa jicho lako ni bovu, mwili wako wote umejaa giza totoro. Kwahiyo, ikiwa nuru ambayo imo ndani yako ni giza hasa, ni giza kubwa kiasi gani!
24 No man can serve two masters. For either he will hate the one, and love the other: or he will sustain the one, and despise the other. You cannot serve God and mammon.
Hakuna hata mmoja anayeweza kuwatumikia mabwana wawili, kwa kuwa atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au la sivyo atajitoa kwa mmoja na kumdharau mwingine. Hamuwezi kumtumikia Mungu na mali.
25 Therefore I say to you, be not solicitous for your life, what you shall eat, nor for your body, what you shall put on. Is not the life more than the meat: and the body more than the raiment?
Kwa hiyo nakuambia, usiwe na mashaka kuhusu maisha yako, kuwa utakula nini au utakunywa nini, au kuhusu mwili wako, utavaa nini. Je! Maisha si zaidi ya chakula na mwili zaidi ya mavazi?
26 Behold the birds of the air, for they neither sow, nor do they reap, nor gather into barns: and your heavenly Father feedeth them. Are not you of much more value than they?
Tazama ndege walioko angani. Hawapandi na hawavuni na hawakusanyi na kutunza ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha wao. Je ninyi si wa thamani zaidi kuliko wao?
27 And which of you by taking thought, can add to his stature by one cubit?
Na ni nani miongoni mwenu kwa kujihangaisha anaweza kuongeza dhiraa moja kwenye uhai wa maisha yake?
28 And for raiment why are you solicitous? Consider the lilies of the field, how they grow: they labour not, neither do they spin.
Na kwa nini mna kuwa na wasiwasi kuhusu mavazi? Fikiria kuhusu maua kwenye mashamba, jinsi yanavyokua. Hayafanyi kazi na hayawezi kujivisha.
29 But I say to you, that not even Solomon in all his glory was arrayed as one of these.
Bado ninawaambia, hata Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama mojawapo ya haya.
30 And if the grass of the field, which is today, and tomorrow is cast into the oven, God doth so clothe: how much more you, O ye of little faith?
Ikiwa Mungu anayavalisha majani katika mashamba, ambayo yadumu siku moja na kesho yanatupwa katika moto, je ni kwa kiasi gani atawavalisha ninyi, ninyi wenye imani ndogo?
31 Be not solicitous therefore, saying, What shall we eat: or what shall we drink, or wherewith shall we be clothed?
Kwa hiyo msiwe na wasiwasi nakusema, 'Je tutakula nini?' au “Je tutakunywa nini?” au “Je tutavaa nguo gani?”
32 For after all these things do the heathens seek. For your Father knoweth that you have need of all these things.
Kwa kuwa mataifa wanatafuta mambo haya, na Baba yenu wa mbinguni anajua kuwa mnahitaji hayo.
33 Seek ye therefore first the kingdom of God, and his justice, and all these things shall be added unto you.
Lakini kwanza tafuteni ufalme wake na haki yake na haya yote yatakabidhiwa kwako.
34 Be not therefore solicitous for tomorrow; for the morrow will be solicitous for itself. Sufficient for the day is the evil thereof.
Kwa hiyo, usione shaka kwa ajili ya kesho, kwa kuwa kesho itajishughulikia yenyewe. Kila siku inatosha kuwa na tatizo lake yenyewe.

< Matthew 6 >