< 1 Chronicles 25 >

1 Moreover David and the chief. officers of the army separated for the ministry the sons of Asaph, and of Heman, and of Idithun: to prophesy with harps, and with psalteries, and with cymbals according to their number serving in their appointed office.
Daudi, pamoja na majemadari wa jeshi, wakawatenga baadhi ya wana wa Asafu, wana wa Hemani na wana wa Yeduthuni, kwa ajili ya huduma ya kutoa unabii, wakitumia vinubi, zeze na matoazi. Hii ndiyo orodha ya watu waliofanya huduma hii:
2 Of the sons of Asaph: Zacchur, and Joseph, and Nathania, and Asarela, sons of Asaph: under the hand of Asaph prophesying near the king.
Kutoka kwa wana wa Asafu walikuwa: Zakuri, Yosefu, Nethania na Asarela. Wana wa Asafu walikuwa chini ya usimamizi wa Asafu, ambaye alitoa unabii chini ya usimamizi wa mfalme.
3 And of Idithun: the sons of Idithun, Godolias, Serf, Jeseias, and Hasabias, and Mathathias, six, under the hand of their father Idithun, who prophesied with a harp to give thanks and to praise the Lord.
Wana wa Yeduthuni walikuwa sita: Gedalia, Seri, Yeshaya, Shimei, Hashabia, na Matithia, nao walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao Yeduthuni, wao walikuwa wakitoa unabii wakitumia vinubi, wakimshukuru na kumtukuza Bwana.
4 Of Heman also: the sons of Heman, Bocciau, Mathaniau, Oziel, Subuel, and Jerimoth, Hananias, Hanani, Eliatha, Geddelthi, and Romemthiezer, and Jesbacassa, Mellothi, Othir, Mahazioth:
Wana wa Hemani walikuwa: Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli na Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti na Romamti-Ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri na Mahaziothi.
5 All these were the sons of Heman the seer of the king in the words of God, to lift up the horn: and God gave to Heman fourteen sons and three daughters.
Wote hawa walikuwa wana wa Hemani mwonaji wa mfalme. Aliwapata wana hawa kutokana na ahadi ya Mungu ili kumwinua. Mungu alimpa Hemani wana kumi na wanne na binti watatu.
6 All these under their father’s hand were distributed to sing in the temple of the Lord, with cymbals, and psalteries and harps, for the service of the house of the Lord near the king: to wit, Asaph, and Idithun, and Heman.
Hawa wanaume wote walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao kwa ajili ya uimbaji katika Hekalu la Bwana wakitumia matoazi, zeze na vinubi, kwa ajili ya huduma katika nyumba ya Mungu. Asafu, Yeduthuni na Hemani walikuwa chini ya usimamizi wa mfalme.
7 And the number of them with their brethren, that taught the song of the Lord, all the teachers, were two hundred and eighty-eight,
Pamoja na ndugu zao wote walikuwa wamefundishwa na kuwa stadi wa uimbaji kwa Bwana. Idadi yao walikuwa 288.
8 And they cast lots by their courses, the elder equally with the younger, the learned and the unlearned together.
Vijana kwa wazee, walimu kwa wanafunzi, wote walipanga kazi zao kwa kupiga kura.
9 And the first lot came forth to Joseph, who was of Asaph. The second to Godolias, to him and his sons, and his brethren twelve.
Kura ya kwanza, ambayo ilikuwa kwa ajili ya Asafu, ilimwangukia Yosefu, wanawe na jamaa zake, 12 Ya pili ikamwangukia Gedalia, yeye na wanawe pamoja na jamaa zake, 12
10 The third to Zachur, to his sons and his brethren twelve.
Ya tatu ikamwangukia Zakuri, wanawe na jamaa zake, 12
11 The fourth to Isari, to his sons and his brethren twelve.
ya nne ikamwangukia Isri, // wanawe na jamaa zake, 12
12 The fifth to Nathania, to his sons and his brethren twelve.
ya tano ikamwangukia Nethania, wanawe na jamaa zake, 12
13 The sixth to Bocciau, to his sons and his brethren twelve.
ya sita ikamwangukia Bukia, wanawe na jamaa zake, 12
14 The seventh to Isreela, to his sons and his brethren twelve.
ya saba ikamwangukia Yesarela, // wanawe na jamaa zake, 12
15 The eighth to Jesaia, to his sons and his brethren twelve.
ya nane ikamwangukia Yeshaya, wanawe na jamaa zake, 12
16 The ninth to Mathanaias, to his sons and his brethren twelve.
ya tisa ikamwangukia Matania, wanawe na jamaa zake, 12
17 The tenth to Semeias, to his sons and his brethren twelve.
ya kumi ikamwangukia Shimei, wanawe na jamaa zake, 12
18 The eleventh to Azareel, to his sons and his brethren twelve.
ya kumi na moja ikamwangukia Azareli, // wanawe na jamaa zake, 12
19 The twelfth to Hasabia, to his sons and his brethren twelve.
ya kumi na mbili ikamwangukia Hashabia, wanawe na jamaa zake, 12
20 The thirteenth to Subael, to his sons and his brethren twelve.
ya kumi na tatu ikamwangukia Shubaeli, wanawe na jamaa zake, 12
21 The fourteenth to Mathathias, to his sons and his brethren twelve.
ya kumi na nne ikamwangukia Matithia, wanawe na jamaa zake, 12
22 The fifteenth to Jerimoth, to his sons and his brethren twelve.
ya kumi na tano ikamwangukia Yeremothi, wanawe na jamaa zake, 12
23 The sixteenth to Hananias, to his sons and his brethren twelve.
Ya kumi na sita ikamwangukia Hanania, wanawe na jamaa zake, 12
24 The seventeenth to Jesbacassa, to his sons and his brethren twelve.
ya kumi na saba ikamwangukia Yoshbekasha, wanawe na jamaa zake, 12
25 The eighteenth to Hanani, to his sons and his brethren twelve.
ya kumi na nane ikamwangukia Hanani, wanawe na jamaa zake, 12
26 The nineteenth to Mellothi, to his sons and his brethren twelve.
ya kumi na tisa ikamwangukia Malothi, wanawe na jamaa zake, 12
27 The twentieth to Eliatha, to his sons and his brethren twelve.
ya ishirini ikamwangukia Eliatha, wanawe na jamaa zake, 12
28 The one and twentieth to Othir, to his sons and his brethren twelve.
ya ishirini na moja ikamwangukia Hothiri, wanawe na jamaa zake, 12
29 The two and twentieth to Geddelthi, to his sons and his brethren twelve.
ya ishirini na mbili ikamwangukia Gidalti, wanawe na jamaa zake, 12
30 The three and twentieth to Mahazioth, to his sons and his brethren twelve.
ya ishirini na tatu ikamwangukia Mahaziothi, wanawe na jamaa zake, 12
31 The four and twentieth to Romemthiezer, to his sons and his brethren twelve.
ya ishirini na nne ikamwangukia Romamti-Ezeri, wanawe na jamaa zake, 12.

< 1 Chronicles 25 >