< Luke 19 >

1 And he entered and was passing through Jericho.
Yesu aliingia na kupita katikati ya Yeriko.
2 And behold, a man called by name Zacchæus; and he was a chief publican, and he was rich.
Na hapo palikuwa na mtu mmoja aitwaye Zakayo. Ambaye alikuwa mkuu wa watoza ushuru tena mtu tajiri.
3 And he sought to see Jesus who he was; and could not for the crowd, because he was little of stature.
Alikuwa anajaribu kumwona Yesu ni mtu wa namna gani, lakini hakuweza kuona kwa sababu ya umati wa watu, kwa kuwa alikuwa mfupi wa kimo.
4 And he ran on before, and climbed up into a sycomore tree to see him: for he was to pass that way.
Hivyo, alitangulia mbio mbele za watu, akapanda juu ya mkuyu ili aweze kumwona, kwa sababu Yesu alikaribia kupita njia hiyo.
5 And when Jesus came to the place, he looked up, and said unto him, Zacchæus, make haste, and come down; for to-day I must abide at thy house.
Wakati Yesu alipofika mahali pale, aliangalia juu akamwambia, 'Zakayo, shuka upesi, maana leo ni lazima nishinde nyumbani mwako.'
6 And he made haste, and came down, and received him joyfully.
Akafanya haraka, akashuka na kumkaribisha kwa furaha.
7 And when they saw it, they all murmured, saying, He is gone in to lodge with a man that is a sinner.
Watu wote walipoona hayo, wakalalamika, wakisema, 'Amekwenda kumtembelea mtu mwenye dhambi.'
8 And Zacchæus stood, and said unto the Lord, Behold, Lord, the half of my goods I give to the poor; and if I have wrongfully exacted aught of any man, I restore fourfold.
Zakayo akasimama akamwambia Bwana, Tazama Bwana nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimemnyang'anya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara nne. '
9 And Jesus said unto him, To-day is salvation come to this house, forasmuch as he also is a son of Abraham.
Yesu akamwambia, 'Leo wokovu umefika katika nyumba hii, kwa sababu yeye pia ni mwana wa Ibrahimu.
10 For the Son of man came to seek and to save that which was lost.
Kwa maana Mwana wa Mtu amekuja kutafuta na kuokoa watu waliopotea. '
11 And as they heard these things, he added and spake a parable, because he was nigh to Jerusalem, and [because] they supposed that the kingdom of God was immediately to appear.
Waliposikia hayo, aliendelea kuongea na alitoa mfano, kwa sababu alikuwa karibu na Yerusalemu, na wao walidhani ya kuwa ufalme wa Mungu ulikuwa karibu kuonekana mara moja.
12 He said therefore, A certain nobleman went into a far country, to receive for himself a kingdom, and to return.
Hivyo akawaambia, 'Ofisa mmoja alikwenda nchi ya mbali ili apokee ufalme na kisha aurudi.
13 And he called ten servants of his, and gave them ten pounds, and said unto them, Trade ye [herewith] till I come.
Aliwaita watumishi wake kumi, akawapa mafungu kumi, akawaambia, 'fanyeni biashara mpaka nitakaporudi.'
14 But his citizens hated him, and sent an ambassage after him, saying, We will not that this man reign over us.
Lakini wananchi wake walimchukia na hivyo wakatuma wajumbe waende kumfuata na kusema, 'Hatutaki mtu huyu atutawale.'
15 And it came to pass, when he was come back again, having received the kingdom, that he commanded these servants, unto whom he had given the money, to be called to him, that he might know what they had gained by trading.
Ikawa aliporudi nyumbani baada ya kufanywa mfalme, akaamuru wale watumishi aliokuwa amewaachia fedha waitwe kwake, apate kujua faida gani waliyoipata kwa kufanya biashara.
16 And the first came before him, saying, Lord, thy pound hath made ten pounds more.
Wa kwanza akaja, akasema, `Bwana, fungu lako limefanya mafungu kumi zaidi. '
17 And he said unto him, Well done, thou good servant: because thou wast found faithful in a very little, have thou authority over ten cities.
Huyo Ofisa akamwambia, Vema, mtumishi mwema. Kwa sababu ulikuwa mwaminifu katika jambo dogo, utakuwa na madaraka juu ya miji kumi. '
18 And the second came, saying, Thy pound, Lord, hath made five pounds.
Wa pili akaja, akasema, 'Bwana, fungu lako limefanya mafungu matano.'
19 And he said unto him also, Be thou also over five cities.
Huyo Afisa akamwambia, 'Chukua mamlaka juu ya miji mitano.'
20 And another came, saying, Lord, behold, [here is] thy pound, which I kept laid up in a napkin:
Na mwingine akaja, akasema, `Bwana hii hapa fedha yako, ambayo niliihifadhi salama katika kitambaa,
21 for I feared thee, because thou art an austere man: thou takest up that which thou layedst not down, and reapest that which thou didst not sow.
kwa maana niliogopa kwa sababu wewe ni mtu mkali. Unaondoa kile usichokiweka na kuvuna usichopanda. '
22 He saith unto him, Out of thine own mouth will I judge thee, thou wicked servant. Thou knewest that I am an austere man, taking up that which I laid not down, and reaping that which I did not sow;
Huyo Ofisa akamwambia, 'Kwa maneno yako mwenyewe, nitakuhukumu, ewe mtumishi mbaya. Ulijua kwamba mimi ni mtu mkali, nachukua nisichokiweka na kuvuna ambacho sikupanda.
23 then wherefore gavest thou not my money into the bank, and I at my coming should have required it with interest?
Basi, mbona hukuweka fedha yangu katika benki, ili nikirudi niichukue pamoja na faida?
24 And he said unto them that stood by, Take away from him the pound, and give it unto him that hath the ten pounds.
Ofisa akawaambia watu waliokuwa wamesimama hapo, 'Mnyang'anyeni hilo fungu na kumpa yule mwenye mafungu kumi.'
25 And they said unto him, Lord, he hath ten pounds.
Wakamwambia, `Bwana, yeye ana mafungu kumi. '
26 I say unto you, that unto every one that hath shall be given; but from him that hath not, even that which he hath shall be taken away from him.
'Nawaambia, kila mtu ambaye anacho atapewa zaidi, lakini ambaye hana, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
27 But these mine enemies, that would not that I should reign over them, bring hither, and slay them before me.
Lakini hawa maadui zangu, ambao hawakutaka niwe Mfalme wao, waleteni hapa na kuwaua mbele yangu. ''
28 And when he had thus spoken, he went on before, going up to Jerusalem.
Baada ya kusema hayo, aliendelea mbele akipanda kwenda Yerusalemu.
29 And it came to pass, when he drew nigh unto Bethphage and Bethany, at the mount that is called Olivet, he sent two of the disciples,
Ikawa alipokaribia Bethfage na Bethania, karibu na mlima wa Mizeituni, aliwatuma wanafunzi wake wawili,
30 saying, Go your way into the village over against [you]; in which as ye enter ye shall find a colt tied, whereon no man ever yet sat: loose him, and bring him.
akisema: `Nendeni katika kijiji cha jirani. Mkiingia, mtakuta mwana-punda hajapandwa bado. Mfungueni, mkamlete kwangu.
31 And if any one ask you, Why do ye loose him? thus shall ye say, The Lord hath need of him.
Kama mtu akiwauliza, `Mbona mnamfungua? ' Semeni, “Bwana anamhitaji. ''
32 And they that were sent went away, and found even as he had said unto them.
Wale waliotumwa wakaenda wakamwona mwana-punda kama Yesu alivyokuwa amewaambia.
33 And as they were loosing the colt, the owners thereof said unto them, Why loose ye the colt?
Walipokuwa wanamfungua mwana punda wamiliki wakawaambia, 'Kwa nini mnamfungua mwana punda huyu?'
34 And they said, The Lord hath need of him.
Wakasema, `Bwana anamhitaji. '
35 And they brought him to Jesus: and they threw their garments upon the colt, and set Jesus thereon.
Basi, wakampelekea Yesu, wakatandika nguo zao juu ya mwana punda na wakampandisha Yesu juu yake.
36 And as he went, they spread their garments in the way.
Alipokuwa akienda watu wakatandaza mavazi yao barabarani.
37 And as he was now drawing nigh, [even] at the descent of the mount of Olives, the whole multitude of the disciples began to rejoice and praise God with a loud voice for all the mighty works which they had seen;
Alipokuwa anateremka mlima wa Mizeituni, jumuiya yote ya wanafunzi wakaanza kushangilia na kumtukuza Mungu kwa sauti kubwa, kwa sababu ya mambo makuu waliyoyaona,
38 saying, Blessed [is] the King that cometh in the name of the Lord: peace in heaven, and glory in the highest.
wakisema, 'Ndiye mbarikiwa Mfalme ajaye kwa jina la Bwana! Amani mbinguni, na utukufu juu!'
39 And some of the Pharisees from the multitude said unto him, Teacher, rebuke thy disciples.
Baadhi ya Mafarisayo katika mkutano wakamwambia, Mwalimu, wanyamazishe wanafunzi wako. '
40 And he answered and said, I tell you that, if these shall hold their peace, the stones will cry out.
Yesu akajibu, akasema, `Nawaambieni, kama hawa wakinyamaza, mawe yatapaza sauti. '
41 And when he drew nigh, he saw the city and wept over it,
Yesu alipoukaribia mji aliulilia,
42 saying, If thou hadst known in this day, even thou, the things which belong unto peace! but now they are hid from thine eyes.
akisema, laiti ungelijua hata wewe, katika siku hii mambo ambayo yanayokuletea amani! Lakini sasa yamefichika machoni pako.
43 For the days shall come upon thee, when thine enemies shall cast up a bank about thee, and compass thee round, and keep thee in on every side,
Kwa kuwa siku zinakuja ambapo adui zako watajenga boma karibu na wewe, na kukuzunguka na kukukandamiza kutoka kila upande.
44 and shall dash thee to the ground, and thy children within thee; and they shall not leave in thee one stone upon another; because thou knewest not the time of thy visitation.
Watakuangusha chini wewe na watoto wako. Hawatakuachia hata jiwe moja juu ya jingine, kwa sababu haukutambua wakati Mungu alipokuwa anajaribu kukuokoa'.
45 And he entered into the temple, and began to cast out them that sold,
Yesu aliingia Hekaluni, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakiuza,
46 saying unto them, It is written, And my house shall be a house of prayer: but ye have made it a den of robbers.
akiwaambia, “Imeandikwa, 'Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala,' lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi”.
47 And he was teaching daily in the temple. But the chief priests and the scribes and the principal men of the people sought to destroy him:
Kwa hiyo, Yesu alikuwa akifundisha kila siku hekaluni. Makuhani wakuu na walimu wa Sheria na viongozi wa watu walitaka kumuua,
48 and they could not find what they might do; for the people all hung upon him, listening.
lakini hawakuweza kupata njia ya kufanya hivyo, kwa sababu watu wote walikuwa wakimsikiliza kwa makini.

< Luke 19 >