< Job 9 >

1 Then Job answered,
Kisha Ayubu akajibu na kusema,
2 “Truly I know that it is so, but how can man be just with God?
“kweli najua kwamba ndivyo hivyo. Lakini ni kwa namna gani mtu anakuwa na haki kwa Mungu?
3 If he is pleased to contend with him, he cannot answer him one time in a thousand.
Kama akitaka kujibishana na Mungu, hatamjibu yeye mara moja katika elfu zaidi.
4 God is wise in heart, and mighty in strength. Who has hardened himself against him and prospered?
Mungu ni mwenye hekima moyoni na ukuu katika nguvu; ni nani daima aliyejifanya mwenyewe kuwa mgumu dhidi yake na akafanikiwa? -
5 He removes the mountains, and they do not know it, when he overturns them in his anger.
ambaye huiondoa milima bila kumtahadharisha yeyote wakati akiipindua katika hasira zake -
6 He shakes the earth out of its place. Its pillars tremble.
ambaye huitikisa nchi itoke mahali pake na mihimili yake hutikisika.
7 He commands the sun and it does not rise, and seals up the stars.
Ni Mungu yule yule ambaye huliamuru jua lisichomoze, nalo halichomozi, na ambaye huzihifadhi nyota,
8 He alone stretches out the heavens, and treads on the waves of the sea.
ambaye peke yake ni mwenye kupanua mbingu na kuyatuliza mawimbi ya bahari,
9 He makes the Bear, Orion, and the Pleiades, and the rooms of the south.
ambaye huumba Dubu, Orioni, kilima, na makundi ya nyota ya kusini.
10 He does great things past finding out; yes, marvelous things without number.
Ni Mungu yule yule atendaye mambo makuu, mambo yasiyofahamika - hasa, mambo ya ajabu yasiyohesabika.
11 Behold, he goes by me, and I do not see him. He passes on also, but I do not perceive him.
Tazama, huenda karibu nami, na siwezi kumuona yeye; pia hupita kwenda mbele, lakini ni simtambue.
12 Behold, he snatches away. Who can hinder him? Who will ask him, ‘What are you doing?’
Kama akichukua kitu chochote, nani atamzuia? Nani awezaye kumuuliza, 'unafanya nini?'
13 “God will not withdraw his anger. The helpers of Rahab stoop under him.
Mungu hataondoa hasira yake; wamsaidiao Rahabu huinama chini yake.
14 How much less will I answer him, and choose my words to argue with him?
Je ni upungufu kiasi gani mimi nitamjibu, je nichague maneno kuhojiana naye?
15 Though I were righteous, yet I would not answer him. I would make supplication to my judge.
Hata kama ni mwenye haki, nisingelimjibu; ningeomba msamaha tu kwa hukumu yangu.
16 If I had called, and he had answered me, yet I would not believe that he listened to my voice.
Hata kama ningelimwita na yeye akanitikia, nisingeamini kuwa ameisikia sauti yangu.
17 For he breaks me with a storm, and multiplies my wounds without cause.
kwa kuwa yeye anidhoofishaye kwa dhoruba na kuyaongeza majeraha yangu pasipo sababu.
18 He will not allow me to catch my breath, but fills me with bitterness.
Yeye hataki hata kuniruhusu nipate kuvuta pumzi; badala yake, hunijaza uchungu.
19 If it is a matter of strength, behold, he is mighty! If of justice, ‘Who,’ says he, ‘will summon me?’
Kama ni habari ya nguvu, tazama! yeye ni mwenye uwezo! Kama ni habari ya haki, ni nani atakaye mhukumu?
20 Though I am righteous, my own mouth will condemn me. Though I am blameless, it will prove me perverse.
Ingawa ni mwenye haki, kinywa changu mwenyewe kitanihukumu; na ingawa ni mtakatifu, maneno yangu yatashuhudia kuwa ni mwenye kosa.
21 I am blameless. I do not respect myself. I despise my life.
Mimi ni mtakatifu, lakini siijali zaidi nafsi yangu; Naudharau uhai wangu mwenyewe.
22 “It is all the same. Therefore I say he destroys the blameless and the wicked.
Haileti tofauti yoyote, kwa sababu hiyo nasema kwamba yeye huangamiza watu wasio na makosa na waovu pia.
23 If the scourge kills suddenly, he will mock at the trial of the innocent.
Kama hilo pigo likiua ghafla, yeye atafurahi mateso yake mtu asiye na kosa.
24 The earth is given into the hand of the wicked. He covers the faces of its judges. If not he, then who is it?
Dunia imetiwa mkononi mwa watu waovu; Mungu hufunika nyuso za waamuzi wake. kama si yeye hufanya, ni nani basi?
25 “Now my days are swifter than a runner. They flee away. They see no good.
Siku zangu zinapita haraka kuliko tarishi akimbiae; siku zangu zinakimbia mbali; wala hazioni mema mahali popote.
26 They have passed away as the swift ships, as the eagle that swoops on the prey.
Zinapita kama mashua zilizoundwa kwa mafunjo ziendazo kwa kasi, na zinakasi kama tai ashukaye upesi katika mawindo yake.
27 If I say, ‘I will forget my complaint, I will put off my sad face, and cheer up,’
Kama ni kisema kwamba mimi nitasahau kuhusu manung'uniko yangu, kwamba nitaacha kuonyesha sura ya huzuni na kuwa na furaha,
28 I am afraid of all my sorrows. I know that you will not hold me innocent.
Mimi nitaziogopa huzuni zangu zote kwa sababu nafahamu kuwa hutanihesabu kuwa sina hatia.
29 I will be condemned. Why then do I labor in vain?
Nitahukumiwa; kwa nini, basi, nitaabike bure?
30 If I wash myself with snow, and cleanse my hands with lye,
Kama najiosha mwenyewe kwa maji ya theluji na kuitakasa mikono yangu na kuwa safi zaidi,
31 yet you will plunge me in the ditch. My own clothes will abhor me.
Mungu atanitumbukiza shimoni, na nguo zangu mwenyewe zitanichukia.
32 For he is not a man, as I am, that I should answer him, that we should come together in judgment.
Kwa kuwa Mungu si mtu, kama mimi, kwamba naweza kumjibu, hata tukaribiane katika hukumu.
33 There is no umpire between us, that might lay his hand on us both.
Hakuna hakimu baina yetu awezaye kuweka mkono wake juu yetu sote.
34 Let him take his rod away from me. Let his terror not make me afraid;
Hakuna hakimu mwingine ambaye anaweza kuniondolea fimbo ya Mungu, awezaye kuzuia kitisho chake kisinitie hofu. kisha ningesema na nisimuogope.
35 then I would speak, and not fear him, for I am not so in myself.
Lakini kama mambo yalivyo sasa, sitaweza kufanya hivyo.

< Job 9 >