< Luke 15 >

1 Now all the tax collectors and sinners were approaching him to hear him.
Siku moja, watoza ushuru na wahalifu wengi walikwenda kumsikiliza Yesu.
2 And the Pharisees and the scholars murmured, saying, This man receives sinners and eats with them.
Mafarisayo na walimu wa Sheria wakaanza kunung'unika: “Mtazameni mtu huyu! Anawakaribisha wenye dhambi, na tena anakula nao.”
3 And he spoke this parable to them, saying,
Yesu akawajibu kwa mfano:
4 What man of you, having a hundred sheep, and having lost one of them, does not leave behind the ninety-nine in the wilderness, and go for that which was lost until he finds it?
“Hivi, mtu akiwa na kondoo mia, akigundua kwamba mmoja wao amepotea, atafanya nini? Atawaacha wale tisini na tisa mbugani, na kwenda kumtafuta yule aliyepotea mpaka ampate.
5 And when he finds it, he lays it on his shoulders, rejoicing.
Akimpata, atambeba mabegani kwa furaha.
6 And when he comes to the house, he calls together his men friends and his men neighbors, saying to them, Rejoice with me, because I have found my sheep that was lost.
Anapofika nyumbani, atawaita rafiki zake akiwaambia, Furahini pamoja nami, kwa sababu nimempata yule kondoo wangu aliyepotea.
7 I say to you, that thus there will be joy in heaven over one sinner who repents, than over ninety-nine righteous men who have no need of repentance.
Kadhalika nawaambieni, ndivyo kutakavyokuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya kutubu kwa mwenye dhambi mmoja, kuliko kwa ajili ya watu tisini na tisa wanaojiona kuwa wema, wasiohitaji kutubu.
8 Or what woman having ten drachmas, if she lose one drachma, does not light a lamp, and sweep the house, and seek diligently until she finds it?
“Au mwaonaje? Tuseme mwanamke fulani ana sarafu kumi za fedha, akipoteza moja, atafanya nini? Atawasha taa, aifagie nyumba na kuitafuta kwa uangalifu mpaka aipate.
9 And when she has found it, she calls together her lady friends and lady neighbors, saying, Rejoice with me, because I found the drachma that I lost.
Akiipata, atawaita rafiki na jirani zake akisema, Furahini pamoja nami, kwa sababu nimeipata ile sarafu yangu iliyopotea.
10 Thus I say to you, there becomes joy in the presence of the agents of God over one sinner who repents.
Kadhalika nawaambieni, ndivyo watakavyofurahi malaika wa Mungu kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja anayetubu.”
11 And he said, A certain man had two sons,
Yesu akaendelea kusema, “Kulikuwa na mtu mmoja mwenye wana wawili.
12 and the younger of them said to his father, Father, give me the portion of goods that falls to me. And he divided to them his living.
Yule mdogo, alimwambia baba yake: Baba, nipe urithi wangu. Naye akawagawia mali yake.
13 And not many days after, the younger son, having gathered all together, journeyed into a distant country, and there he squandered his wealth living recklessly.
Baada ya siku chache, yule mdogo aliuza urithi wake, akasafiri na fedha aliyopata, akaenda nchi ya mbali ambako aliitumia ovyo.
14 And when he spent all, a mighty famine developed in that country, and he began to be in want.
Alipomaliza kutumia kila kitu, kukatokea njaa kali katika nchi ile, naye akaanza kuhangaika.
15 And having gone, he was joined to one of the citizens of that country, and he sent him into his fields to feed swine.
Akaomba kazi kwa mwananchi mtu mmoja wa huko naye akampeleka shambani mwake kulisha nguruwe.
16 And he longed to fill his belly from the husks that the swine ate, and no man gave to him.
Alitamani kula maganda waliyokula wale nguruwe, ila hakuna mtu aliyempa kitu.
17 But when he came to himself, he said, How many hired men of my father's have abundance of loaves, but I am perishing with hunger.
Alipoanza kupata akili akafikiri: Mbona kuna wafanyakazi wengi wa baba yangu wanaokula na kusaza, nami ninakufa njaa?
18 After rising, I will go to my father, and will say to him, Father, I have sinned against heaven and in thy sight.
Nitarudi kwa baba yangu na kumwambia: Baba, nimemkosea Mungu, na nimekukosea wewe pia.
19 I am no more worthy to be called thy son. Make me as one of thy hired men.
Sistahili hata kuitwa mwanao. Nifanye kama mmoja wa wafanyakazi wako.
20 And having risen, he went to his father. But while he was still distant, afar off, his father saw him and felt compassion. And having ran, he fell on his neck, and kissed him much.
Basi, akaanza safari ya kurudi kwa baba yake. Alipokuwa bado yu mbali, baba yake alimwona, na kwa moyo wa huruma alimkimbilia, akamkumbatia na kumbusu.
21 And the son said to him, Father, I have sinned against heaven and in thy sight. I am no more worthy to be called thy son.
“Mwanawe akamwambia: Baba, nimemkosea Mungu, na nimekukosea wewe pia. Sistahili hata kuitwa mwanao.
22 But the father said to his bondmen, Bring forth the best robe and clothe him, and give a ring for his hand, and shoes for his feet.
Lakini baba yake akawaambia watumishi wake: Haraka! Leteni nguo nzuri mkamvike! Mvisheni pete na viatu!
23 And having brought the fatted calf, kill it, and having eaten, we will be cheerful,
Mchinjeni ndama mnono; tule kusherehekea!
24 because this my son was dead, and became alive again. And he was lost, and is found. And they began to be cheerful.
Kwa sababu huyu mwanangu alikuwa amekufa, kumbe yu mzima alikuwa amepotea, lakini sasa amepatikana. Wakaanza kufanya sherehe.
25 But his elder son was in a field. And while coming, having approached the house, he heard music and dancing.
“Wakati huo kaka yake alikuwa bado shambani. Alipokuwa akirudi na kukaribia nyumbani akasikia vifijo na ngoma.
26 And having summoned one of the boys, he inquired what these things might be.
Akamwita mmoja wa watumishi, akamwuliza: Kuna nini?
27 And he said to him, Thy brother arrived, and thy father has killed the fatted calf, because he received him back healthy.
Huyo mtumishi akamwambia: Ndugu yako amerudi nyumbani, na baba yako amemchinjia ndama mnono kwa kuwa amempata akiwa salama salimini.
28 But he was angry, and would not go in. Therefore, his father having come out, he called him.
Huyo kijana mkubwa akawaka hasira hata akakataa kuingia nyumbani. Baba yake akatoka nje na kumsihi aingie.
29 But having answered, he said to his father, Lo, so many years do I serve thee, and I never passed by a commandment of thine, and yet thou never gave me a goat that I might be merry with my friends.
Lakini yeye akamjibu: Kumbuka! Miaka yote nimekutumikia, sijavunja amri yako hata mara moja. Umenipa nini? Hujanipa hata mwana mbuzi mmoja nikafanye sherehe pamoja na rafiki zangu!
30 But when this thy son came, who has devoured thy living with harlots, thou killed for him the fatted calf.
Lakini mtoto wako huyu aliyekula mali yako pamoja na makahaba, mara tu alipokuja umemchinjia yule ndama mnono.
31 And he said to him, Child, thou are always with me, and all my things are yours.
Baba yake akamjibu: Mwanangu, wewe uko pamoja nami siku zote, na kila nilicho nacho ni chako.
32 But it was needful to make merry and be glad, because this thy brother was dead, and became alive again, and was lost, and was found.
Ilitubidi kufanya sherehe na kufurahi, kwa sababu huyu ndugu yako alikuwa amekufa, kumbe yu mzima; alikuwa amepotea, lakini sasa amepatikana.”

< Luke 15 >