< Nahum 2 >

1 Een vernieler trekt op u af: Bewaak de vesting, Let op de weg, de lenden omgord, Al uw krachten ingespannen!
Yule ambaye atakuharibu vipande vipande anakuja dhidi yako. Linda kuta za mji, linda barabara, jitieni nguvu ninyi wenyewe, yakusanyeni majeshi yenu.
2 Waarachtig Jahweh zal de wijngaard van Jakob herstellen, Als Israëls glorie: Omdat de rovers hem hebben geplunderd, En zijn ranken hebben vernield!
Maana Yehova anarejesha fahari ya Yakobo, kama fahari ya Israeli, ingawa wateka nyara waliwaharibu na kuharibu matawi ya zabibu zao.
3 Het schild van zijn helden is rood geverfd, Zijn krijgers zijn purper gekleurd; Als vuur flikkert het staal van zijn wagens, Hij staat nu ten strijde gereed, de lansen worden gezwaaid.
Ngao za mashujaa wake ni nyekundu, na watu hodari wamevaa nguo nyekundu; magari ya vita yameandaliwa yanang'ara kwenye vyuma vyake wakati wa mchana, na mikuki ya mivinje inarushwa hewani.
4 Over de wegen razen de wagens, Over de vlakten jagen ze voort; Ze gloeien als fakkels Als bliksemschichten schieten ze uit.
Magari ya vita yapo kasi kwenye mitaa; yanakimbia mbele na nyuma katika mitaa. Yapo kama kurunzi, na yanakimbia kama radi.
5 Hij roept zijn dapperen op, Ze struikelen in hun vaart, En spoeden zich naar de wallen;
Yule ambaye atakuvunja vipande vipande anawaita maafisa wake; wanajikwaa kila mmoja kwa mwingine katika kutembea kwao; wanaharakisha kuushambulia ukuta wa mji. Ngao kubwa imetayarishwa kujikinga na hawa washambuliaji.
6 Het stormdak geplaatst, de sluizen der stromen geopend! Het paleis overstroomd,
Malango kwenye mito yamelazishwa kufunguka, na jumba la mfalme linaanguka kwenye uharibifu.
7 De vrouwen eruit, de ballingschap in: Haar maagden klagen als duiven, En slaan op de borst.
Husabu amevuliwa mavazi yake na amachukuliwa; watumishi wake wa kike wanaomboleza kama njiwa, wanavipiga vifua vyao.
8 Ninive is als een vijver geworden, Waarvan het water wegloopt: "Blijft hier, blijft hier!" Maar niemand ziet om.
Ninawi ni kama bwawa la maji linalovuja, watu wake kwa pamoja wanakimbia kama maji yanayotiririka. Wengine wanasema, “Simama, simama,” lakini hakuna anayegeuka nyuma.
9 Rooft zilver, rooft goud, Geen eind aan de schatten; Kiest het heerlijkste uit Van haar kostbaar bezit!
Chukua nyara ya fedha, kuchua nyara ya dhahabu, maana hakuna mwisho wake, kwa fahari ya vitu vyote vizuri vya Ninawi.
10 Plundering, roof en vernieling, Bonzende harten, knikkende knieën, Alle lenden verlamd, Alle gezichten doodsbleek.
Ninawi ipo tupu na imeharibiwa. Moyo wa kila mtu unayeyuka, magoti ya kila mmoja yanagongana pamoja, na uchungu upo kwa kila mmoja; sura zao wote zimepauka.
11 Waar is nu het hol van den leeuw, De krocht van de leeuwenwelpen, Waarheen de leeuw sluipt met de leeuwin En de welpen, door niemand verschrikt?
Sasa liko wapi pango la simba, sehemu ambapo simba wadogo hula chakula, sehemu ambapo simba dume na simba jike walitembea, pamoja wana-simba, ambapo hawakuogopa kitu chochote?
12 Waar is de leeuw, die roofde voor zijn jongen, En worgde voor zijn leeuwinnen, Die zijn holen vulde met buit, Zijn krochten met prooi?
Simba alirarua mawindo yake vipande vipande kwa ajili ya watoto wake; aliwanyonga mawindo wake kwa ajili ya wake zake, na kulijaza pango lake mawindo, makao yake kwa mizoga iliyoraruliwa.
13 Uw leger laat Ik opgaan in rook, Het zwaard zal uw welpen verslinden; Ik zal uw buit van de aarde verdelgen, Het gebrul uwer leeuwinnen verstomt.
“Tazama, mimi nipo kinyume na wewe- hili ni neno la Yehova wa majeshi. Nitayachoma magari yenu ya vita katika moshi, na upanga utateketeza simba wenu vijana. Nitazuia nyara zenu kutoka kwenye nchi yangu, na sauti za wajumbe wenu hazitasikika tena.”

< Nahum 2 >