< Jakovljeva 4 >

1 Odakle ratovi, odakle borbe među vama? Zar ne odavde: od pohota što vojuju u udovima vašim?
Ugonvi na migogoro miongoni mwenu vyatoka wapi? Haviinuki kutoka katika tamaa zenu mbaya zinazoleta vita ndani ya washirika wenu?
2 Žudite, a nemate; ubijate i hlepite, a ne možete postići; borite se i ratujete. Nemate jer ne ištete.
Mnatamani kile msichokuwa nacho. Mnauwa na mnafukuzia kile msichoweza kuwa nacho. Mnapigana na kugombana, na bado hampati kwa sababu hamumwombi Mungu.
3 Ištete, a ne primate jer rđavo ištete: da u pohotama svojim potratite.
Mnaomba na hampokei kwa sababu mnaomba kwa ajili ya mambo mabaya, ili kwamba muweze kuvitumia kwa tamaa zenu mbaya.
4 Preljubnici! Ne znate li da je prijateljstvo sa svijetom neprijateljstvo prema Bogu? Tko god dakle hoće da bude prijatelj svijeta, promeće se u neprijatelja Božjega.
Enyi wazinzi! Hamjui kwamba urafiki na ulimwengu ni uadui dhidi ya Mungu? Kwa hiyo, yeyote aamuaye kuwa rafiki wa ulimwengu hujifanya mwenyewe adui wa Mungu.
5 Ili mislite da Pismo uzalud veli: Ljubomorno čezne za duhom što ga nastani u nama?
Au mnadhani maandiko hayana maana yasemapo kwamba Roho aliyoweka ndani yetu ana wivu sana kwa ajili yetu?
6 A daje on i veću milost. Zato govori: Bog se oholima protivi, a poniznima daje milost.
Lakini Mungu hutoa neema zaidi, ndiyo maana maandiko husema, “Mungu humpinga mwenye kiburi, lakini humpa neema mnyenyekevu.”
7 Podložite se dakle Bogu! Oduprite se đavlu i pobjeći će od vas!
Hivyo, jitoeni kwa Mungu. Mpingeni ibilisi na yeye atakimbia kutoka kwenu.
8 Približite se Bogu i on će se približiti vama! Očistite ruke, grešnici! Očistite srca, dvoličnjaci!
Sogeeni karibu na Mungu, na yeye atakaribia karibu nanyi. Safisheni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na takaseni mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.
9 Zakukajte, protužite, proplačite! Smijeh vaš nek se u plač obrati i radost u žalost!
Huzunikeni, ombolezeni, na kuria! Geuzeni kicheko chenu kuwa huzuni na furaha yenu kuwa maombolezo.
10 Ponizite se pred Gospodinom i on će vas uzvisiti!
Jinyenyekezeni wenyewe mbele za Bwana, na atawainua juu.
11 Ne ogovarajte, braćo, jedni druge! Tko ogovara ili sudi brata svoga, ogovara i sudi Zakon. A sudiš li Zakon, nisi vršitelj nego sudac Zakona.
Msineneane kinyume ninyi kwa ninyi, ndugu. Mtu anenaye kinyume na ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, hunena kinyume na sheria na huihukumu sheria ya Mungu. Mkiihukumu sheria, hamuitii sheria, bali mnaihukumu.
12 Jedan je Zakonodavac i Sudac: Onaj koji može spasiti i pogubiti. A tko si ti da sudiš bližnjega?
Ni mmoja tu ambaye ni mtoa sheria na hakimu, Mungu, yeye ambaye ana uwezo wa kuokoa na kuangamiza. Wewe ni nani ambaye unamhukumu jirani yako?
13 De sada, vi što govorite: “Danas ili sutra otići ćemo u taj i taj grad, provesti ondje godinu, trgovati i zaraditi”,
Sikilizeni, ninyi msemao, “Leo au kesho tutakwenda katika mji huu, na kukaa mwaka huko, na kufanya biashara, na kutengeneza faida.”
14 a ne znate što će sutra biti. Ta što je vaš život? Dašak ste što se načas pojavi i zatim nestane!
Ni nani ajuaye nini kitatokea kesho, na maisha yenu ni nini hasa? Kwa kuwa mnafanana kama ukungu unaotokea kwa muda mfupi na kisha hupotea.
15 Umjesto da govorite: “Htjedne li Gospodin, živjet ćemo i učiniti ovo ili ono”,
Badala yake mngesema, “kama ni mapenzi ya Bwana, tutaishi na tutafanya hiki au kile.”
16 vi se razmećete svojim hvastanjima! Svako je takvo hvastanje opako.
Lakini sasa mnajivuna juu ya mipango yenu. Majivuno yote hayo ni uovu.
17 Znati dakle dobro činiti, a ne činiti - grijeh je.
Kwahiyo, kwake yeye ajuaye kutenda mema lakini hayatendi, kwake huyo ni dhambi.

< Jakovljeva 4 >