< 路加福音 21 >

1 耶穌抬頭觀看,見財主把捐項投在庫裏,
Yesu alitazama akawaona wanaume matajiri waliokuwa wanaweka zawadi zao kwenye hazina.
2 又見一個窮寡婦投了兩個小錢,
Akamuona mjane mmoja masikini akiweka senti zake mbili.
3 就說:「我實在告訴你們,這窮寡婦所投的比眾人還多;
Hivyo akasema, “Kweli nawaambieni, huyu Mjane maskini ameweka nyingi kuliko wengine wote.
4 因為眾人都是自己有餘,拿出來投在捐項裏,但這寡婦是自己不足,把她一切養生的都投上了。」
Hawa wote wametoa hizi zawadi kutoka katika vingi walivyonavyo. Lakini huyu mjane, katika umaskini wake, ametoa fedha zote alizokuwa nazo kwa ajili ya kuishi kwake.”
5 有人談論聖殿是用美石和供物妝飾的;
Wakati wengine walipokuwa wakisema juu ya hekalu, namna lilivyokuwa limepambwa na mawe mazuri na matoleo, alisema,
6 耶穌就說:「論到你們所看見的這一切,將來日子到了,在這裏沒有一塊石頭留在石頭上,不被拆毀了。」
“Kwa habari ya mambo haya mnayoyaona, siku zitakuja ambazo hakuna jiwe moja ambalo litaachwa juu ya jiwe jingine ambalo halitabomolewa.”
7 他們問他說:「夫子!甚麼時候有這事呢?這事將到的時候有甚麼預兆呢?」
Hivyo wakamuuliza, wakasema, “Mwalimu, mambo haya yatatokea lini? Na nini ni itakuwa ishara kwamba haya mambo yako karibu kutokea?”
8 耶穌說:「你們要謹慎,不要受迷惑;因為將來有好些人冒我的名來,說:『我是基督』,又說:『時候近了』,你們不要跟從他們!
Yesu akajibu, “Muwe waangalifu kwamba msidanganywe. Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, 'Mimi ndiye, 'na 'Muda umekaribia'. Msiwafuate.
9 你們聽見打仗和擾亂的事,不要驚惶;因為這些事必須先有,只是末期不能立時就到。」
Mkisikia vita na vuruguvurugu msiogope, kwa sababu haya mambo lazima yatokee kwanza, lakini mwisho hautatokea upesi.”
10 當時,耶穌對他們說:「民要攻打民,國要攻打國;
Kisha akawaambia, “Taifa litainuka kupigana na taifa jingine, na ufalme juu ya ufalme mwingine.
11 地要大大震動,多處必有饑荒、瘟疫,又有可怕的異象和大神蹟從天上顯現。
Kutakuwa na matetemeko makubwa, na njaa na tauni katika maeneo mbalimbali. Kutakuwa na matukio ya kutisha na ishara za kutisha kutoka mbinguni.
12 但這一切的事以先,人要下手拿住你們,逼迫你們,把你們交給會堂,並且收在監裏,又為我的名拉你們到君王諸侯面前。
Lakini kabla ya mambo haya yote, wataweka mikono yao juu yenu na kuwatesa, kuwapeleka kwenye masinagogi na magereza, kuwaleta mbele za wafalme na wenye mamlaka kwa sababu ya jina langu.
13 但這些事終必為你們的見證。
Hii itawafungulia fursa kwa ushuhuda wenu.
14 所以,你們當立定心意,不要預先思想怎樣分訴;
Kwahiyo amueni mioyoni mwenu kutoandaa utetezi wenu mapema,
15 因為我必賜你們口才、智慧,是你們一切敵人所敵不住、駁不倒的。
kwa sababu nitawapa maneno na hekima, ambayo adui zenu wote hawataweza kuipinga au kuikana.
16 連你們的父母、弟兄、親族、朋友也要把你們交官;你們也有被他們害死的。
Lakini mtakataliwa pia na wazazi wenu, ndugu zenu, jamaa zenu na rafiki zenu, na watawaua baadhi yenu.
17 你們要為我的名被眾人恨惡,
Mtachukiwa na kila mmoja kwa sababu ya jina langu.
18 然而,你們連一根頭髮也必不損壞。
Lakini hakuna hata unywele mmoja wa vichwa vyenu utakaopotea.
19 你們常存忍耐,就必保全靈魂。」
Katika kuvumilia mtaziponya nafsi zenu.
20 「你們看見耶路撒冷被兵圍困,就可知道它成荒場的日子近了。
Mtakapoona Yerusalemu imezungukwa na majeshi, basi jueni kwamba uharibifu wake umekaribia.
21 那時,在猶太的應當逃到山上;在城裏的應當出來;在鄉下的不要進城;
Hapo wale walioko Yudea wakimbilie milimani, na wale walioko katikati ya jiji waondoke, na msiwaache walioko vijijini kuingia.
22 因為這是報應的日子,使經上所寫的都得應驗。
Maana hizi ni siku za kisasi, ili kwamba mambo yote yaliyoandikwa yapate kutimilika.
23 當那些日子,懷孕的和奶孩子的有禍了!因為將有大災難降在這地方,也有震怒臨到這百姓。
Ole ni kwa wale walio na mimba na kwa wale wanyonyeshao katika siku hizo! Kwa maana kutakuwa na adha kuu juu ya nchi, na ghadhabu kwa watu hawa.
24 他們要倒在刀下,又被擄到各國去。耶路撒冷要被外邦人踐踏,直到外邦人的日期滿了。」
Na wataanguka kwa ncha ya upanga na watachukuliwa mateka kwa mataifa yote, na Yerusalem itakanyagwa na watu wa mataifa, mpaka wakati wa watu wa mataifa utakapotimilika.
25 「日、月、星辰要顯出異兆,地上的邦國也有困苦;因海中波浪的響聲,就慌慌不定。
Kutakuwa na ishara katika jua, mwezi na nyota. Na katika nchi kutakuwa na dhiki ya mataifa, katika kukata tamaa kutokana na mlio wa bahari na mawimbi.
26 天勢都要震動,人想起那將要臨到世界的事,就都嚇得魂不附體。
Kutakuwa na watu wakizimia kwa hofu na katika kutarajia mambo yatakoyo tokea juu ya dunia. Kwa maana nguvu za mbingu zitatikiswa.
27 那時,他們要看見人子有能力,有大榮耀駕雲降臨。
Kisha watamwona Mwana wa Adamu akija mawinguni katika nguvu na utukufu mkuu.
28 一有這些事,你們就當挺身昂首,因為你們得贖的日子近了。」
Lakini mambo haya yatakapoanza kutokea, simameni, inueni vichwa vyenu, kwa sababu ukombozi wenu umesogea karibu.”
29 耶穌又設比喻對他們說:「你們看無花果樹和各樣的樹;它發芽的時候,你們一看見,自然曉得夏天近了。
Yesu akawaambia kwa mfano, “Uangalieni mtini, na miti yote.
Inapotoa machipukizi, mnajionea wenyewe na kutambua kwamba kiangazi tayari kiko karibu.
31 這樣,你們看見這些事漸漸地成就,也該曉得上帝的國近了。
Vivyo hivyo, mnapoona mambo haya yanatokea, ninyi tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu umekaribia.
32 我實在告訴你們,這世代還沒有過去,這些事都要成就。
Kweli, nawaambieni, kizazi hiki hakitapita, mpaka mambo haya yote yatakapotokea.
33 天地要廢去,我的話卻不能廢去。」
Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
34 「你們要謹慎,恐怕因貪食、醉酒,並今生的思慮累住你們的心,那日子就如同網羅忽然臨到你們;
Lakini jiangalieni wenyewe, ili kwamba mioyo yenu isije ikalemewa na ufisadi, ulevi, na mahangaiko ya maisha haya. Kwa sababu ile siku itawajia ghafla
35 因為那日子要這樣臨到全地上一切居住的人。
kama mtego. Kwasababu itakuwa juu ya kila mmoja aishiye katika uso wa dunia nzima.
36 你們要時時警醒,常常祈求,使你們能逃避這一切要來的事,得以站立在人子面前。」
Lakini mwe tayari wakati wote, mwombe kwamba mtakuwa imara vya kutosha kuyaepuka haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.”
37 耶穌每日在殿裏教訓人,每夜出城在一座山,名叫橄欖山住宿。
Hivyo wakati wa mchana alikuwa akifundisha hekaluni na usiku alitoka nje, na kwenda kukesha katika mlima unaoitwa wa Mzeituni.
38 眾百姓清早上聖殿,到耶穌那裏,要聽他講道。
Watu wote walimjia asubuhi na mapemaili kumsikiliza ndani ya hekalu.

< 路加福音 21 >