< 耶利米书 38 >

1 玛坦的儿子示法提雅、巴施户珥的儿子基大利、示利米雅的儿子犹甲、玛基雅的儿子巴施户珥听见耶利米对众人所说的话,说:
Shefatia mwana wa Matani, Gedalia mwana wa Pashuri, na Pashuri mwana wa Malkiya alisikia maneno ambayo Yeremia alikuwa akitanganza kwa wato wote. Alikuwa akisema,
2 “耶和华如此说:住在这城里的必遭刀剑、饥荒、瘟疫而死;但出去归降迦勒底人的必得存活,就是以自己命为掠物的,必得存活。
“Yahwe asema hivi: Yeyote anayeishi kwenye mji huu atauwawa kwa upanga, njaa, na pigo. Lakini yeyote ambaye aendae kwa Wakaldayo ataishi. Atatoroka pamoja na maisha yake mwenyewe, na kuishi.
3 耶和华如此说:这城必要交在巴比伦王军队的手中,他必攻取这城。”
Yahwe asema hivi: Huu mji huu utapewa kwa mkono wa jeshi la mfalme wa Babeli, na ataukamata.”
4 于是首领对王说:“求你将这人治死;因他向城里剩下的兵丁和众民说这样的话,使他们的手发软。这人不是求这百姓得平安,乃是叫他们受灾祸。”
Kwa hiyo maafisa walisema kwa mfalme, “Acha mtu huu afe, kwa kuwa kwa njia hii anadhofisha mikono ya wanaume wapiganaji waliobaki kwenye mji huu, na mikono ya watu wote. Anatanganza maneno haya, kwa kuwa huyu mtu hafanyi kwa usalama wa watu hawa, lakini kwa majanga.”
5 西底家王说:“他在你们手中,无论何事,王也不能与你们反对。”
Basi mfalme Sedekia alisema, “Tazama, yuko mkononi mwako kwa kuwa hakuna mfalme awezae kumpinga.”
6 他们就拿住耶利米,下在哈米勒的儿子玛基雅的牢狱里;那牢狱在护卫兵的院中。他们用绳子将耶利米系下去。牢狱里没有水,只有淤泥,耶利米就陷在淤泥中。
Kisha walimchukua Yeremia na kumtupa kwenye kisima cha Malkiya, mwana wa mfalme. Kisima kilikuwa kwenye uwanja wa mlinzi. Walimshusha Yeremia chini kwa kamba. Hapakuwa na maji kwenye kisima, lakini kulikuwa na matope, na alizama chini ya matope.
7 在王宫的太监古实人以伯·米勒,听见他们将耶利米下了牢狱(那时王坐在便雅悯门口),
Sasa Ebed Meleki Mkushi alikuwa mmoja wa watowashi katika nyumba ya mfalme. Alisikia kwamba walikuwa wamemuweka Yeremia kwenye kisima. Sasa mfalme alikuwa ameketi kwa mlango wa Benjamini.
8 以伯·米勒就从王宫里出来,对王说:
Basi Ebed Meleki alienda toka nyumba ya mfalme na kuzungumza na mfalme.
9 “主—我的王啊,这些人向先知耶利米一味地行恶,将他下在牢狱中;他在那里必因饥饿而死,因为城中再没有粮食。”
Alisema, “Bwana wangu mfalme, hawa wanaume wamefanya uovu kwa namna walivyomtendea Yeremia nabii. Walimtupa kwenye kisima kwa ajili ya kufa kutokana na njaa, tangu hakuna chakula zaidi katika mji.”
10 王就吩咐古实人以伯·米勒说:“你从这里带领三十人,趁着先知耶利米未死以前,将他从牢狱中提上来。”
Kisha mfalme alitoa amri kwa Ebed Meleki Mkushi. Alisema, “Chukua amri ya watu thelasini kutoka hapa na mtoe Yeremia nabii nje ya kisima kabla hajafa.”
11 于是以伯·米勒带领这些人同去,进入王宫,到库房以下,从那里取了些碎布和破烂的衣服,用绳子缒下牢狱去到耶利米那里。
Basi Ebed Meleki alichukua amri ya watu hao na akaenda nyumba ya mfalme, kwenye ghala la nguo chini ya nyumba. Toka hapo alichukua vitambaa na nguo zilizochanika na kuyashusha chini kwa kamba kwa Yeremia ndani ya kisima.
12 古实人以伯·米勒对耶利米说:“你用这些碎布和破烂的衣服放在绳子上,垫你的胳肢窝。”耶利米就照样行了。
Ebed Meleki Mkushi alisema kwa Yeremia, “Weka matambara na nguo zilizoraruka chini ya mikono yako na juu ya kamba.” Basi Yeremia alifanya hivyo.
13 这样,他们用绳子将耶利米从牢狱里拉上来。耶利米仍在护卫兵的院中。
Kisha walimvuta Yeremia kwa kamba. Kwa njia hii walimtoa kutoka kisimani. Basi Yeremia alibaki kwenye uwanja wa mlinzi.
14 西底家王打发人带领先知耶利米,进耶和华殿中第三门里见王。王就对耶利米说:“我要问你一件事,你丝毫不可向我隐瞒。”
Kisha Mfalme Sedekia alituma neno na kumleta Yeremia nabii kwake, kwenye lango la tatu la nyumba ya Yahwe. Mfalme alisema kwa Yeremia, “Nataka nikuulize kitu. Usinizuilie jibu mimi.”
15 耶利米对西底家说:“我若告诉你,你岂不定要杀我吗?我若劝戒你,你必不听从我。”
Yeremia alisema kwa Sedekia, “Kama nakujibu, hautaniuawa kwa hakika? Na kama nakupa ushauri, hautanisikiliza mimi.”
16 西底家王就私下向耶利米说:“我指着那造我们生命之永生的耶和华起誓:我必不杀你,也不将你交在寻索你命的人手中。”
Lakini Mfalme Sedekia aliapa kwa Yeremia kwa siri na kusema, “Kama Yahwe aishivyo, yeye aliyetufanya sisi, Sitakuuwa au kukuweka kwenye mkono wa watu wale wanaotafuta maisha yako.”
17 耶利米对西底家说:“耶和华—万军之 神、以色列的 神如此说:你若出去归降巴比伦王的首领,你的命就必存活,这城也不致被火焚烧,你和你的全家都必存活。
Kwa hiyo Yeremia alisema kwa Sedekia, “Yahwe, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi: Kama kwa kweli utatoka kwenda kwa maafisa wa mfalme wa Babeli basi utaishi, and mji huu hautachomwa. Wewe na familia yako mtaishi.
18 你若不出去归降巴比伦王的首领,这城必交在迦勒底人手中。他们必用火焚烧,你也不得脱离他们的手。”
Lakini kama hautaenda kwa maafisa wa mfalme wa Babeli, basi mji huu utachukuliwa kwa mkono wa Wakaldayo. Watauchoma, na hautakwepa kutoka mkono wao.”
19 西底家王对耶利米说:“我怕那些投降迦勒底人的犹大人,恐怕迦勒底人将我交在他们手中,他们戏弄我。”
Mfalme Sedekia alisema kwa Yeremia, “Lakini ninaogopa watu wa Yuda waliotoka jangwani kwenda kwa Wakaldayo, kwa sababu nitapewa katika mkono wao, kwa kunifanyia vibaya.”
20 耶利米说:“迦勒底人必不将你交出。求你听从我对你所说耶和华的话,这样你必得好处,你的命也必存活。
Yeremia alisema, “Hawatakutoa kwao. Tii ujumbe toka kwa Yahwe ambao ninakuambia, ili kusudi mambo yataenda vizuri kwako, na ili kusudi utaishi.
21 你若不肯出去,耶和华指示我的话乃是这样:
Lakini kama unakataa kutoka, hivi ndivyo Yahwe amenionesha mimi.
22 犹大王宫里所剩的妇女必都带到巴比伦王的首领那里。这些妇女必说: 你知己的朋友催逼你, 胜过你; 见你的脚陷入淤泥中, 就转身退后了。
Tazama! Wanawake wote walioachwa kwenye nyumba yako, mfalme wa Yuda, ataletwa kwa maafisa wa mfalme wa Babeli. Hawa wanawake watasema kwako, “Umedaganywa na rafiki zako; wamekuharibu. Miguu yako sasa imezama kwenye matope, na rafiki zako watakimbia.'
23 “人必将你的后妃和你的儿女带到迦勒底人那里;你也不得脱离他们的手,必被巴比伦王的手捉住;你也必使这城被火焚烧。”
Kwa kuwa wake zenu wote na watoto wataletwa kwa Wakaldayo, na wewe mwenyewe hautatoroka nchi yao. Utashikwa na mkono wa mfalme wa Babeli, na mji huu utachomwa.”
24 西底家对耶利米说:“不要使人知道这些话,你就不至于死。
Kisha Sedekia alisema kwa Yeremia, “Usimjulishe yeyote kuhusu maneno haya, ili kwamba usije kufa.
25 首领若听见了我与你说话,就来见你,问你说:‘你对王说什么话不要向我们隐瞒,我们就不杀你。王向你说什么话也要告诉我们。’
Kama maafisa wanasikia kwamba nimeongea na wewe- kama wanakuja na kusema kwako, 'Tuambia umezungumza nini pamoja na mfalme. Usitufiche, au tutakuuwa. Na tuambie nini mfalme amesema kwako'-
26 你就对他们说:‘我在王面前恳求不要叫我回到约拿单的房屋死在那里。’”
kisha unapaswa kusema nao, “Nilishawishiana pamoja na mfalme asirudi kwangu kwa nyumba ya Yonathan nitakufa humo.”
27 随后众首领来见耶利米,问他,他就照王所吩咐的一切话回答他们。他们不再与他说话,因为事情没有泄漏。
Kisha maafisa wote walikuja kwa Yeremia na kumuuliza, basi aliwajibu kama mfalme alivyomuelekeza. Basi waliacha kuongea pamoja naye, kwa sababu hawakusikia mazungumzo kati ya Yeremia na mfalme.
28 于是耶利米仍在护卫兵的院中,直到耶路撒冷被攻取的日子。
Basi Yeremia alibaki kwenye uwanja wa mlinzi mpaka siku ile Yerusalem ilipotekwa.

< 耶利米书 38 >