< Luka 9 >

1 Ayicila nono katwa mye likure nin wabe, ana nani likara kitene nagbergenu nin shizhinu nin tikonu.
Akawaita wale kumi na wawili pamoja, akawapa uwezo na mamlaka juu ya mapepo yote na kuponya magonjwa.
2 Ato nani, idi bellin uliru kiti kipin tigo mye, nin shizinu nanan tikonu.
Akawatuma waende kuhubiri ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa.
3 A woro nani na iwa yiru imon bara ucine ba, sa uca, imon inyi, imonlii, ukurfung, sa alutuk abba.
Akawaambia, “Msichukue chochote kwa ajili ya safari yenu wala fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala pesa wala msichukue kanzu mbili.
4 Vat kilari ka na ipira soo kinin, udu liyiri lo na iba cinu kipine.
Nyumba yoyote mtakayo iingia, kaeni humo mpaka mtakapo ondoka mahali hapo.
5 Inung alle na inari munu, asa iba nuzu nanya kipin, kotinon lidau we nabune mine, liba so ushaida nati mine.”
Na kwa wale wasio wapokea, mtakapo ondoka mji huo, jikung'uteni vumbi katika miguu yenu kwa ushuhuda juu yao”.
6 Itunna iwatuna, ipira nigbire itina nbellin nliru umang, nin shizinu nanit niti niti.
Wakaondoka na kwenda kupitia vijijini, wakitangaza habari njema na kuponya watu kila mahali.
7 Hirdus ugo na alanza ile imon na idinsu, au Yohanna unan shintu nanit infita.
Sasa Herode, mtawala, alisikia yote yaliyo kuwa yakitokea alitaabika sana, kwa sababuu ilisemekana na baadhi kwamba Yohana mbatizaji amefufuka kutoka wafu,
8 Kiti namong idin su Iliya nsah, among woro umon unan nburnari, in fita nanya na nan nlai.
na baathi kwamba Elia amekwisha tokea, na kwa wengine kwamba mmoja wa manabii wa zamani amefufuka katika wafu tena.
9 Hiridus woro, “Ina malu ukalu liti Yohanna, ani ghari ndi nlanzu kiti mee nene.” Hiridus do npiziru ayene Yesu ku.
Herode alisema, “nilimchinja Yohana, lakini huyu ni nani ninae sikia habari zake? Na Herode alitafuta njia ya kumwona Yesu.
10 Alenge na iwa tuu nani issah, ibellinghe vat nile imon na isu, anya nanghinu ligowe nanghe, udu kipin Batsaida.
Wakati waliporudi wale waliotumwa, wakamwamwambia kila kitu walicho fanya. Akawachukua pamoja naye, akaenda peke yake katika mji uitwao Bethsadia.
11 Inung ligoze lanza nani Idofinghe, atah nani mahadi, abelle nani ubellen kipin tigo na idinin su inshinue.
Lakini makutano wakasikia kuhusu hili wakamfuata, na aliwakaribisha, na akaongea nao kuhusu ufalme wa Mungu, na aliwaponya wale waliohitaji uponyaji.
12 Nin ndu kulelen, inung likure nin wabe, woroghee suuna ligoze idoo nigbir nkilinue, idi piziru kiti linanin nin nimonli, bara kikane na tidi ku kushori.
Siku ikaanza kuisha, na wale kumi na wawili wakaenda kwake na kusema, “Watawanye makutano kwamba waende katika vijiji vya karibu na mijini wakatafute mapumziko na chakula, kwa sababu tupo eneo la nyikani.”
13 Aworo nani, “Nan nani imonli ili.” Inug woro, “na tidi nin nimomon na ikatin nfungul utaun nin niboo ibba ba, sse tido tidi seru nani imonli bara ligozi vat.
Lakini akawaambia, “Nyie wapeni kitu cha kula.” Wakasema “Hatuna zaidi ya vipande vitano vya mikate na samaki wawili, isipokuwa tungeenda na kununua chakula kwa ajili ya kusanyiko hili la watu.”
14 Iwadi annit amui alaun. A woro nono kadura mye, “Taan nani iso acuri akut ataun taun.
Kulikua na wanaume wapatao elfu tano pale. Akawambia wanafunzi wake. “Wakalisheni chini katika makundi ya watu wapatao hamsini kwa kila kundi.
15 Isu nani anite so vat kutyin.
Kwa hiyo wakafanya hivyo na watu wa wakaketi chini.
16 A yauna ufungul utaune nin niboo ibe, ato iyiizi kitene atah nmari ku, a pucu agir anaa nono katuwa mye, inin koso nani.
Akachukua mikate mitano na samaki wawili na akatazama mbinguni, akavibariki, na kuvimega katika vipande, akawapa wanafunzi wake ili waviweke mbele ya makutano.
17 Inung vat leo ishito, kagisin nbubun nimole nazza, ipitirno ita nakuzun likure nin nabba.
Wote wakala na wakashiba, na vipande vya chakula vilivyo baki viliokotwa na kujaza vikapu kumi na viwili.
18 Idoo nkon kubi adin nti nliran usame, nono katuwa mye nanghe anin tirino nani, “Ligozi din su meng ghari?”
Nayo ikawa kwamba, alipokuwa akiomba peke yake, wanafunzi wake walikuwa pamoja naye, na akawauliza akisema, “watu husema mimi ni nani?”
19 Ikauwa ghe iworo, “Yohanna unan shintu nmyen (Baptisma) amon woro Iliya, amon woro nkon kunan nburnuari in fita.”
Wakijibu, wakasema, “Yohana mbatizaji, lakini wengine husema Eliya, na wengine husema mmoja wa manabii wa nyakati za zamani amefufuka tena.”
20 Anin woro nani, “Anung dinsu meng ghari?” Bitrus kauwa aworo kristi unuzu Kutelle.”
Akawambia, “Lakini ninyi mwasema mimi ni nani?” Akijibu Petro akasema, “Kristo kutoka kwa Mungu.”
21 A wunno nani atuf, Yesu woro nani na iwa bellin umon ba.
Lakini kwa kuwaonya, Yesu akawaelekeza kutomwambia yeyote juu ya hili,
22 Nworu gono nnit ba niu nin nimon gbardang, iba nari ghe, akune nin uso napirist a anan ninyerte, iba mollughe ayiri atat a ba fitu nin lai.
akasema kwamba mwana wa Adamu lazma ateseke kwa mambo mengi na kukataliwa na wazee na Makuhani wakuu na waandishi, na atauawa, na siku ya tatu atafufuka.
23 A woro nani vat, “Asa ule na adinin nsu adak kiti nigh, aba nari liti mye, aba diru, ule na anari litime bara meng aba se utucu.
Akawambia wote, “kama mtu yeyote akitaka kunifuata, lazima ajikane mwenyewe, achukue msalaba wake kila siku, na anifuate.
24 Ulenge na idinin su a tucu liti mye, aba diru, ule na anari litime bara meng aba se utucu.
Yeyote ajaribuye kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote apotezae maisha yake kwa faida yangu, atayaokoa.
25 Iyaghari ncaute unit se imon inye vat, anin dira ulai mye?
Je kitamfaidia nini mwanadamu, kama akiupata ulimwengu wote, lakini akapoteza au akapata hasara ya nafsi yake?
26 Vat nle na adi nlanzu ncin nigh nin ligbulang nigh, gono nnit ba lanzu ncin mye nwui une na aba dak nanya ngongon Ncif mye nin nono kadura Kutelle.
Yeyote atakaye nionea aibu mimi na maneno yangu, kwake yeye mwana wa Adam atamuonea aibu atakapo kuwa katika utukufu wake, na utukufu wa Baba na malaika watakatifu.
27 Nworo munu kidegenere indi bellu munu, among yisin kikane, na ukul ba dudu nani ba, se idoo kipin tigo Kutelle.”
Lakini ninawaambia ukweli, kuna baadhi yenu wasimamao hapa, hawata onja umauti mpaka wauone ufalme wa Mungu.”
28 Na ayiri kulir nkata na Yesu nbelle nani tigbulang tone, ayira Bitrus, Yohanna, a Yakubu, ighana kitene kupara ati nlirag.
Ikatokea yapata siku nane baada ya Yesu kusema maneno haya kwamba akawachukua pamoja nae Petro, Yohana na, Yakobo, wakapanda mlimani kuomba.
29 Na adi nliraghe, umuro mye saka, imon mye tunna ipo pau nwaltu.
Na alipokuwa katika kuomba, muonekano wa uso wake ulibadilika, na mavazi yake yakawa meupe na ya kung'aa.
30 Itunna ise amon naba ida idin nliru nanghe, ashe Musa nin Iliya.
Na tazama, walikuwepo wanaume wawili wakiongea naye! Walikuwa Musa na Elia,
31 Ale na iwa yenje nani gongon, idin nliru kitene nnyiu mye, ule na iba kullu nanya Urushelima.
walionekana katika utukufu. Waliongea kuhusu kuondoka kwake, jambo ambalo alikaribia kulitimiza Yerusalem.
32 Kubi, Bitrus nan nale na iwa di nanghe nmoro wadi nani kang, na izinto, iyene ngongon mye nin nale iwa yisin nanghe.
Sasa Petro na wale waliokua pamoja naye walikuwa katika usingizi mzito. Lakini walipokuamka, waliuona utukufu wake na wanaume wawili waliokuwa wamesimama pamoja nae.
33 Uso nani, na inya ligowe nan Yesu, Bitrus woroghe, “Cikilari ucaun na tidi kikane, tiba ke adanga atat, ti ke kurum kun Iliya.” Na ayinno ile imon na adin belle ba.
Ikatokea kwamba, walipokuwa wakiondoka kwa Yesu, Petro akamwambia, “Bwana, ni vizuri kwetu kukaa hapa na inatupasa tutengeneze makazi ya watu watatu. Tutengeneze moja kwa ajili yako, moja kwa ajili ya Musa, na moja kwa ajili ya Eliya.” Hakuelewa alichokuwa akiongelea.
34 Kube na adin belle nleli imone, kuwut tolo ku tursu nani, fiu da nani, na kuwute nkilino nani.
Alipokuwa akisema hayo, likaja wingu na likawafunika; na waliogopa walipoona wamezunguwa na wamezungukwa na wingu.
35 Liwui nuzu nanya kuwute liworo, “Gono nighari kane na ina fere lanzan ghe.”
Sauti ikatoka kwenye wingu ikasema, “Huyu ni Mwanangu mteule. Msikilizeni yeye.”
36 Na imala ulanzu liwuiye, Yesu yita usame, inung so tik, nanya nayiri ane na iwa bellin umong ba, ile imon na iyene.
Sauti iliponyamaza, Yesu alikuwa peke yake. walikaa kimya, na katika siku hizo hawakumwambia yeyote lolote miongoni mwa waliyoyaona.
37 Ukurtunu nkuiye, na isa unuzu kupara, ligozi nanit da zuro nanghe.
Siku iliyofuata, baada ya kutoka mlimani, kusanyiko kubwa la watu lilikutana naye.
38 Umon nanya ligozi gilla a woro, “Unan yiru ndin fofi nacara yene usaun nighe, amere gono nighe cas.
Tazama, mwanaume kutoka kwenye kusanyiko alilia kwa sauti, akisema, “Mwalimu ninakuomba umtazame mwanangu, kwa kuwa ni mwanangu wa pekee.
39 Yene Uruhu sa uyaunghe, amalzino, aketize, anutuzuno kupunget nnuwe, na asa usunghe ba, se ushalaghe.
Unaona roho chafu humshika, na mara hupiga kelele, na pia humfanya achanganyikiwe na kutokwa povu kinywani. Nayo humtoka kwa shida, ikimsababshia maumivu makali.
40 Asa nfo nono katwa fa acara, nshin ninghe na isa iyinno ba.”
Naliwasihi wanafunzi wako kuikea itoke. lakini hawakuweza.”
41 Yesu kauwa a woro, “Anung anan salin nyinnu nin kuji kugbas, udu kishiyari nba yinu uso nanghinu danin nsaun fe kikane.”
Yesu akajibu akasema, “Enyi kizazi kisichoamini na kilichopotoka, mpaka lini nitkaa nanyi na kuchukuliana nanyi? Mlete mwanao hapa.”
42 Na gone din cinu uduwe agbergenu yaunghe ilina kutyin atunna nketizu. Yesu kpada Uruhu unanzang, ashino nin gone, anin nakpa ucife.
Kijana aliokuwa anakuja, roho cha ikamuangusha chini na kumtikisa kwa fujo. Lakini Yesu aliikemea ile roho chafu, alimponya mvulana, na kamkabidhi kwa baba yake.
43 Vat mine yene nziziki ngbardang Kutelle, na vat mine nkiffo tunu nile imon asu, ani woro nono katuwa mye,
Wote walishangazwa na ukuu wa Mungu. Lakini walipokuwa wakistaajabu wote kwa mambo yote aliyo yaliyotedeka, akasema kwa wanafunzi wake,
44 “Na to tigbulanghe do piit nnit nacara nanit.”
“Maneno yawakae masikioni mwenu, kwa kuwa Mwana wa Adamu atatolewa mikononi mwa wanadamu.”
45 Na inin wa yinin ule idiru ba, Bara na uwa nyeshin kiti mine na iyinno liti nlire ba. Vat nani nlanza fiu nworu itiringhe uliru une.
Lakni hawakuelewa maana ya maneno hayo, na yalifichwa machoni pao, ili wasije wakalielewa. Waliogopa kumuuliza kuhusu neno hilo.
46 Manyardang fita nanya mine, nbelleng nworu ghari ba so udiya mine.
Kisha mgogoro ulianza ulizuka miongoni mwao i juu ya nani angekuwa mkuu.
47 Yesu nin yiru nkpilizu nibinai mine, a yicila kagone kabene a yisa likot me,
Lakini Yesu alipotambua walichokuwa wakihojiana mioyoni mwao, alimchukua mtoto mdogo, na kumuweka upande wake,
48 Anin woro nani, ulenge na asere gono kane, asere menku. Ulenge na asere menku, asere ulenge na ana tuuyi, ulenge na aceo liti me nafo gono kibene amere ba so udya nanya mine.
na akasema, “kama mtu yeyote akimpokea mtoto mdogo kama huyu kwa jina langu, anipokea mimi pia, na yeyote akinipokea mimi, ampokea pia aliyenituma, kwa kuwa aliye mdogo kati yenu wote ndiye alie mkuu”
49 Yohanna kauwa, “Cikilari tiyene umong nutuzunu nagbergenu nin lisafe, tinanin wantinghe, bara na adi ndortu nari ba.”
Yohana akajibu akasema, “Bwana, tulimuona mtu akifukuza pepo kwa jina lako na tukamzuia, kwa sababu haambatani na sisi.”
50 Na iwa wantinghe ba, “Ubellun Yesu, vat nlenge na adi nivira nan ghinu ba unminere.”
Lakini Yesu akamwambia, “Msimzuie, kwa kuwa asiye kinyume na ninyi ni wa kwenu”
51 Na ayiri nyiu me nda susut aceo umuro me udu Urushelima.
Ikatokea kwamba, kulinga na siku zilivyokua zikikaribia zsiku zake za kwenda mbinguni, kwa uimara alielekeza uso wake Yerusalemu.
52 Ato anan kadura nbun me, inya ipira kagbir Nsamariya, ikeleghe imone.
Akatuma wajumbe mbele yake, nao wakaenda na kuingia katika kijiji cha Wasamaria ili wamtayarishie mahali.
53 Anite kikane wa tighe mahabi ba, bara amal ciu umuro me udu Urushelima.
Lakini watu huko hawakumpokea, kwasababu alikua ameelekeza uso wake Yerusalemu.
54 Na nono katuwa me, Yakubu nin Yohanna inyene nani, iworo, “Cikilari titi ulah tolu umolu nani?”
Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipo liona hili, wakasema, “Bwana unahitaji tuamuru moto ushuke chini kutoka mbinguni uwateketeze?”
55 A gitirino a kpada nani.
Lakini aliwageukia akawakemea.
56 Itunna inya udu nkan kagbir.
Kisha walikwenda kijiji kingine.
57 Na idin cine libau we, umon woroghe, “Meng ba dofin fi udu kika na uba duu.”
Walipokuwa wakienda katika njia yao, mtu mmoja akamwambia, “Nitakufuata popote uendapo.”
58 Yesu kauwa a woroghe, “Ninyan yau dinin tiyyi, Anyin yita nin nado, meng gono nnit dinin kiti nciu liti ba.
Yesu akamwambia, “Mbweha wanamashimo, ndege wa angani wana viota, lakini mwana wa Adamu hana pakulaza kichwa chake.”
59 Anin woro nmong, “Dofini.” Ame woroghe, “Cikilari ucizine na ndo ndi kassu ucif nigh.”
Ndipo akamwambia mtu mwingine, “Nifuate.” Lakini yeye akasema, “Bwana, niruhusu kwanza niende nikamzika baba yangu,”
60 Ame atimine anan nkul, fe can udi belle piit nin npash uliru kipin tigo Kutelle.”
Lakini yeye akamwambia, “Waache wafu wawazike wafu wao, lakini wewe nenda ukautangaze ufalme wa Mungu kila mahali.”
61 Umong ugang woroghe, “Meng ba dofinfi Cikilari, na ntuu ndi bellin anan kilari nighe meng nya.”
Pia mtu mwingine akasema. “Nitakufuata, Bwana, lakini niruhusu kwanza nikawaage walio katika nyumba yangu.”
62 Yesu kauwa a woroghe, “Na umong duku alenge na ata ucara me nkeke nikawa, asa a gitirno, na abase upiri kipin tigo Kutelle ba.”
Laki Yesu akamwambia hakuna mtu, atiaye mkono wake kulima na kuangalia nyuma atakayefaa kwa ufalme wa Mungu.”

< Luka 9 >