< 2 Ukorintiyawa 13 >

1 Ulele untatari naidin dasu kiti min, “an wabaa sa an watat nwa ti iyizi imba ulirun soo vat ni lemong na iibenle”
Hii ni mara yangu ya tatu kuja kwenu. “Kila tatizo litatatuliwa kwa ushahidi wa watu wawili au watatu,” yasema Maandiko.
2 Iwa malun benlu minu alee na isu kulapi nin kidung udu va mine kubi kon aiwa diku udakin baa mmini kuru benle: andi daa tutung na ima cinu nanin ba.
Nilikwisha sema, na kama ilivyokuwa safari ya pili, sasa nasema tena nikiwa mbali: wale wote waliotenda uovu bila kutubu, na pia wale wengine, nitakapokuja, watakiona cha mtema kuni.
3 In belin minu ule na bara na idin piziru iyizi in ba au Kristi din liru nanya ning Na a dira likara nanya mine ba nmanimako adi nin likara nanya mine.
Mtajionea wenyewe kwamba Kristo anasema ndani yangu. Kwenu Kristo si dhaifu; bali nguvu yake yafanya kazi miongoni mwenu.
4 Bara na iwa banaghe nin sali likara bara nani adi nin lai nin likara Kutelle. Bara na arik sali nin likara nanya m, bara nini ti ba yitu nin lai ninghe me. likara Kutelle nanya mine.
Maana hata kama alisulubiwa kwa sababu ya udhaifu, lakini sasa anaishi kwa uwezo wa Mungu. Sisi pia tu dhaifu kwa kuungana naye lakini tutaishi naye kwa uwezo wa Mungu kwa ajili yenu.
5 Dumunang atimine iyene sa idi nanya yenu sa uyun. Gbardan atimin. Na i iyiru ba Yesu Kristi di nanya mine. Aduku sai dai na iyiru mun ba
Jichunguzeni ninyi wenyewe mpate kujua kama kweli mnayo imani. Jichunguzeni ninyi wenyewe. Je, hamjui kwamba Kristo Yesu yumo ndani yenu? Kama sivyo, basi ninyi mmeshindwa.
6 Mang di nin nayi akune au i ma yinu na isa yina nin narik b.
Lakini natumaini kwamba ninyi mnajua kuwa sisi hatukushindwa.
7 Nene ti dinin nlira cindu kiti Kutelle au na i wa se i utanu ba andi na nani ba imase ti lau udumun, au bara nani in taa nlira inan su ilemon na ica, imoti tima yenu nafo ti deu udumune
Tunamwomba Mungu msifanye uovu wowote, lakini si kusudi tuonekane kama watu waliokwisha faulu, bali mpate kutenda mema, hata kama sisi tunaonekana kuwa tumeshindwa.
8 Bara tiwa gya tisu imomo usa bani kidegen, bara kidegenere kawai.
Maana hatuwezi kuupinga ukweli; uwezo tulio nao ni wa kuuendeleza ukweli.
9 Asa ti lanza mmang bara na arik ndiri anun nin kulun. Tinani kuru ti taa nlira au i se minu kulum
Tunafurahi kwamba sisi tu dhaifu, lakini ninyi mna nguvu; kwa hiyo tunaomba mpate kuwa wakamilifu.
10 Indin yertu nilele bara na ndi piit nan ghen, bara na nwadi nanghinu na mma yitu gbagbai nati mine b, insu katwa nin likara lo na ucif nay inke minu kokuwa in musuzu minu ba
Basi, ninaandika barua hii nikiwa mbali, ili nitakapofika kwenu nisilazimike kuwa mkali kwenu kwa kutumia ule uwezo alionipa Bwana; naam, uwezo wa kujenga na si wa kubomoa.
11 Nimalin, nwana ni lime nin nishono taan ayi aboo! sun katwa bara ukurtuzun, sun nin nibinai likara yinnan nin nwana nat, sun nanya ncanam nibinai, Kutelle su nin shau kibinai ba yitu ligowe nan ghenu.
Kwa sasa, ndugu, kwaherini! Muwe na ukamilifu, shikeni mashauri yangu, muwe na nia moja; kaeni kwa amani. Naye Mungu wa mapendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
12 Lison vat mine nin nilip ngbindirnu
Salimianeni kwa ishara ya upendo.
13 Vat anan yinnu sa uyenu din lisu minu
Watu wote wa Mungu huku wanawasalimuni.
14 Ubolu Kutelle Ncif Yesu Kristi usu Kutelle, nin lidondon Nfip milau yita nan ghenu vat.
Neema ya Bwana Yesu Kristo na upendo wa Mungu na umoja wa Roho Mtakatifu, viwe nanyi nyote.

< 2 Ukorintiyawa 13 >