+ Mataayi 1 >

1 Agha ghe matavua agha kikoko kya Yesu kilisite umhuma mu kisina kya ntwa uDavidi, ikisina kya Abulahimu.
Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.
2 Uabulahamu akampaapa uIsaka, uIsaka akampaapa una uYakovo, UYakovo akampaapa uYuuda na vanine.
Ibrahimu alikuwa baba wa Isaka, na Isaka baba wa Yakobo, na Yakobo baba wa Yuda na ndugu zake.
3 UYuuda akampaapa uPelesi nu Sela mwa Tamali, uPelesi akampaapa uHesiloni, Hesiloni akampaapa uAlamu.
Yuda alikuwa baba wa Peresi na Sera kwa Tamari, Peresi baba wa Hezeroni, na Hezeroni baba wa Ramu.
4 UAlamu akampaapa UAminadabu, uAminadabu akampaapa uNasoni, uNasoni akampaapa uSalimoni.
Ramu alikuwa baba wa Aminadabu, Aminadabu baba wa Nashoni, na Nashoni baba wa Salimoni.
5 USalimoni akampaapa uBohasi mwa Lahavu, UBohasi akampaapa UObedi mwa Luti, uObedi akampaapa uYese,
Salimoni alikuwa baba wa Boazi kwa Rahabu, Boazi baba wa Obedi kwa Ruth, Obedi baba wa Yese,
6 ghwope UYese akampaapa Untwa UDavidi. UDavidi akampaapa uSolomoni mwa mukijuuva juno alyale n'dala ghwa Ulia.
Yese alikuwa baba wa mfalme Daudi. Daudi alikuwa baba wa Sulemani kwa mke wa Uria.
7 USolomoi akampaapa uLehoboamu, ULehoboamu akampaapa uAbia, uAbia akampaapa uAsa.
Sulemani alikuwa baba wa Rehoboamu, Rehoboamu baba wa Abiya, Abiya baba wa Asa.
8 uAsa akampaapa uYehoshafati, UYehoshafati akampaapa uYolamu, uYolamu akampaapa uUsia.
Asa alikuwa baba wa Yehoshafati, Yehoshafati baba wa Yoramu, na Yoramu baba wa Uzia.
9 UUsia akampaapa uYotamu, uYotamu akampaapa uAhasi, UAhasi akampaapa uUhesekia.
Uzia alikuwa baba wa Yothamu, Yothamu baba wa Ahazi, Ahazi baba wa Hezekia.
10 uHEsekia akampaapa uMnase, uManase akampaapa uAmoni, ghwope uAmoni akampaapa uYosia.
Hezekia alikuwa baba wa Manase, Manase baba wa Amoni na Amoni baba wa Yosia.
11 uYosia akampaapa uYekonia na vanine unsiki ghuno aVaisilaeli ye vatwalilue ku vuhesia, ku Babeli.
Yosia alikuwa baba wa Yekonia na kaka zake wakati wa kuchukuliwa kwenda Babeli.
12 Ye vatwalilue ku vuhesia ku Babeli, uYekonia akampaapa uSalatieli, uSalatieli akampaapal uSelubabeli.
Na baada ya kuchukuliwa kwenda Babeli, Yekonia alikuwa baba wa Shatieli, Shatieli alikuwa babu yake na Zerubabeli.
13 uSelubabeli akampaapa uAbihudi, uAbihudi akampaapa uEliakimu, uEliakimu akampaapa uAsoli.
Zerubabeli alikuwa baba wa Abiudi, Abiudi baba wa Eliakimu, na Eliakimu baba wa Azori.
14 uAsoli akampaapa uSadoki, uSadoki akampaapa uAkimu, uAkimu akampaapa uEliudi.
Azori alikuwa baba wa Zadoki, Zadoki baba wa Akimu, na Akimu baba wa Eliudi.
15 uEliudi akampaapa uElieseli, uElieseli akampaapa uMatani, ghwope uMatani akampaapa uYakovo.
Eliudi alikuwa baba wa Elieza, Elieza baba wa Matani na Matani baba wa Yakobo.
16 uYkovo akampaapa Yosefu umughoosi ghwa Maliya. UMaliya ghwe juno akampapile uYesu juno ghwe Kilisite.
Yakobo alikuwa baba wa Yusufu mume wa Mariamu, ambaye kwa yeye Yesu alizaliwa, aitwaye Kristo.
17 Lino, kuhuma kwa Abulahamu kufika kwa ntwa uDavidi kwefilyale ifisina kijigho na fine. Kange, kuhuma pa Davidi kufila unsiki ghuno aVaisilaeli vitwalua ku vuhesia ku Babeli, kwefilyale ifisina ifingi kijigho n a fine. Kange, kuhuma unsiki ghuno vitwalua ku Babeli kuhanga kufika unsiki ye iholua uKilisite, kwefilyale ifisina ifingi kijigho na fine.
Vizazi vyote tangu Ibrahimu hadi Daudi vilikuwa vizazi kumi na vinne, kutoka Daudi hadi kuchukuliwa kwenda Babeli vizazi kumi na vinne, na kutoka kuchukuliwa kwenda Babeli hadi Kristo vizazi kumi na vinne.
18 Kuholua kwa Yesu Kilisite kulyale ndiiki. Unguna jonop ilitavua lyake ghwe Maliya, alyalimilue nu Yosefu. Neke ye akyale kutolua alyavoniike kuuti ali nu vukunue ku ngufu sa Mhepo uMwimike.
Kuzaliwa kwa Yesu Kristo kulikuwa kwa namna hii. Mama yake, Mariamu, alichumbiwa na Yusufu, lakini kabla hawajakutana, alionekana kuwa na mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
19 Ulwakuva uYosefu juno alyamulimiile uMaliya alyale mugholofu pamaso gha Nguluve, naakalondagha kuuti ankosie isoni uMaliya. Pe akalamula pikumuleka kisyefu.
Mume wake Yusufu, alikuwa mtu mwenye haki hakutaka kumwaibisha hadharani. Aliamua kusitisha uchumba wake naye kwa siri.
20 Ye alamwile uluo, unyamhola ghwa mtwa uNguluve akam'bonekela mu njosi, akam'buula akati, “Ghwe Yosefu, ghwe mhuma mu kisina ikya ntwa uDavidi, uleke pikwoghopa pikuntoola uMaliya, uLwakuva uvukunue vuno ali navwo, apelilue mu ngufu sa Mhepo uMwimike.
Alipokuwa akifikiri juu ya mambo haya, Malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema,'' Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu kama mkeo, kwa sababu mimba aliyonayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
21 Neke ipaapa umwana un'diimi, ukumpeela ilitavua ili Yesu, ulwakuva ilikuvapokagha avaanhu vaake mu nyivi saave.”
Atajifungua mtoto wa kiume na utamwita jina lake Yesu, kwa maana atawaokoa watu wake na dhambi zao.''
22 Sooni isio siliyavombiike enendikio kukwilanisia ilisio lino uMutwa alyajovile kukilila um'bili ghwake kuuti, “
Yote haya yalitokea kutimizwa kile kilichonenwa na Bwana kwa njia ya nabii, akisema,
23 Lolagha! Umhinja juno naammanyile umughoosi, iiva nu vukunue, ipaapa umwana un'diimi! pe vikumpeela umwana ujuo ilitavua ili Manueli.” Umuluvo ghwa litavua ilio kwekuti, “UNguluve ali palikimo nusue.”
“Tazama, bikira atachukua mimba na kuzaa mtoto wa kiume, na watamwita jina lake Imanueli”— maana yake, “Mungu pamoja nasi.”
24 Yosefu akasisimuka, akavomba ndavule unyamhola ghwa Mutwa vule am'bulile, akantoola uMaliya kuuva n'dala ghwake.
Yusufu aliamka kutoka usingizini na kufanya kama malaika wa Bwana alivyomwamuru na alimchukua kama mkewe.
25 Looli naakaghelile kughona naghwo kuhanga usinki ghuno uMaliya ipaapa umwana un'diimi. Pe uYosefu akampeela umwana ujuo ilitavua ili Yesu.
Hata hivyo, hakulala naye mpaka alipojifungua mtoto wa kiume na alimwita jina lake Yesu.

+ Mataayi 1 >