< Mathayo 10 >

1 Yesu aliwaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa uwezo wa kutoa pepo wachafu na kuponya magonjwa na maradhi yote.
耶穌叫了十二個門徒來,給他們權柄,能趕逐污鬼,並醫治各樣的病症。
2 Majina ya hao mitume kumi na wawili ni haya: wa kwanza ni Simoni aitwae Petro, na Andrea ndugu yake; Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohane ndugu yake;
這十二使徒的名:頭一個叫西門(又稱彼得),還有他兄弟安得烈,西庇太的兒子雅各和雅各的兄弟約翰,
3 Filipo na Bartholomayo, Thoma na Mathayo aliyekuwa mtoza ushuru; Yakobo mwana wa Alfayo, na Thadayo;
腓力和巴多羅買,多馬和稅吏馬太,亞勒腓的兒子雅各,和達太,
4 Simoni Mkanaani, na Yuda Iskarioti ambaye alimsaliti Yesu.
奮銳黨的西門,還有賣耶穌的加略人猶大。
5 Yesu aliwatuma hao kumi na wawili na kuwapa maagizo haya: “Msiende kwa watu wa mataifa mengine, wala msiingie katika mji wa Wasamaria.
耶穌差這十二個人去,吩咐他們說:「外邦人的路,你們不要走;撒馬利亞人的城,你們不要進;
6 Ila nendeni kwa watu wa Israeli waliopotea kama kondoo.
寧可往以色列家迷失的羊那裏去。
7 Mnapokwenda hubirini hivi: Ufalme wa mbinguni umekaribia.
隨走隨傳,說『天國近了!』
8 Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo. Mmepewa bure, toeni bure.
醫治病人,叫死人復活,叫長大痲瘋的潔淨,把鬼趕出去。你們白白地得來,也要白白地捨去。
9 Msichukue mifukoni mwenu dhahabu, wala fedha, wala sarafu za shaba.
腰袋裏不要帶金銀銅錢;
10 Msichukue mkoba wa kuombea njiani, wala koti la ziada, wala viatu, wala fimbo. Maana mfanyakazi anastahili riziki yake.
行路不要帶口袋;不要帶兩件褂子,也不要帶鞋和柺杖。因為工人得飲食是應當的。
11 “Mkiingia katika mji wowote au kijiji, tafuteni humo mtu yeyote aliye tayari kuwakaribisheni, na kaeni naye mpaka mtakapoondoka mahali hapo.
你們無論進哪一城,哪一村,要打聽那裏誰是好人,就住在他家,直住到走的時候。
12 Mnapoingia nyumbani wasalimuni wenyeji wake.
進他家裏去,要請他的安。
13 Kama wenyeji wa nyumba hiyo wakiipokea salamu hiyo, basi, amani yenu itakaa pamoja nao. Lakini ikiwa hawaipokei, basi amani yenu itawarudia ninyi.
那家若配得平安,你們所求的平安就必臨到那家;若不配得,你們所求的平安仍歸你們。
14 Kama mtu yeyote atakataa kuwakaribisheni au kuwasikilizeni, basi mtokapo katika nyumba hiyo au mji huo, yakung'uteni mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao.
凡不接待你們、不聽你們話的人,你們離開那家,或是那城的時候,就把腳上的塵土跺下去。
15 Kweli nawaambieni, Siku ya hukumu mji huo utapata adhabu kubwa kuliko ile iliyoipata miji ya Sodoma na Gomora.
我實在告訴你們,當審判的日子,所多瑪和蛾摩拉所受的,比那城還容易受呢!」
16 “Sasa, mimi nawatuma ninyi kama kondoo kati ya mbwa mwitu. Muwe na busara kama nyoka, na wapole kama njiwa.
「我差你們去,如同羊進入狼群;所以你們要靈巧像蛇,馴良像鴿子。
17 Jihadharini na watu, maana watawapeleka ninyi mahakamani na kuwapiga viboko katika masunagogi yao.
你們要防備人;因為他們要把你們交給公會 ,也要在會堂裏鞭打你們,
18 Mtapelekwa mbele ya watawala na wafalme kwa sababu yangu, mpate kutangaza Habari Njema kwao na kwa mataifa.
並且你們要為我的緣故被送到諸侯君王面前,對他們和外邦人作見證。
19 Basi, watakapowapeleka ninyi mahakamani, msiwe na wasiwasi mtasema nini au namna gani; wakati utakapofika, mtapewa la kusema.
你們被交的時候,不要思慮怎樣說話,或說甚麼話。到那時候,必賜給你們當說的話;
20 Maana si ninyi mtakaosema, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu.
因為不是你們自己說的,乃是你們父的靈在你們裏頭說的。
21 “Ndugu atamsaliti ndugu yake auawe, na baba atamsaliti mwanawe, nao watoto watawashambulia wazazi wao na kuwaua.
弟兄要把弟兄,父親要把兒子,送到死地;兒女要與父母為敵,害死他們;
22 Watu wote watawachukieni kwa sababu ya jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho, ataokolewa.
並且你們要為我的名被眾人恨惡。惟有忍耐到底的必然得救。
23 “Watu wakiwadhulumu katika mji mmoja, kimbilieni mji mwingine. Kweli nawaambieni, hamtamaliza ziara yenu katika miji yote ya Israeli kabla Mwana wa Mtu hajafika.
有人在這城裏逼迫你們,就逃到那城裏去。我實在告訴你們,以色列的城邑,你們還沒有走遍,人子就到了。
24 “Mwanafunzi si mkuu kuliko mwalimu wake, wala mtumishi si mkuu kuliko bwana wake.
學生不能高過先生;僕人不能高過主人。
25 Yatosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumishi kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mkubwa wa jamaa Beelzebuli, je hawatawaita watu wengine wa jamaa hiyo majina mabaya zaidi?
學生和先生一樣,僕人和主人一樣,也就罷了。人既罵家主是別西卜,何況他的家人呢?」
26 “Basi, msiwaogope watu hao. Kila kilichofunikwa kitafunuliwa, na kila kilichofichwa kitafichuliwa.
「所以,不要怕他們;因為掩蓋的事沒有不露出來的,隱藏的事沒有不被人知道的。
27 Ninalowaambieni ninyi katika giza, lisemeni katika mwanga; na jambo mlilosikia likinong'onezwa, litangazeni hadharani.
我在暗中告訴你們的,你們要在明處說出來;你們耳中所聽的,要在房上宣揚出來。
28 Msiwaogope wale wauao mwili, lakini hawawezi kuiua roho. Afadhali zaidi kumwogopa yule awezaye kuuangamiza mwili pamoja na roho katika moto wa Jehanamu. (Geenna g1067)
那殺身體、不能殺靈魂的,不要怕他們;惟有能把身體和靈魂都滅在地獄裏的,正要怕他。 (Geenna g1067)
29 Shomoro wawili huuzwa kwa senti tano. Lakini hata mmoja wao haanguki chini bila kibali cha Baba yenu.
兩個麻雀不是賣一分銀子嗎?若是你們的父不許,一個也不能掉在地上;
30 Lakini kwa upande wenu, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote.
就是你們的頭髮也都被數過了。
31 Kwa hiyo msiogope; ninyi mu wa thamani kuliko shomoro wengi.
所以,不要懼怕,你們比許多麻雀還貴重!」
32 “Kila mtu anayekiri hadharani kwamba yeye ni wangu, mimi pia nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.
「凡在人面前認我的,我在我天上的父面前也必認他;
33 Lakini yeyote atakayenikana hadharani, nami nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.
凡在人面前不認我的,我在我天上的父面前也必不認他。」
34 “Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali upanga.
「你們不要想我來是叫地上太平;我來並不是叫地上太平,乃是叫地上動刀兵。
35 Maana nimekuja kuleta mafarakano kati ya mtu na baba yake, kati ya binti na mama yake, kati ya mkwe na mkwe wake.
因為我來是叫 人與父親生疏, 女兒與母親生疏, 媳婦與婆婆生疏。
36 Na maadui wa mtu ni watu wa nyumbani mwake.
人的仇敵就是自己家裏的人。
37 “Ampendaye baba au mama yake kuliko anipendavyo mimi, hanistahili. Ampendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
「愛父母過於愛我的,不配作我的門徒;愛兒女過於愛我的,不配作我的門徒;
38 Mtu asiyechukua msalaba wake na kunifuata, hanistahili.
不背着他的十字架跟從我的,也不配作我的門徒。
39 Anayeyashikilia maisha yake, atayapoteza; lakini anayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayapata.
得着生命的,將要失喪生命;為我失喪生命的,將要得着生命。」
40 “Anayewakaribisha ninyi, ananikaribisha mimi; na anayenikaribisha mimi, anamkaribisha yule aliyenituma.
「人接待你們就是接待我;接待我就是接待那差我來的。
41 Anayemkaribisha nabii kwa sababu ni nabii, atapokea tuzo la nabii. Anayemkaribisha mtu mwema kwa sababu ni mtu mwema, atapokea tuzo la mtu mwema.
人因為先知的名接待先知,必得先知所得的賞賜;人因為義人的名接待義人,必得義人所得的賞賜。
42 Kweli nawaambieni, yeyote atakayempa mmojawapo wa wadogo hawa kikombe cha maji baridi kwa sababu ni mfuasi wangu, hatakosa kamwe kupata tuzo lake.”
無論何人,因為門徒的名,只把一杯涼水給這小子裏的一個喝,我實在告訴你們,這人不能不得賞賜。」

< Mathayo 10 >