< 1 Wakorintho 4 >

1 Mtu na atuone sisi kuwa ni watumishi wa Kristo tuliokabidhiwa siri za mungu.
Let men this wyse esteme vs eve as the ministers of Christ and disposers of ye secretes of God.
2 Kinachotakiwa kwa yeyote yule aliyekabidhiwa kazi ni kuwa mwaminifu.
Furthermore it is requyred of the disposers that they be founde faithfull.
3 Kwangu mimi si kitu nikihukumiwa na ninyi, au na mahakama ya kibinadamu; wala sijihukumu.
With me is it but a very smal thinge that I shuld be iudged of you ether of (mans daye) No I iudge not myn awne selfe.
4 Dhamiri yangu hainishtaki kwa jambo lolote, lakini hiyo haionyeshi kwamba sina lawama. Bwana ndiye anayenihukumu.
I know nought by my selfe: yet am I not therby iustified. It is the Lorde that iudgeth me.
5 Basi, msihukumu kabla ya wakati wake acheni mpaka Bwana atakapokuja. Yeye atayafichua mambo ya giza yaliyofichika, na kuonyesha wazi nia za mioyo ya watu. Ndipo kila mmoja atapata sifa anayostahili kutoka kwa Mungu.
Therfore iudge no thinge before the tyme vntill the Lorde come which will lighten thinges that are hyd in darcknes and ope the counsels of the hertes. And then shall every man have prayse of God.
6 Ndugu, hayo yote niliyosema juu ya Apolo na juu yangu, ni kielelezo kwenu: kutokana na mfano wangu mimi na Apolo nataka mwelewe maana ya msemo huu: “Zingatieni yaliyoandikwa.” Kati yenu pasiwe na mtu yeyote anayejivunia mtu mmoja na kumdharau mwingine.
These thinges brethre I have described in myn awne person and Apollos for youre sakes that ye myght learne by vs that no man coute of him selfe beyonde that which is above written: that one swell not agaynst another for eny mans cause.
7 Nani amekupendelea wewe? Una kitu gani wewe ambacho hukupewa? Na ikiwa umepewa, ya nini kujivunia kana kwamba hukukipewa?
For who preferreth the? What hast thou that thou hast not receaved? Yf thou have receaved it why reioysest thou as though thou haddest not receaved it?
8 Haya, mmekwisha shiba! Mmekwisha kuwa matajiri! Mmekuwa wafalme bila ya sisi! Naam, laiti mngekuwa kweli watawala, ili nasi pia tuweze kutawala pamoja nanyi.
Now ye are full: now ye are made rych: ye raygne as kinges with out vs: and I wold to god ye dyd raygne that we might raygne with you.
9 Nafikiri Mungu ametufanya sisi mitume tuwe watu wa mwisho kabisa, kama watu waliohukumiwa kuuawa, maana tumekuwa tamasha mbele ya ulimwengu wote, mbele ya malaika na watu.
Me thinketh that God hath set forth vs which are Apostles for the lowest of all as it were me appoynted to deeth. For we are a gasyngestocke vnto the worlde and to ye angels and to men.
10 Sisi ni wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi ni wenye busara katika kuungana na Kristo! Sisi ni dhaifu, ninyi ni wenye nguvu. Ninyi mnaheshimika, sisi tunadharauliwa.
We are foles for Christes sake and ye are wyse thorow Christ. We are weake and ye are stroge. Ye are honorable and we are despised.
11 Mpaka dakika hii, sisi tuna njaa na kiu, hatuna nguo, twapigwa makofi, hatuna malazi.
Eve vnto this daye we honger and thyrst and are naked and are boffetted wt fistes and have no certayne dwellinge place
12 Tena twataabika na kufanya kazi kwa mikono yetu wenyewe. Tukitukanwa, tunawatakia baraka; tukidhulumiwa, tunavumilia;
and laboure workinge with oure awne hondes. We are revysed and yet we blesse. We are persecuted and suffer it.
13 tukisingiziwa, tunajibu kwa adabu. Mpaka sasa tumetendewa kama uchafu wa dunia; na kwa kila mtu sisi ni takataka!
We are evyll spoken of and we praye. We are made as it were the filthynes of the worlde the ofscowringe of all thinges even vnto this tyme.
14 Siandiki mambo haya kwa ajili ya kuwaaibisha ninyi, bali kwa ajili ya kuwafundisheni watoto wangu wapenzi.
I write not these thinges to shame you: but as my beloved sonnes I warne you.
15 Maana hata kama mnao maelfu ya walezi katika maisha yenu ya Kikristo, baba yenu ni mmoja tu, kwani katika maisha ya Kikristo mimi ndiye niliyewazaeni kwa kuihubiri Habari Njema.
For though ye have ten thousande instructours in Christ: yet have ye not many fathers. In Christ Iesu I have begotten you thorowe ye gospell.
16 Kwa hiyo, nawasihi: fuateni mfano wangu.
Wherfore I desyre you to folowe me.
17 Ndiyo maana nimemtuma Timetheo kwenu. Yeye ni mtoto wangu mpenzi na mwaminifu katika Bwana. Atawakumbusheni njia ninayofuata katika kuishi maisha ya Kikristo; njia ninayofundisha kila mahali katika makanisa yote.
For this cause have I sent vnto you Timotheus which is my deare sonne and faithfull in the Lorde which shall put you in remembrauce of my wayes which I have in Christ eve as I teache every where in all congregacios.
18 Baadhi yenu wameanza kuwa na majivuno wakidhani kwamba sitakuja tena kwenu.
Some swell as though I wolde come no more at you.
19 Lakini, Bwana akipenda, nitakuja kwenu upesi; na hapo ndipo nitakapojionea mwenyewe, sio tu kile wanachoweza kusema hao wenye majivuno, bali pia kila wanachoweza kufanya.
But I will come to you shortely yf God will: and will knowe not ye wordes of the which swell but ye power:
20 Maana Utawala wa Mungu si shauri la maneno matupu, bali ni nguvu.
for ye kyngdome of God is not in wordes but in power.
21 Mnapendelea lipi? Nije kwenu na fimbo, ama nije na moyo wa upendo na upole?
What will ye? Shall I come vnto you with a rodde or els in love and in the sprete of mekenes?

< 1 Wakorintho 4 >