< Hesabu 7 >

1 Siku ambayo Musa alikamilsha masikani, alitia mafuta na kuiweka wakfu kwa BWANA, pamoja na mapambo yake. Aliifanyia hivyo madhabahu na vyombo vyake. Aliitia mafuta na kuiweka wakfu kwa BWANA.
ויהי ביום כלות משה להקים את המשכן וימשח אתו ויקדש אתו ואת כל כליו ואת המזבח ואת כל כליו וימשחם ויקדש אתם
2 Siku hiyo, viongozi wa Israeli na wale vichwa vya familia za mababu walitoa sadaka. Hawa wanaume walikuwa viongozi wa makabila. Walisaidia kuhesabu watu kwenye ile sensa.
ויקריבו נשיאי ישראל ראשי בית אבתם הם נשיאי המטת הם העמדים על הפקדים
3 Walileta sadaka zao kwa BWANA. Walileta magari sita yaliyofunikwa na mafahari kumi na mbili. Walileta gari moja kwa kila viongozi wawili, kila kiongozi alileta fahari moja. Walileta vitu hivi mbele ya masikani.
ויביאו את קרבנם לפני יהוה שש עגלת צב ושני עשר בקר--עגלה על שני הנשאים ושור לאחד ויקריבו אותם לפני המשכן
4 Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia,
ויאמר יהוה אל משה לאמר
5 “Uzipokee hizo sadaka kutoka kwao na uzitumie kwa matumizi ya kazi ya hema ya kukutania. Uwape hizo sadaka Walawi, kwa kila mmoja kadri ya uhitaji wa kazi yake.”
קח מאתם והיו לעבד את עבדת אהל מועד ונתתה אותם אל הלוים איש כפי עבדתו
6 Musa akayatwaa yale magari na mafahari. na kuwapatia Walawi.
ויקח משה את העגלת ואת הבקר ויתן אותם אל הלוים
7 Aliwapa magari mawili na mafahari wanne wale wa uzao wa Gerishoni, kwa sababu ndivyo kazi yao ilivyohitaji.
את שתי העגלות ואת ארבעת הבקר--נתן לבני גרשון כפי עבדתם
8 Aliwapatia uzao wa Merari magari manne na mafahari nane, chini ya uangalizi wa Ithamari mwana wa Haruni kuhani. Alifanya hivi kwa sababu ya uhitaji wa kazi yao.
ואת ארבע העגלת ואת שמנת הבקר--נתן לבני מררי כפי עבדתם ביד איתמר בן אהרן הכהן
9 Lakini wale wa uzao wa Kohathi hakuwapa chochote kwa sababu wao waliangalia vitu vtakatifu amabvyo vilipaswa vibebwe mabagani mwao, siyo kwa magari.
ולבני קהת לא נתן כי עבדת הקדש עלהם בכתף ישאו
10 Viongozi walitoa bidhaa zo zingine kwa ajili ya kuwekwa wakfu kwa madhabahu katika siku ile ambayo Musa aliitia mafuta madhabahu. Viongozi walitoa sadaka zao mbele ya madhabahu hiyo.
ויקריבו הנשאים את חנכת המזבח ביום המשח אתו ויקריבו הנשיאם את קרבנם לפני המזבח
11 BWANA akasema na Musa, “kila kiongozi atatoa sadaka kwa siku yake kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu.”
ויאמר יהוה אל משה נשיא אחד ליום נשיא אחד ליום יקריבו את קרבנם לחנכת המזבח
12 Katika siku ya kwanza, Nashoni mwana wa Aminadabu, wa kabila ya Yuda, alitoa sadaka yake.
ויהי המקריב ביום הראשון--את קרבנו נחשון בן עמינדב למטה יהודה
13 Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli moja ya fedha ambayo uzito wake ni shekeli sabini, kwa kipimo cha mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
וקרבנו קערת כסף אחת שלשים ומאה משקלה מזרק אחד כסף שבעים שקל בשקל הקדש שניהם מלאים סלת בלולה בשמן--למנחה
14 Pia alimpa unga wa dhahabu kiasi cha bakuli moja chenye uzani wa shekeli kumi kilichojaa ubani
כף אחת עשרה זהב מלאה קטרת
15 Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mchanga, kondoo dume mmoja na mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja.
פר אחד בן בקר איל אחד כבש אחד בן שנתו--לעלה
16 Alitoa beberu kama kama sadaka ya hatia.
שעיר עזים אחד לחטאת
17 Alitoa makisai mbili, kondoo waume watano, beberu watano na wanakondoo dume watano wenye umri wa mwaka mmoja mmoja, kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa sadaka ya Nashoni mwana wa Aminadabu.
ולזבח השלמים בקר שנים אילם חמשה עתודים חמשה כבשים בני שנה חמשה זה קרבן נחשון בן עמינדב
18 Siku ya pili, Nethanel mwana wa Zuari, kiongozi wa Isakari, alitoa sadaka yake.
ביום השני הקריב נתנאל בן צוער--נשיא יששכר
19 Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha ya uzito wa shekeli130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa sheli sabini, kwa kipimo cha mahali patakatifu. Viyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kwa sadaka ya unga.
הקרב את קרבנו קערת כסף אחת שלשים ומאה משקלה מזרק אחד כסף שבעים שקל בשקל הקדש שניהם מלאים סלת בלולה בשמן--למנחה
20 Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzito wa shekeli kumi, iliyojaa ubani.
כף אחת עשרה זהב מלאה קטרת
21 Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mchanga, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo mmoja dume.
פר אחד בן בקר איל אחד כבש אחד בן שנתו--לעלה
22 Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
שעיר עזים אחד לחטאת
23 Alitoa makisai wawili, Kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka ya amani. Hiii likuwa sadaka ya Nethaneli mwana wa Zuari.
ולזבח השלמים בקר שנים אילם חמשה עתדים חמשה כבשים בני שנה חמשה זה קרבן נתנאל בן צוער
24 Siku ya tatu, Eliabu mwana wa Heloni, kiongozi wa uzao wa Zabuloni alitoa sadaka yake.
ביום השלישי נשיא לבני זבולן--אליאב בן חלן
25 Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha lenye uzito wa shekeli sabini kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. vyombo vyote hivi vilikuwa vimeja unga mwembemba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
קרבנו קערת כסף אחת שלשים ומאה משקלה מזרק אחד כסף שבעים שקל בשקל הקדש שניהם מלאים סלת בלולה בשמן--למנחה
26 Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
כף אחת עשרה זהב מלאה קטרת
27 Alitoa sadaka ya fahari mchanga, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume mmoja.
פר אחד בן בקר איל אחד כבש אחד בן שנתו--לעלה
28 Alitoa beberu mmoja kama sadaka ya dhambi.
שעיר עזים אחד לחטאת
29 Alitoa makisai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja. kuwa sadaka ya amani. Hii ilikuwa sadaka ya Eliabu mwana Heloni.
ולזבח השלמים בקר שנים אילם חמשה עתדים חמשה כבשים בני שנה חמשה זה קרבן אליאב בן חלן
30 Siku ya nne, Elizuri mwana wa shedeuri, kiongozi wa uzao wa Reubeni, alitoa sadaka yake.
ביום הרביעי נשיא לבני ראובן--אליצור בן שדיאור
31 Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo hivi vyote vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
קרבנו קערת כסף אחת שלשים ומאה משקלה מזרק אחד כסף שבעים שקל בשקל הקדש שניהם מלאים סלת בלולה בשמן--למנחה
32 Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichoo jaa ubani.
כף אחת עשרה זהב מלאה קטרת
33 Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga, mwanakondoo dume mmoja mchanga wa mwaka mmoja.
פר אחד בן בקר איל אחד כבש אחד בן שנתו--לעלה
34 Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.
שעיר עזים אחד לחטאת
35 Alitoa maksai wawili, kondoo dume watano wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ilikuwa sadaka ya Elizuri mwana wa Shedeuri.
ולזבח השלמים בקר שנים אילם חמשה עתדים חמשה כבשים בני שנה חמשה זה קרבן אליצור בן שדיאור
36 Siku ya tano, Shelumieli mwana wa Zurishadai, kiongozi wa uzao wa Simeoni, alitoa sadaka yake.
ביום החמישי נשיא לבני שמעון--שלמיאל בן צורישדי
37 Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shaekali 130 na bakuli mojala fedha lenye uzani wa shekeli sabini kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
קרבנו קערת כסף אחת שלשים ומאה משקלה מזרק אחד כסף שבעים שקל בשקל הקדש שניהם מלאים סלת בלולה בשמן--למנחה
38 Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, uliojaa ubani.
כף אחת עשרה זהב מלאה קטרת
39 Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mchanga, dume la kondoo, na dume la mwanakondoo la mwaka mmoja.
פר אחד בן בקר איל אחד כבש אחד בן שנתו--לעלה
40 Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.
שעיר עזים אחד לחטאת
41 Alitao maksai wawili, dume wawili wa kondoo, beberu watano, na dume watano wa wanakondoo wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka y amani. Hiindiyo iliyokuwa sadka ya Shelumei mwana wa Zurishadai.
ולזבח השלמים בקר שנים אילם חמשה עתדים חמשה כבשים בני שנה חמשה זה קרבן שלמיאל בן צורישדי
42 Siku ya sita, Eliasafu mwana wa Deuli, kiongozi wa uzao wa Gadi, alitoa sadaka yake.
ביום הששי נשיא לבני גד--אליסף בן דעואל
43 Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli la shaba lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo hivi vyote vilikuwa vimejaa unga mwembemba uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya unga.
קרבנו קערת כסף אחת שלשים ומאה משקלה מזרק אחד כסף שבעים שקל בשקל הקדש שניהם מלאים סלת בלולה בשמן--למנחה
44 Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
כף אחת עשרה זהב מלאה קטרת
45 Alitoa sadaka ya kuteketezwa ya fahari changa, kondoo dume mmoja, na dume la mwanakondoo mmoja wa mwaka mmoja.
פר אחד בן בקר איל אחד כבש אחד בן שנתו--לעלה
46 Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
שעיר עזים אחד לחטאת
47 Alitoa maksai wawili, dume watano wa kondoo, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Eliasafu mwana wa Deuli.
ולזבח השלמים בקר שנים אילם חמשה עתדים חמשה כבשים בני שנה חמשה זה קרבן אליסף בן דעואל
48 Siku ya saba, Elishama mwana wa Amihudi, kiongozi wa uzao wa Efraimu, alitoa sadaka yake.
ביום השביעי נשיא לבני אפרים--אלישמע בן עמיהוד
49 Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo hivi vyote ilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
קרבנו קערת כסף אחת שלשים ומאה משקלה מזרק אחד כסף שבעים שקל בשקל הקדש שניהם מלאים סלת בלולה בשמן--למנחה
50 Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu, kilichojaa ubani
כף אחת עשרה זהב מלאה קטרת
51 Alitoa sadaka ya kuteketezwa, fahari mmoja, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja.
פר אחד בן בקר איל אחד כבש אחד בן שנתו--לעלה
52 Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
שעיר עזים אחד לחטאת
53 Alitoa maksai wawili, kondo dume watano, beberu watano, na na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sdaka ya Elishama mwana wa Amidu.
ולזבח השלמים בקר שנים אילם חמשה עתדים חמשה כבשים בני שנה חמשה זה קרבן אלישמע בן עמיהוד
54 Siku y a nane, Gamaliel mwana wa Pedazuri, kiongozi wa uzao wa Manase, alitoa sadaka yake.
ביום השמיני נשיא לבני מנשה--גמליאל בן פדהצור
55 Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
קרבנו קערת כסף אחת שלשים ומאה משקלה מזרק אחד כסף שבעים שקל בשקל הקדש שניהם מלאים סלת בלולה בשמן--למנחה
56 Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
כף אחת עשרה זהב מלאה קטרת
57 Alitoa sadaka ya kuteketezwa ya fahari mmoja, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja.
פר אחד בן בקר איל אחד כבש אחד בן שנתו--לעלה
58 Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
שעיר עזים אחד לחטאת
59 Alitoa maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Gamaliel mwana wa Pedazuri.
ולזבח השלמים בקר שנים אילם חמשה עתדים חמשה כבשים בני שנה חמשה זה קרבן גמליאל בן פדהצור
60 Siku ya tisa, Abidani mwana wa Gidioni, kiongozi wa uzao wa Benjamini, alitoa sadaka yake.
ביום התשיעי נשיא לבני בנימן--אבידן בן גדעני
61 Sadaka yake ilikuwa sahani moja yafedha yenye uzani wa sheli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzito wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
קרבנו קערת כסף אחת שלשים ומאה משקלה מזרק אחד כסף שבעים שקל בשקל הקדש שניהם מלאים סלת בלולה בשמן--למנחה
62 Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
כף אחת עשרה זהב מלאה קטרת
63 Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja.
פר אחד בן בקר איל אחד כבש אחד בן שנתו--לעלה
64 Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
שעיר עזים אחד לחטאת
65 Alitoa makisai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Abidani mwana wa Gidioni.
ולזבח השלמים בקר שנים אילם חמשה עתדים חמשה כבשים בני שנה חמשה זה קרבן אבידן בן גדעני
66 Siku ya kumi, Ahizeri mwana wa Amishadai kiongozi wa Dani alitoa sadaka yake.
ביום העשירי נשיא לבני דן--אחיעזר בן עמישדי
67 Alitoa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shaekeli 130 na bakuli moja lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
קרבנו קערת כסף אחת שלשים ומאה משקלה מזרק אחד כסף שבעים שקל בשקל הקדש שניהם מלאים סלת בלולה בשמן--למנחה
68 Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzito wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
כף אחת עשרה זהב מלאה קטרת
69 Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga, dume moja la kondoo, na dume moja la mwanakondoo wa mwaka mmoja.
פר אחד בן בקר איל אחד כבש אחד בן שנתו--לעלה
70 Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.
שעיר עזים אחד לחטאת
71 Alitoa maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja, kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Ahizeri mwana wa Amishadai.
ולזבח השלמים בקר שנים אילם חמשה עתדים חמשה כבשים בני שנה חמשה זה קרבן אחיעזר בן עמישדי
72 Siku ya kumi na moja. Pagieli mwana wa Okrani kiongozi wa uzao wa Asheri alaitoa sadaka yake.
ביום עשתי עשר יום נשיא לבני אשר--פגעיאל בן עכרן
73 Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabani, kwa kipimo cha shekeli ya mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi ilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
קרבנו קערת כסף אחת שלשים ומאה משקלה מזרק אחד כסף שבעים שקל בשקל הקדש שניהם מלאים סלת בלולה בשמן--למנחה
74 Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
כף אחת עשרה זהב מלאה קטרת
75 Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga. dume la kondoo moja, dume moja la mwanakondoo wa mwaka mmoja.
פר אחד בן בקר איל אחד כבש אחד בן שנתו--לעלה
76 Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.
שעיר עזים אחד לחטאת
77 Alitoa maksai wawili, dume watano wa kondoo, na wanakondoo dume watano kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Pagieli mwana wa Okrani.
ולזבח השלמים בקר שנים אילם חמשה עתדים חמשה כבשים בני שנה חמשה זה קרבן פגעיאל בן עכרן
78 Siku ya kumi na mbili., Ahira mwana wa Enani, kiongozi wa uzao wa Naftali, alitoa sadaka yake.
ביום שנים עשר יום נשיא לבני נפתלי--אחירע בן עינן
79 Sadaka yake ailikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shaekeli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba ulichanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
קרבנו קערת כסף אחת שלשים ומאה משקלה מזרק אחד כסף שבעים שקל בשקל הקדש שניהם מלאים סלת בלולה בשמן--למנחה
80 Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
כף אחת עשרה זהב מלאה קטרת
81 Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga, dume moja la kondoo, na mwanakondoo dume moja wa mwaka mmoja.
פר אחד בן בקר איל אחד כבש אחד בן שנתו--לעלה
82 Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.
שעיר עזים אחד לחטאת
83 Alitoa maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Ahra mwana wa Enani.
ולזבח השלמים בקר שנים אילם חמשה עתדים חמשה כבשים בני שנה חמשה זה קרבן אחירע בן עינן
84 Viongozi wa Israeli waliviweka wakfu hivi vitu vyote siku ambayo Musa alimimina mafuta kwenye madhabahu. Waliziweka wakfu zile sahani kumi na mbili za fedha, Bakuli kumi na mbili za fedha, na vijiko kumi na vili vya dhahabu.
זאת חנכת המזבח ביום המשח אתו מאת נשיאי ישראל קערת כסף שתים עשרה מזרקי כסף שנים עשר כפות זהב שתים עשרה
85 Zile sahani za fedha kila moja ilikuwa na uzani wa shaekeli 130 na kila bakuli ye fedha ilikuwa na uzani wa shekeli sabini. Vyombo vyote vya fedh vilikuwa na ujumla ya uzani wa shekeli 2, 400, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu.
שלשים ומאה הקערה האחת כסף ושבעים המזרק האחד כל כסף הכלים אלפים וארבע מאות בשקל הקדש
86 Vile vijiko vya dhahabu vilivyokuwa vimejaa ubani, vilikuwa na uzani wa shekeli kumi kila kimoja. Vijiko vyote vya dhahabu vilikuwa na uzani wa shekeli 120.
כפות זהב שתים עשרה מלאת קטרת עשרה עשרה הכף בשקל הקדש כל זהב הכפות עשרים ומאה
87 Waliwatenga wanyama wote kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, fahari kumi na wawili, kondoo dume kumi na wawili, na wanakondoo dume kumi na wawili wa mwaka mmoja mmoja. Walitoa sadaka yao ya unga. Walitoa beberu kumi na wawili kuwa sadaka ya dhambi.
כל הבקר לעלה שנים עשר פרים אילם שנים עשר כבשים בני שנה שנים עשר--ומנחתם ושעירי עזים שנים עשר לחטאת
88 Kutokana na ng'ombe zao, walitoa fahari ishirini na nne, kondoo dume sitini beberu sitini, na wanakondoo dume sitini wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ilikuwa kwa ajiliya kuiweka wafu ile madhabahu baada ya kumiminiwa mafuta.
וכל בקר זבח השלמים עשרים וארבעה פרים אילם ששים עתדים ששים כבשים בני שנה ששים זאת חנכת המזבח אחרי המשח אתו
89 Musa alipoingia kwenye hema ya kukutania kusema na BWANA, ndipo alipoisikia sauti yake ikisema naye. BWANA alinena naye kutoka juu ya kiti cha rehema kilichokuwa juu ya sanduku la ushahidi, kutoka katikati ya makerubi. Alinena naye.
ובבא משה אל אהל מועד לדבר אתו וישמע את הקול מדבר אליו מעל הכפרת אשר על ארן העדת מבין שני הכרבים וידבר אליו

< Hesabu 7 >