< Luka 21 >

1 Yesu alitazama akawaona wanaume matajiri waliokuwa wanaweka zawadi zao kwenye hazina.
Yesun atilinga am'bweni analome matajiri, bababile kababika zawadi yabe mu akiba.
2 Akamuona mjane mmoja masikini akiweka senti zake mbili.
Amweni ywa wilikwe yumo maskini kabika senti yake ibele.
3 Hivyo akasema, “Kweli nawaambieni, huyu Mjane maskini ameweka nyingi kuliko wengine wote.
Nga nyo ngabaya kweli wendakuwabakia, hayu ngwelekwa maskini abika yanambone kuliko benge boti.
4 Hawa wote wametoa hizi zawadi kutoka katika vingi walivyonavyo. Lakini huyu mjane, katika umaskini wake, ametoa fedha zote alizokuwa nazo kwa ajili ya kuishi kwake.”
Haba boti bapiyite bayi zawadi buka katika yanambone yababile nayo, lakini hayu n'gwelekwa katika umaskini wake, apiyite mbanje yoti yabile nayo kwaajili ya lama kwake,”
5 Wakati wengine walipokuwa wakisema juu ya hekalu, namna lilivyokuwa limepambwa na mawe mazuri na matoleo, alisema,
Wakati wenge pababile kababaya usu hekalu, namna mwalibile litipambilwe na maliwe yananoga ni matoleo atibaya,
6 “Kwa habari ya mambo haya mnayoyaona, siku zitakuja ambazo hakuna jiwe moja ambalo litaachwa juu ya jiwe jingine ambalo halitabomolewa.”
“Kwa habari ya makowe aga mwamugabona, machuba gaicha ambayo ntopo liwe limo ambalo lalekelwa panani ya liwe lyinge ambalo lya bomolelwa kaa,”
7 Hivyo wakamuuliza, wakasema, “Mwalimu, mambo haya yatatokea lini? Na nini ni itakuwa ishara kwamba haya mambo yako karibu kutokea?”
Nga nyoo, batikunnokia babayite, “Mwalimu, makowe aga gapita lichuba gani? namani yabaa ishara kwamba aga makowe gai karibu pitya.
8 Yesu akajibu, “Muwe waangalifu kwamba msidanganywe. Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, 'Mimi ndiye, 'na 'Muda umekaribia'. Msiwafuate.
Yesu ayangwi, “Mube aangalifu kwamba kana mukongelwe, kwa sababu baingi baicha kwa lina lyangu, kababaya Nenga nga naywembe, ni muda utikaribia.'kana muakengame.
9 Mkisikia vita na vuruguvurugu msiogope, kwa sababu haya mambo lazima yatokee kwanza, lakini mwisho hautatokea upesi.”
Mana muyowine vita ni vurugu vurugu kana mwayogope, kwa sababu aga makowe agapiti kwanza lakini mwisho wapitya kwaa upesi.”
10 Kisha akawaambia, “Taifa litainuka kupigana na taifa jingine, na ufalme juu ya ufalme mwingine.
Kai ababakiye, Taifa lakakatuka kumbwana ni taifa lenge, ufalme ni ufalme wenge.
11 Kutakuwa na matetemeko makubwa, na njaa na tauni katika maeneo mbalimbali. Kutakuwa na matukio ya kutisha na ishara za kutisha kutoka mbinguni.
Pabaa ni malendemo makulu, ni njala ni tauni katika maeneo mbalembale bapaa matukio yatisha ni ishara yatisha buka kumaunde.
12 Lakini kabla ya mambo haya yote, wataweka mikono yao juu yenu na kuwatesa, kuwapeleka kwenye masinagogi na magereza, kuwaleta mbele za wafalme na wenye mamlaka kwa sababu ya jina langu.
Lakoni kabla makowe aga goti, babika maboko gabe panani yinuni kubatesa kubapelekanga mu'masinagogi ni mumagereza, kunneta nnongi ya ufalme ni bene mamlaka kwasababu ya lina lyangu.
13 Hii itawafungulia fursa kwa ushuhuda wenu.
Ayii ipakunyoghulyanga mwenga nafasi kwa ushuhuda winu.
14 Kwahiyo amueni mioyoni mwenu kutoandaa utetezi wenu mapema,
Kwaiyo muamue mumyoyo yinu aandaa kwaa kwinu mapema,
15 kwa sababu nitawapa maneno na hekima, ambayo adui zenu wote hawataweza kuipinga au kuikana.
Kwasababu nampea maneno aga hekima, ambago adui zinu boti bawecha kwaa kuipinga au kuikana.
16 Lakini mtakataliwa pia na wazazi wenu, ndugu zenu, jamaa zenu na rafiki zenu, na watawaua baadhi yenu.
Lakini mwa kanilwa kae ni azazi binu anunabinu, alongo binu ni mabwiga ni bapakumulaga baadhi yinu.
17 Mtachukiwa na kila mmoja kwa sababu ya jina langu.
Mwatolelwa ni kila yumo kwa sababu ya lina lyangu.
18 Lakini hakuna hata unywele mmoja wa vichwa vyenu utakaopotea.
Lakini ntopo hata unywi kwaa umo wa mitwe yinu waupala oba.
19 Katika kuvumilia mtaziponya nafsi zenu.
Katika vumilia mwaipanga nafsi yinu.
20 Mtakapoona Yerusalemu imezungukwa na majeshi, basi jueni kwamba uharibifu wake umekaribia.
Pampala bona Yerusalemu baitindiike majeshi, basi mutange kwamba ualibifu wake ukalibiye.
21 Hapo wale walioko Yudea wakimbilie milimani, na wale walioko katikati ya jiji waondoke, na msiwaache walioko vijijini kuingia.
Hapo balo babile Yudea babutukii muitumbii, ni balo bababile pakatikati ya jiji babuke, ni kana mwaleke bababile muijiji jingya.
22 Maana hizi ni siku za kisasi, ili kwamba mambo yote yaliyoandikwa yapate kutimilika.
Mana aga nga machuba ga kisasi, linga kwamba makowe goti gagaandikilwe gapate timya.
23 Ole ni kwa wale walio na mimba na kwa wale wanyonyeshao katika siku hizo! Kwa maana kutakuwa na adha kuu juu ya nchi, na ghadhabu kwa watu hawa.
Ole kwa balo bene ndumbo ni kwa balo babayongeya katika machuba aga! kwa maana pabaa ni tabu nkolo muilambo ni nyongo kwa bandu haba.
24 Na wataanguka kwa ncha ya upanga na watachukuliwa mateka kwa mataifa yote, na Yerusalem itakanyagwa na watu wa mataifa, mpaka wakati wa watu wa mataifa utakapotimilika.
Ni batumbuka kwa ncha ya lipanga na batolelwa mateka kwa mataifa goti, ni Yerusalemu yalibatilwa ni bandu ba mataifa, mpaka wakati wa bandu ba mataifa paupala timilika.
25 Kutakuwa na ishara katika jua, mwezi na nyota. Na katika nchi kutakuwa na dhiki ya mataifa, katika kukata tamaa kutokana na mlio wa bahari na mawimbi.
Yapanga ni ishara katika liumu, mwei ni ndondwa. Ni katika ilambo papabaa ni dhiki ya mataifa, katika kata tamaa bukana lilobe lya habari ni mawimbi.
26 Kutakuwa na watu wakizimia kwa hofu na katika kutarajia mambo yatakoyo tokea juu ya dunia. Kwa maana nguvu za mbingu zitatikiswa.
Panga ni bandu kabainduka kwa yogopa ni katika tarajia mambo gagapita duniani. Kwa maana ngupu ya mbingu ya tikwa tikwa.
27 Kisha watamwona Mwana wa Adamu akija mawinguni katika nguvu na utukufu mkuu.
Nga bamona mwana wa Adamu kaicha kumaunde katika ngupu ni utikufu mkulu.
28 Lakini mambo haya yatakapoanza kutokea, simameni, inueni vichwa vyenu, kwa sababu ukombozi wenu umesogea karibu.”
Lakini makowe aga gapatumbwa pitya muyimee mukakatuye mitwe yinu kwa sababu kombolelwa kwinu kwanda egelwa karibu.”
29 Yesu akawaambia kwa mfano, “Uangalieni mtini, na miti yote.
Yesu aabakiye kwa mfano, “Muulinge mtini, ni mikongo yoti.
30 Inapotoa machipukizi, mnajionea wenyewe na kutambua kwamba kiangazi tayari kiko karibu.
Paiipuka, mwenda kuiboniya mwabene ni tanga kwamba mpenja tayari ui karibu.
31 Vivyo hivyo, mnapoona mambo haya yanatokea, ninyi tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu umekaribia.
Nyonyo, pamona makowe aga kagapitya mwenga mutange ya kuwa ufalme wa Nnongo utikaribiya.
32 Kweli, nawaambieni, kizazi hiki hakitapita, mpaka mambo haya yote yatakapotokea.
Kweli, nenda kuwabakiya, ubeleko wuno wapeta kwaa, mpaka mambo aga goti mpaka gapita kwaa.
33 Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Kumaunde ni kilambo gapeta, lakini maneno gangu gapita kwaa kabisa.
34 Lakini jiangalieni wenyewe, ili kwamba mioyo yenu isije ikalemewa na ufisadi, ulevi, na mahangaiko ya maisha haya. Kwa sababu ile siku itawajia ghafla
Lkini muilinge mwa bene linga kwamba mioyo ginu kana yalemewa ni ufisadi, ulevi, ni mahangaiko ga maisha aga. Kwa sababu lilo lichoba yabaichilya gafula.
35 kama mtego. Kwasababu itakuwa juu ya kila mmoja aishiye katika uso wa dunia nzima.
Kati ntego, kwa sababu yabaa kwa kila yumo ywaishi katika kuminyo ya kilambo choti.
36 Lakini mwe tayari wakati wote, mwombe kwamba mtakuwa imara vya kutosha kuyaepuka haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.”
Lakini mube tayari wakati woti, mulobe kwamba mwaba imara ya kutosha kugaepuka aga goti pagapita, na yima nnongi ya mwana wa Adamu.”
37 Hivyo wakati wa mchana alikuwa akifundisha hekaluni na usiku alitoka nje, na kwenda kukesha katika mlima unaoitwa wa Mzeituni.
Nga nyo wakati wa mutwekati abile kafundisha muhekalu ni kiloo apitike panja ni yenda keleka katika kitumbi chakikemelwa cha Mizeituni.
38 Watu wote walimjia asubuhi na mapemaili kumsikiliza ndani ya hekalu.
Bandu boti bamwichi kwaa kindai na mapema linga kumpikaniya nkati ya hekalu.

< Luka 21 >