< Ayubu 30 >

1 Sasa vijana wananidhihaki - vijana ambao baba zao wasingeweza hata kuwahudumia mbwa wa kundi langu.
但如今,比我年少的人戲笑我; 其人之父我曾藐視, 不肯安在看守我羊群的狗中。
2 Kwa kweli, nguvu za mikono ya baba zao, zingenisaidia nini - watu ambao hawakuwa na nguvu wakati wa kukua kwao?
他們壯年的氣力既已衰敗, 其手之力與我何益呢?
3 Walidhoofishwa na umasikini na njaa; walisaga nchi kavu mafichoni.
他們因窮乏飢餓,身體枯瘦, 在荒廢淒涼的幽暗中齦乾燥之地,
4 Walichuma mche chumvi na majani ya vichaka; mizizi ya mti wa ufagio ilikuwa ndiyo chakula chao.
在草叢之中採鹹草, 羅騰的根為他們的食物。
5 Waliondolewa miongoni mwa watu waliopiga kelele nyuma yao kama ambavyo mtu angempigia kelele mwizi.
他們從人中被趕出; 人追喊他們如賊一般,
6 Hivyo walipaswa kuishi katika mabonde ya mto, katika mashimo ya ardhi na miamba.
以致他們住在荒谷之間, 在地洞和巖穴中;
7 Walilia kwa uchungu porini kama punda; chini ya vichaka walikutana.
在草叢中叫喚, 在荊棘下聚集。
8 Walikuwa uzao wa wapumbavu, hakika, wa watu wasiofaa; waliondolewa duniani kama waarifu.
這都是愚頑下賤人的兒女; 他們被鞭打,趕出境外。
9 Lakini sasa, nimekua sababu ya wimbo wa dhihaka kwa wana wao; hakika, nimekuwa mzaa kwao.
現在這些人以我為歌曲, 以我為笑談。
10 Wananichukia na kusimama mbali nami; hawaachi kunitemea usoni.
他們厭惡我,躲在旁邊站着, 不住地吐唾沫在我臉上。
11 Kwa maana Mungu ameondoa kamba katika upinde wangu na amenipiga, na hivyo watu hawa wanashindwa kujizuia mbele yangu.
鬆開他們的繩索苦待我, 在我面前脫去轡頭。
12 Kundi la vijana wabaya wanashambulia nguvu zangu; wananiondolea mbali na kukusanya kinyume changu rundo la kuhusuru.
這等下流人在我右邊起來, 推開我的腳,築成戰路來攻擊我。
13 Wanaharibu maisha yangu; wanapeleka mbele maangamizi yangu, watu wasio na wakuwazuia.
這些無人幫助的, 毀壞我的道,加增我的災。
14 Wanakuja kinyume changu kama jeshi katika tundu pana katika ukuta wa mji; katikati ya maangamizi wanajizungusha juu yangu.
他們來如同闖進大破口, 在毀壞之間滾在我身上。
15 Hofu zimeniandama; heshima yangu imeondolewa mbali nami kama kwa upepo; mafanikio yangu yameondolewa kama wingu.
驚恐臨到我, 驅逐我的尊榮如風; 我的福祿如雲過去。
16 Sasa uhai wangu umeondolewa ndani yangu; siku nyingi za maumivu zimenipita.
現在我心極其悲傷; 困苦的日子將我抓住。
17 Mifupa inauma ndani yangu wakati wa usiku; maumivu yanayonisaga hayaishi.
夜間,我裏面的骨頭刺我, 疼痛不止,好像齦我。
18 Nguvu kuu ya Mungu imeshika mavazi yangu; yananizunguka kama kala ya vazi langu.
因上帝的大力,我的外衣污穢不堪, 又如裏衣的領子將我纏住。
19 Amenitupa matopeni; nimekuwa kama vumbi na majivu.
上帝把我扔在淤泥中, 我就像塵土和爐灰一般。
20 Nakulilia wewe, Mungu, lakini haunijibu; ninasimama, nawe unaniangalia tu.
主啊,我呼求你,你不應允我; 我站起來,你就定睛看我。
21 Umegeuka na kuwa mkali kwangu; kwa nguvu za mkono wako umenitesa.
你向我變心,待我殘忍, 又用大能追逼我,
22 Unaniinua katika upepo na kuufanya unikokote; unanirusha huku na kule katika dhoruba.
把我提在風中,使我駕風而行, 又使我消滅在烈風中。
23 Kwa maana najua ya kwamba utanipeleka mautini, nyumba ya hatima kwa viumbe vyote.
我知道要使我臨到死地, 到那為眾生所定的陰宅。
24 Lakini, je hakuna ainuaye mkono wake kuomba msaada aangukapo? Je hakuna aombaye msaada akiwa tabuni?
然而,人仆倒豈不伸手? 遇災難豈不求救呢?
25 Je sikulia kwa ajili yake aliyekuwa tabuni? Je sijahuzunika kwa ajili ya mwitaji?
人遭難,我豈不為他哭泣呢? 人窮乏,我豈不為他憂愁呢?
26 Nilipotazamia mema, ndipo yalipokuja mabaya; niliposubiri nuru, giza lilikuja badala yake.
我仰望得好處,災禍就到了; 我等待光明,黑暗便來了。
27 Moyo wangu umetaabika na hautulii; siku za mateso zimenipata.
我心裏煩擾不安, 困苦的日子臨到我身。
28 Nimekuwa na ngozi nyeusi lakini si kwa sababu ya jua; nasimama katika kusanyiko na kulilia msaada.
我沒有日光就哀哭行去; 我在會中站着求救。
29 Nimekuwa ndugu kwa mbwea, mshirika wa mbuni.
我與野狗為弟兄, 與鴕鳥為同伴。
30 Ngozi yangu imekuwa nyeusi na inapukutika; mifupa yangu imeunguzwa na joto.
我的皮膚黑而脫落; 我的骨頭因熱燒焦。
31 Kwa hiyo kinubi changu kimefunguliwa kwa nyimbo za maombolezo, zomari yangu kwa kuimba kwao waombolezao.
所以,我的琴音變為悲音; 我的簫聲變為哭聲。

< Ayubu 30 >