< Yeremia 5 >

1 Kimbieni mkapite katika mitaa ya Yerusalemu, Tafuteni katika viwanja vyake. Kama mtaweza kumpata hata mtu mmoja anayetenda kwa haki na kufanya kwa uaminifu, basi nitaisamehe Yerusalemu. 2 Hata kama wanasema, 'Kama BWANA aishivyo,' wanaapa uongo.” 3 BWANA, macho yako hayatazami uaminifu? Unawapiga watu, lakini hawasikii maumivu. Umewaangsmiza kabisa, lakini bado wanakataa kuwa waadilifu. Wanafanya nyuso zao kuwa ngumu kama mwamba. kwa kuwa wanakataa kutubu. 4 Kwa hiyo nilisema, “Hakika hawa ni watu masikini, Ni wapumbavu, Kwa kuwa hawazijui njia za BWANA, wala maagizo ya Mungu wao. 5 Nitaenda kwa watu wa muhimu na kutangaza ujumbe wa Mungu kwao, kwa kuwa angalau wanazijua njia za BWANA, maagizo ya Mungu wao. Lakini wote wanavunja nira yao pamoja; wote wanaivunja ile minyororo inayowafunga kwa ajili ya Mungu. 6 Kwa hiyo simba kutoka mwituni atawavamia. Mbweha kutoka Arabaha atawaangamiza. Chui ataivunja miji yao. Mtu yeyota anayeenda nje ya mji wake atavunjwavunjwa. Kwa kuwa maovu yao yameongezeka. Matendo yao ya uasi hayana ukomo. 7 Kwa nini niwasamehe hawa watu? Wana wenu wameniacha na wamefanya viapo na wale ambao si miungu. Niliwalisha vya kutosha, lakini wamefanya uasherati na kuchukua alama za nyumba ya uzinzi. 8 Walikuwa farasi wanaotafuta kupandwa. Walitembea huku na huku wakitafutwa kupandwa. Kila mwanamume alimkaribia mke wa jirani yake. 9 Kwa hiyo kwa nini nisiwaadhibu - asema BWANA - na kwa nini nisijilipizie kisasi juu ya taifa kama hili? 10 Nenda hadi kwenye kuta za shamba lake la mizabibu na zihariibuni. Lakini wao msiwaharibu kabisa. Ondoeni matawi kwa sababu hayatoki kwa BWANA. 11 Kwa sababu nyumba ya Yuda na Israeli wamenisaliti kabisa - asema BWANA - 12 na wamenikataa. Wanasema, ''Yeye si halisi. Maovu hayawezi kutupata, wala hatutaona upanga wala njaa. 13 Kwa kuwa manabii wamekuwa si kitu kama upepo na hakuna mtu mwiingine wa kunena ujumbe wa BWANA kwetu. Vitisho vyao na viwjie wao wenyewe.”' 14 Kwa hiyo BWANA, Mungu wa majeshi asema hivi, tazama nataka kuweka maneno yangu katika kinywa chako. Yatakuwa kama moto na watu hawa watakuwa kama kuni! Kwa kuwa utawaramba. 15 Tazama nataka kuleta taifa dhidi yenu kutoka mbali, enyi nyumba ya Israeli - asema BWANA - ni taifa linalodumu, taifa la kale! Ni taifa ambalo lugha yake hamuijui, wala hamtaelewa wasemacho. 16 Podo lao ni kaburi wazi. Wote ni wanajeshi. 17 Kwa hiyo mavuno yako yataliwa, wana wako na binti zako pia, na chakula chako. Watakula kondoo wako na ng'ombe wako, watakula matunda ya zabibu zako na ya mitiini. Wataiangusha chini miji yenu na boma zake ambazo mnazitumainia. 18 Lakini hata katika siku hizo - asema BWANA - sikusudii kuwaharibu kabisa. 19 Itatokea kwenu, ninyi Yuda na Israeli, mkisema, 'Kwa nini BWANA, Mungu wetu ametufanyia haya yote?' kwamba wewe Yeremia, utawaambia, 'Kama vile mlivyomwacha BWANA na kuabudu miungu mingine katika nchi yenu, vivyo hivyo mtawatumikia wageni katika nchi ambayo si yenu.' 20 Waambia haya watu wa nyumba ya Yakobo na yasikike katika Yuda. Waambie, 21 'Sikilizeni hili, eny watu wapumbavu! Sanamu hazina matakwa; zina masikio lakini haziwawezi kusikia. 22 Je, hamnihofu mimi - asema BWANA - au kutetemeka mbele ya uso wangu? Nimeweka mpaka wa mchanga kwenye bahari, ambao ni agizo la kudumu ambalo halibomoki - hata kama bahari ina kupwa na kujaa, bado hauwenzi kubomoka. Hata kama mawimbi yake yanaunguruma, hayawezi kuvuka. 23 Lakini hawa watu wana mioyo ya usumbufu. Hugeuka kuwa wapinzani na kuondoka. 24 Kwa kuwa hawasemi mioyoni mwao, “basi na tumche BWANA, Mungu wetu, yeye aletaye mvua za awali na mvua za vuli - kwa wakati wake, ambaye hutuzna majuma ya mavuno kwa ajili yetu.” 25 uovu wako umezuia haya yasitokee. Dhambi zako zimeyazuia mambo mema yasitokee. 26 Kwa watu waovu wamo kati ya watu wangu. Wanatazama kama mtu anayenyatia ili kukamata ndege; wanaweka mitego na kukamata watu; 27 Kama tundu la mtego lijaavyo ndege, nyumba zao zimejaa uongo. Kwa hiyo wanakua na kutajirika. 28 Wamenenepa; wanang'aa na kupendeza. Wamepitiliza hata mipika ya maovu. Wala hawajali sababu ya kuwepo kwa watu na wala uwepo wa yatima. Wanafanikiwa hata kama hawatoi hukumu ya haki kwa yatima. 29 Kwa nini nisiwadhibu kwa sababu ya haya - asema BWANA - sitajilipizia kisasi juu ya taifa la namna hii? 30 Jambo la ajabu na la kuchukiza limetokea katika nchi hii. 31 Mananbii wanatabiri kwa uongo, na makuhani wanatwala kwa msaada wa wa hao. Watu wangu wanapenda mambo ya hivyo, lakini mwisho kitatokea nini?

< Yeremia 5 >