< Wagalatia 5 >

1 Ni kwa sababu Kristo alitupa uhuru ili tuwe huru. Hivyo, simameni imara wala msinaswe tena katika kongwa la utumwa.
State, et nolite iterum iugo servitutis contineri.
2 Tazama, Mimi Paulo, ninawaambia kwamba ikiwa mtatahiriwa, Kristo hatawafaidia kwa njia yoyote ile.
Ecce ego Paulus dico vobis: quoniam si circumcidamini, Christus vobis nihil proderit.
3 Tena, namshuhudia kila mwanaume aliyetahiriwa kwamba anapaswa kuwajibika kwa sheria yote.
Testificor autem rursus omni homini circumcidenti se, quoniam debitor est universæ legis faciendæ.
4 Mmetengwa mbali na Kristo, wale wote “mnaohesabiwa haki” kwa sheria. Mmeanguka mbali na neema.
Evacuati estis a Christo, qui in lege iustificamini: a gratia excidistis.
5 Maana kwa njia ya Roho, kwa imani tunasubiri ujasiri wa haki.
Nos enim spiritu ex fide, spem iustitiæ expectamus.
6 Katika Kristo Yesu kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuna maana yoyote. Ni imani pekee inayofanya kazi kupitia upendo ndiyo humaanisha kitu.
Nam in Christo Iesu neque circumcisio aliquid valet, neque præputium: sed fides, quæ per charitatem operatur.
7 Mlikuwa mnapiga mbio vizuri. Nani aliwazuia kutokuitii kweli?
Currebatis bene: quis vos impedivit veritati non obedire?
8 Ushawishi wa kufanya hivyo hautoki kwake yeye anayewaita ninyi.
Persuasio hæc non est ex eo, qui vocat vos.
9 Chachu kidogo huathiri donge zima.
Modicum fermentum totam massam corrumpit.
10 Nina matumaini na ninyi katika Bwana kwamba hamtafikiri kwa njia nyingine yoyote. Yeyote yule atakayewapotosha atabeba hukumu yake yeye mwenyewe, yeyote yule.
Ego confido in vobis in Domino, quod nihil aliud sapietis: qui autem conturbat vos, portabit iudicium, quicumque est ille.
11 Ndugu, kama naendelea kutangaza tohara, kwanini bado ninateswa? Kwa suala hilo kile ambacho ni kizuizi cha msalaba kitaweza kuharibiwa.
Ego autem, fratres, si circumcisionem adhuc prædico: quid adhuc persecutionem patior? Ergo evacuatum est scandalum crucis.
12 Ni matakwa yangu kuwa wale wanaowaongoza vibaya watajihasi wenyewe.
Utinam et abscindantur qui vos conturbant.
13 Mungu amewaiteni ninyi, ndugu, kwenye uhuru. Ila msiutumie uhuru wenu kama fursa kwa mwili. Badala yake kwa upendo mhudumiane ninyi kwa ninyi.
Vos enim in libertatem vocati estis fratres: tantum ne libertatem in occasionem detis carnis, sed per charitatem Spiritus servite invicem.
14 Kwa kuwa sheria yote imekamilika katika amri moja; nayo ni “Ni lazima umpende jirani yako kama wewe mwenyewe.”
Omnis enim lex in uno sermone impletur: Diliges proximum tuum sicut teipsum.
15 Lakini kama mkiumana na kulana, jiangalieni kwamba msijiharibu ninyi kwa ninyi.
Quod si invicem mordetis, et comeditis: videte ne ab invicem consumamini.
16 Nasema, tembeeni kwa roho, na wala hamtazitimiza tamaa za mwili.
Dico autem: Spiritu ambulate, et desideria carnis non perficietis.
17 Kwa kuwa mwili una tamaa kubwa dhidi ya Roho, na Roho ina tamaa kubwa dhidi ya mwili. Hizi zinapingana kila moja na nyingine. Matokeo ni kwamba hamfanyi vitu mnavyotamani kuvifanya.
Caro enim concupiscit adversus spiritum: spiritus autem adversus carnem: hæc enim sibi invicem adversantur: ut non quæcumque vultis, illa faciatis.
18 Lakini kama Roho anawaongoza ninyi, hamko chini ya sheria.
Quod si Spiritu ducimini, non estis sub lege.
19 Sasa matendo ya mwili yanaonekana. Nayo ni uasherati, uchafu, ufisadi,
Manifesta sunt autem opera carnis: quæ sunt fornicatio, immunditia, impudicitia, luxuria,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, husuda, kuwaka hasira, ushindani, faraka, mgawanyiko wa madhehebu,
idolorum servitus, veneficia, inimicitiæ, contentiones, æmulationes, iræ, rixæ, dissensiones, sectæ,
21 wivu, ulevi, ulafi na mambo mengine kama haya. Nawaonya ninyi, kama nilivyowaonya mwanzoni, kwamba wale wanaofanya mambo kama hayo hawataurithi ufalme wa Mungu.
invidiæ, homicidia, ebrietates, comessationes, et his similia, quæ prædico vobis, sicut prædixi: quoniam qui talia agunt, regnum Dei non consequentur.
22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, ukarimu, utu wema, imani,
Fructus autem Spiritus est: charitas, gaudium, pax, patientia, benignitas, bonitas, longanimitas,
23 upole, na kiasi. Hakuna sheria dhidi ya mambo kama hayo.
mansuetudo, fides, modestia, continentia, castitas. Adversus huiusmodi non est lex.
24 Wale walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na shauku na tamaa zao mbaya.
Qui autem sunt Christi, carnem suam crucifixerunt cum vitiis, et concupiscentiis.
25 Kama tukiishi kwa Roho, pia tutembee kwa Roho.
Si Spiritu vivimus, Spiritu et ambulemus.
26 Tusiwe wa kujivuna, tusichokozane kila mmoja na mwenzake, wala tusioneane wivu.
Non efficiamur inanis gloriæ cupidi, invicem provocantes, invicem invidentes.

< Wagalatia 5 >