< 2 Wafalme 18 >

1 Ikawa katika mwaka wa tatu wa Hoshea mwana wa Ela, mfalme wa Israeli, Hezekia mwana wa Ahazi, mfalme wa Yuda akaanza kutawala.
ויהי בשנת שלש להושע בן אלה מלך ישראל מלך חזקיה בן אחז מלך יהודה
2 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala; alitawala miaka ishirini na tisa katika Yerusalemu. Jina la mama yake alikuwa anaitwa Abija; alikuwa binti wa Zekaria.
בן עשרים וחמש שנה היה במלכו ועשרים ותשע שנה מלך בירושלם ושם אמו אבי בת זכריה
3 Alifanya yaliyo mema usoni pa Yahwe, kufuata mfano wa yote ambayo Daudi, babu yake, aliyoyafanya.
ויעש הישר בעיני יהוה ככל אשר עשה דוד אביו
4 Alipaondoa mahali pa juu, akaiharibu nguzo ya jiwe, akaikata hiyo nguzo ya Ashera. Akavunja vipande vipande ile nyoka ambayo Musa aliyokuwa ameifanya, kwa sababu siku zile wana wa Israeli walikuwa wakichoma ubani katika hiyo; ilikuwa inaitwa “Nehushtani.”
הוא הסיר את הבמות ושבר את המצבת וכרת את האשרה וכתת נחש הנחשת אשר עשה משה כי עד הימים ההמה היו בני ישראל מקטרים לו ויקרא לו נחשתן
5 Hezekia alimwamini Yahwe, Mungu wa Israeli, hivyo basi baada ya yeye hapakuwa kama yeye miongoni mwa wafalme wote wa Yuda, wala miongoni mwa wafalme ambao walikuwa kabla yake.
ביהוה אלהי ישראל בטח ואחריו לא היה כמהו בכל מלכי יהודה ואשר היו לפניו
6 Aliambatana na Yahwe. Hakuacha kumfuata lakini alizifuata amri zake, ambazo Yahwe alimwamuru Musa.
וידבק ביהוה לא סר מאחריו וישמר מצותיו אשר צוה יהוה את משה
7 Hivyo Yahwe alikuwa na Hezekia, kila alipokwenda alifanikiwa. Akaasi dhidi ya mfalme wa Ashuru na hakumtumikia.
והיה יהוה עמו בכל אשר יצא ישכיל וימרד במלך אשור ולא עבדו
8 Akawashambulia Wafilisti hadi Gaza na mipaka inayoizunguka, kutoka mnara wa walinzi hadi hadi mji wenye ngome.
הוא הכה את פלשתים עד עזה ואת גבוליה ממגדל נוצרים עד עיר מבצר
9 Katika mwaka wa nne wa Mfalme Hezekia, ambao ulikuwa mwaka wa saba wa Hoshea mwana wa Ela mfalme wa Israeli, Shalmanesa mfalme wa Ashuru akapanda hadi Samaria na kuizunguka.
ויהי בשנה הרביעית למלך חזקיהו--היא השנה השביעית להושע בן אלה מלך ישראל עלה שלמנאסר מלך אשור על שמרון--ויצר עליה
10 Mwishoni mwa miaka mitatu wakaichukua, katika mwaka wa sita wa Hezekia, ambao ulikuwa mwaka wa tisa wa Hoshea mfalme wa Israeli; hivi ndivyo Samaria ilivyotekwa.
וילכדה מקצה שלש שנים בשנת שש לחזקיה היא שנת תשע להושע מלך ישראל נלכדה שמרון
11 Basi mfalme wa Ashuru akawachukua Israeli kwenda Ashuru na kuwaweka kwenye Hala, na katika mto Habori katika Gozani, na katika mji wa Wamedi.
ויגל מלך אשור את ישראל אשורה וינחם בחלח ובחבור נהר גוזן--וערי מדי
12 Alifanya hivi kwasababu hakutii sauti ya Yahwe Mungu wao, lakini walikiuka makubaliano ya agano lake, yote yale ambayo Musa yule mtumishi wa Yahwe aliwaamuru. Walikataa kuyasikiliza au kuyafanya.
על אשר לא שמעו בקול יהוה אלהיהם ויעברו את בריתו את כל אשר צוה משה עבד יהוה ולא שמעו ולא עשו
13 Kisha katika mwaka wa kumi na nne wa mfalme Hezekia, Senakerebu mfalme wa Ashuru akaishambulia miji yote yenye boma na kuwateka mateka.
ובארבע עשרה שנה למלך חזקיה עלה סנחריב מלך אשור על כל ערי יהודה הבצרות--ויתפשם
14 Basi Hezekia mfalme wa Yuda akatuma neno kwenda kwa mfalalme wa Yuda akatuma neno kwa mfalme wa Ashuru, ambaye alikuwa Lachishi, akisema, “Nimekuudhi. Nichukue. Popote utakaponiweka nitavumulia”. Mfalme wa Ashuru akamtaka Hezekia mfalme wa Yuda kulipa talanta mia tatu za fedha na talanta thelathini za dhahabu.
וישלח חזקיה מלך יהודה אל מלך אשור לכישה לאמר חטאתי שוב מעלי--את אשר תתן עלי אשא וישם מלך אשור על חזקיה מלך יהודה שלש מאות ככר כסף ושלשים ככר זהב
15 Hivyo Hezekia akampatia fedha zote ambazo zilikuwa zimepatikana kwenye nyumba ya Yahwe na kawenye hazina nyumba ya mfalme.
ויתן חזקיה את כל הכסף הנמצא בית יהוה ובאצרות בית המלך
16 Kisha Hezekia akaikata ile dhahabu kutoka kwenye milango ya hekalu la Yahwe na kutoka juu ya nguzo; akampatia dhahabu mfalme wa Ashuru.
בעת ההיא קצץ חזקיה את דלתות היכל יהוה ואת האמנות אשר צפה חזקיה מלך יהודה ויתנם למלך אשור
17 Lakini mfalme wa Ashuru akalihamasisha jeshi lake kubwa, akawatuma Tartani na Rabsarisi na amiri jeshi mkuu kutoka Lakishi kwenda kwa Hezekia huko Yerusalemu. Wakasafiri hadi kwenye mabarabara na kufika nje ya Yerusalemu. Wakakaribia karibu na mfereji wa birika la juu, kwenye barabara kuu ya shamba la dobi, na kusimama hapo.
וישלח מלך אשור את תרתן ואת רב סריס ואת רבשקה מן לכיש אל המלך חזקיהו בחיל כבד--ירושלם ויעלו ויבאו ירושלם ויעלו ויבאו ויעמדו בתעלת הברכה העליונה אשר במסלת שדה כבס
18 Wakati walipokuwa wamemwita Mfalme Hezekia, Eliakimu mwana wa Hilkia, ambaye alikuwa kiongozi wa nyumba ya mfalme na Shebna mwandishi, na Joa mwana wa Asafu, anayeandika kumbukumbu, wakatoka nje kwenda kuwalaki
ויקראו אל המלך ויצא אלהם אליקים בן חלקיהו אשר על הבית ושבנה הספר ויואח בן אסף המזכיר
19 Basi yule amiri jeshi mkuu akawaambia wamwambie Hezekia kile alichosema mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru, amesema: “Nini chanzo cha ujasiri wako?
ויאמר אליהם רבשקה אמרו נא אל חזקיהו כה אמר המלך הגדול מלך אשור מה הבטחון הזה אשר בטחת
20 Unaongea maneno yasiyo na maana, kusema lipo neno na nguvu ya vita. Sasa unamtumainia nani? Nani anakupa ujasiri wa kuasi dhidi yangu?
אמרת אך דבר שפתים--עצה וגבורה למלחמה עתה על מי בטחת כי מרדת בי
21 Tazama, unatumainia kutembelea fimbo ya mwanzi huu uliopondeka wa Misri, lakini kama mtu akiutegemea, utamchapa kwenye mkono wake na kuutoboa. Hicho ndicho Farao mfalme wa Misri kwa ymtu yeyote ambaye anayemtumainia.
עתה הנה בטחת לך על משענת הקנה הרצוץ הזה על מצרים אשר יסמך איש עליו ובא בכפו ונקבה כן פרעה מלך מצרים לכל הבטחים עליו
22 Lakini kama ukiniambia, 'Tunamwamini Yahwe Mungu watu; je si yeye ambaye mahali pa juu na madhabahu Hezekia amezichukua, na kumwambia Yuda na kwa Yerusalemu, 'Lazima uabudu mbele ya hii madhabahu katika Yerusalemu'?
וכי תאמרון אלי אל יהוה אלהינו בטחנו הלוא הוא אשר הסיר חזקיהו את במתיו ואת מזבחתיו ויאמר ליהודה ולירושלם לפני המזבח הזה תשתחוו בירושלם
23 Basi kwa hiyo, nataka kukufanyia ahadi nzuri kutoka kwa bwana wangu mfalme wa Ashuru. Nitakupatia farasi elfu mbili, kama unaweza kuwatafuta kuwaendesha kwa ajili yao.
ועתה התערב נא את אדני את מלך אשור ואתנה לך אלפים סוסים אם תוכל לתת לך רכבים עליהם
24 Wanawezaje kumpinga hata nahodha mmoja wa watumishi walio wadogo? Mmeweka tumaini lenu katika Misri kwa magari ya farasi na waendesha farasi!
ואיך תשיב את פני פחת אחד עבדי אדני--הקטנים ותבטח לך על מצרים לרכב ולפרשים
25 Je nimesafiri kwenda huko juu bila Yahwe kupapigania hapa mahali na kupaharibu? Yahwe ameniambia, 'Ishambulie hii nchi na uiharibu.”'
עתה המבלעדי יהוה עליתי על המקום הזה להשחתו יהוה אמר אלי עלה על הארץ הזאת והשחיתה
26 Kisha Elikana mwana wa Hilkia, na Shebna, na Joa wakamwambia amiri jeshi mkuu, “Tafadhali ongea na watumishi wako katika lugha ya Kiaramu, kwa kuwa tunaielewa. Usiongee nasi katika lugha ya Yuda katika masikio ya watu ambao wako ukutani.”
ויאמר אליקים בן חלקיהו ושבנה ויואח אל רבשקה דבר נא אל עבדיך ארמית--כי שמעים אנחנו ואל תדבר עמנו יהודית באזני העם אשר על החמה
27 Lakini yule amiri jeshi mkuu akawaambia, “Je bwana wangu amenituma kwa bwana wako na kuwachukua kuongea haya maneno? Je hajanituma kwa hawa watu ambao wameketi kwenye ukuta, ambao watakula kinyesi chao na kunywa mkojo wao wenyewe?”
ויאמר אליהם רבשקה העל אדניך ואליך שלחני אדני לדבר את הדברים האלה הלא על האנשים הישבים על החמה לאכל את חריהם (צואתם) ולשתות את שניהם (מימי רגליהם) עמכם
28 Kisha yule amiri jeshi mkuu akasimama na akapiga kelele kubwa kwa lugha ya Kiyahudi, akisema, “Sikilizeni neno la mfalme mkuu, mfale wa Ashuru.
ויעמד רבשקה ויקרא בקול גדול יהודית וידבר ויאמר שמעו דבר המלך הגדול מלך אשור
29 Mfalme asema, 'Msimwache Hezekia akawadanganya, kwa kuwa hataweza kuwaokoa kwenye nguvu yangu.
כה אמר המלך אל ישא לכם חזקיהו כי לא יוכל להציל אתכם מידו
30 Msimwache Hezekia akawatumainisha katika Yahwe, akisema, “Yahwe atatuokoa hakika, na huu mji hautawekwa kwenye mkono wa mfalme wa Ashuru.'”
ואל יבטח אתכם חזקיהו אל יהוה לאמר הצל יצילנו יהוה ולא תנתן את העיר הזאת ביד מלך אשור
31 Msikilize Hezekia, kwa kuwa hivi ndivyo mfalme wa Ashuru asemavyo: 'Fanyeni amani pamoja nami na njooni kwangu. Kisha kila mmoja wenu atakula kutoka kwenye mzabibu wake mwenyewe na kutoka kwenye mtini wake mwenyewe, na kunywa kutoka kwenye maji kwenye maji ya birika lake mwenyewe.
אל תשמעו אל חזקיהו כי כה אמר מלך אשור עשו אתי ברכה וצאו אלי ואכלו איש גפנו ואיש תאנתו ושתו איש מי ברו
32 Mtafanya hivyo hadi nitakapokuja na kuwachukua kwenda kwenye nchi kama nchi yenu, nchi ya nafaka na divai, nchi ya mkate na mashamba ya mizabibu, nchi ya miti ya mizaituni na asali, ili muweze kuishi na sio kufa.' Msimsikilize Hezekia wakati atakapojaribu kuwashawishi, akisema, 'Yahwe atatuokoa.'
עד באי ולקחתי אתכם אל ארץ כארצכם ארץ דגן ותירוש ארץ לחם וכרמים ארץ זית יצהר ודבש וחיו ולא תמתו ואל תשמעו אל חזקיהו כי יסית אתכם לאמר יהוה יצילנו
33 Je miungu yeyote ya watu inayewaokoa kutoka kwenye nchi ya mfalme wa Ashuru?
ההצל הצילו אלהי הגוים איש את ארצו מיד מלך אשור
34 Iko wapi miungu ya Hamathi na Arpadi? iko wapi miungu ya Sefarvaimu, Hena, na Iva? Je imeiokoa Samaria kutoka mkono wangu?
איה אלהי חמת וארפד איה אלהי ספרוים--הנע ועוה כי הצילו את שמרון מידי
35 Miongoni mwa miungu yote ya nchi, je kuna mungu ambaye ameiokoa nchi yake kutoka kwenye nguvu yangu? Inawezekanaje Yahwe akaiokoa Yerusalemu kutoka kwenye uwezo wangu?”
מי בכל אלהי הארצות אשר הצילו את ארצם מידי כי יציל יהוה את ירושלם מידי
36 Lakini watu wakabaki kimya na hawakujibu, kwa kuwa mfalme alikuwa ameamuru, “Msimjibu.”
והחרישו העם ולא ענו אתו דבר כי מצות המלך היא לאמר לא תענהו
37 Kisha Eliakimu mwana wa Hilkia, ambaye alikuwa juu ya nyumba ya mfalme; Shebna yule mwandishi; na Joa mwana wa Asafu, mtunza kumbukumbu, akaja kwa Hezekia pamoja na nguo zao zilizoraruliwa, na kumpatia taarifa ya maneno ya yule amiri mkuu.
ויבא אליקים בן חלקיה אשר על הבית ושבנא הספר ויואח בן אסף המזכיר אל חזקיהו--קרועי בגדים ויגדו לו דברי רבשקה

< 2 Wafalme 18 >