< 1 Samweli 20 >

1 Kisha Daudi akakimbia kutoka Nayothi huko Rama akaenda na kumwambia Yonathani, “Nimefanya nini? Uovu wangu ni upi? Dhambi yangu ni ipi kwa baba yako, inayofanya atafute kuutoa uhai wangu.”
Y David huyó de Naiot que es en Ramá, y vino delante de Jonatán, y dijo: ¿Qué he hecho yo? ¿Cuál es mi maldad, o cuál mi pecado contra tu padre, que él busca mi vida?
2 Yonathani akamwambia Daudi, “La hasha; hautakufa. Baba yangu hafanyi jambo kubwa wala dogo bila kunijulisha. Kwa nini inamlazimu baba yangu anifiche jambo hili? La, siyo hivyo?”
Y él le dijo: En ninguna manera; no morirás. He aquí que mi padre ninguna cosa hará, grande ni pequeña, que no me la descubra; ¿por qué, pues, me encubrirá mi padre este negocio? No será así.
3 Bado Daudi aliapa tena na akasema, “Baba yako anajua wazi kwamba nimepata kibali machoni pako. Pengine anasema, 'Asije Yonathani akajua jambo hili, labda atahuzunika.' Lakini kweli kama BWANA aishivyo, kama wewe uishivyo, kuna hatua moja tu kati yangu na mauti.”
Y David volvió a jurar, diciendo: Tu padre sabe claramente que yo he hallado gracia delante de tus ojos, y dirá en sí: No sepa esto Jonatán, para que no tenga pesar; y ciertamente, vive el SEÑOR y vive tu alma, que apenas hay un paso entre mí y la muerte.
4 Kisha Yonathani akamwambia Daudi, “Lolote utakalosema, nitakufanyia.”
Y Jonatán dijo a David: ¿Qué dice tu alma, y lo haré por ti?
5 Daudi akamwambia Yonathani, “Kesho ni siku ya mwezi mpya, na inanibidi kukaa na kula pamoja na mfalme. Lakini acha niende, ili niweze kujificha katika shamba hadi siku ya tatu jioni.
Y David respondió a Jonatán: He aquí que mañana será nueva luna, y yo acostumbro sentarme con el rey a comer; mas tú dejarás que me esconda en el campo hasta la tarde del tercer día.
6 Baba yako akinikosa kabisa, ndipo utasema, 'Daudi aliniomba kwa msisitizo ruhusa aondoke kwenda mjini kwake Bethlehemu; kwa sababu huko ni kipindi cha utoaji wa dhabihu ya mwaka kwa familia yao yote.'
Si tu padre hiciere mención de mí, dirás: Me rogó mucho que lo dejase ir presto a Belén su ciudad, porque todos los de su linaje tienen allá sacrificio aniversario.
7 Kama atasema kuwa ni vyema, 'basi mtumishi wako atakuwa na amani. Lakini kama atakasirika sana, ndipo utajua kwamba ameamua kunitendea uovu.
Si él dijere: Bien está, paz tendrá tu siervo; mas si se enojare, sabe que la malicia es en él consumada.
8 Kwa hiyo, umtendee wema mtumishi wako. Kwa maana umemweka mtumishi katika agano la BWANA pamoja na wewe. Lakini kama kuna dhambi ndani yangu, wewe mwenyewe uniuwe; maana kwa nini basi unipeleke kwa baba yako?”
Harás, pues, misericordia con tu siervo, ya que has traído tu siervo a alianza del SEÑOR contigo; y si maldad hay en mí mátame tú, que no hay necesidad de llevarme hasta tu padre.
9 Yonathani akasema, “La hasha! Ikiwa ninajua kwamba baba ameamua baya likupate, siwezi kukuambia?”
Y Jonatán le dijo: Nunca tal te suceda; antes bien, si yo entendiera ser consumada la malicia de mi padre, para venir sobre ti, ¿no había yo de descubrírtelo?
10 Ndipo Daudi akamwambia Yonathani, “Ni nani ataniambia ikiwa imetokea, baba yako akakujibu kwa ukali?”
Dijo entonces David a Jonatán: ¿Quién me dará aviso? O, ¿ qué si tu padre te respondiere ásperamente?
11 Yonathani akamwambia Daudi, “Njoo, hebu twende huko shambani.” Ndipo wote wakaondoka kwenda shambani.
Y Jonatán dijo a David: Ven, salgamos al campo. Y salieron ambos al campo.
12 Yonathani akamwambia Daudi, “Na BWANA, Mungu wa Israeli, awe shahidi. Kesho muda kama huu, nitakuwa nimemuuliza baba yangu, au siku ya tatu, tazama, ikiwa kutakuwa na jambo zuri upande wa Daudi; je, nisikutumie taarifa na kulidhihirisha kwako?
Entonces dijo Jonatán a David: Oh SEÑOR Dios de Israel, cuando habré yo preguntado a mi padre mañana a esta hora, o después de mañana, y si él me hablare bien de David, si entonces no enviare a ti, y te lo descubriere,
13 Na kama ikimpendeza baba yangu akufanyie madhara, Basi BWANA ayafanye hayo kwa Yonathani na kuzidi ikiwa sitakujulisha jambo na kukupeleka mbali, ili kwamba uende kwa amani. Na BWANA awe pamoja nawe, kama alivyokuwa na baba yangu.
el SEÑOR haga así a Jonatán, y esto añada. Mas si a mi padre pareciere bien hacerte mal, también te lo descubriré, y te enviaré, y te irás en paz; y sea el SEÑOR contigo, como fue con mi padre.
14 Kama bado nikiwa hai, hautanionesha uaminifu wa agano la BWANA, kwamba siwezi kufa?
Y si yo viviere, harás conmigo misericordia del SEÑOR; mas si fuere muerto,
15 Na usivunje kabisa uaminifu wako wa agano kati yako na nyumba yangu, hata wakati BWANA atakapowaodoa kila mmoja wa adui za Daudi kutoka uso wa dunia.”
no quitarás perpetuamente tu misericordia de mi casa. Cuando desarraigare el SEÑOR uno por uno los enemigos de David de la tierra, aun a Jonatán quite de su casa, si te faltare; y requiera el SEÑOR de la mano de los enemigos de David.
16 Basi Yonathani akafanya agano na nyumba ya Daudi na kusema, “Naye BWANA atawaondoa maadui wa Daudi.”
Así hizo Jonatán alianza con la casa de David.
17 Yonathani akamtaka Daudi aape tena kwa sababu ya upendo aliokuwa nao juu yake, kwa sababu alimpenda kama alivyopenda roho yake mwenyewe.
Y volvió Jonatán a jurar a David, porque le amaba, porque le amaba como a su propia alma.
18 Kisha Yonathani akamwambia Daudi, “Kesho ni siku ya mwezi mpya. Hautakuwapo, kwa sababu kiti chako kitakuwa wazi.
Le dijo luego Jonatán: Mañana es nueva luna, y tú serás echado de menos, porque tu asiento estará vacío.
19 Utakapokuwa umekaa huko siku tatu, uende upesi hadi mahala ulipojificha mara ya kwanza, wakati shughuli ikifanyika, na ukaye karibu jiwe Ezeli.
Estarás, pues, tres días, y luego descenderás, y vendrás al lugar donde estabas escondido el día de trabajo, y esperarás junto a la piedra de Ezel;
20 Nitatupa mishale mitatu pembeni mwa jiwe, kama vile ninalenga kitu fulani.
y yo tiraré tres saetas hacia aquel lado, como ejercitándome al blanco.
21 Kisha nitamtuma kijana wangu na kumwambia, 'Nenda utafute hiyo mishale.' Kama nitamwambia kijana hivi, 'Tazama, mishale iko upande huu wa kwako; kaichukue,” ndipo uje; maana hapo kutakuwa na usalama kwako na siyo madhara, kama BWANA aishivyo.
Y luego enviaré el criado, diciéndole: Ve, busca las saetas. Y si dijere al criado: He allí las saetas más acá de ti, tómalas; tú vendrás, porque paz tienes, y nada hay de mal, vive el SEÑOR.
22 “Lakini kama nikimwambia kijana hivi, 'Tazama, mishale iko mbele yako,' ndipo utakapokwenda zako, maana BWANA ametaka uende zako.
Mas si yo dijere al criado así: He allí las saetas más allá de ti; vete, porque el SEÑOR te ha enviado.
23 Kulingana na makubaliano ambayo mimi na wewe tumeongea, angalia, BWANA yupo kati yangu na wewe milele.'”
Y cuanto a las palabras que yo y tú hemos hablado, sea el SEÑOR entre mí y ti para siempre.
24 Kwa hiyo Daudi akajificha mle shambani. Pindi mwezi ulipoandama, mfalme aliketi chini ale chakula.
David, pues, se escondió en el campo, y venida que fue la nueva luna, se sentó el rey a comer pan.
25 Mfalme alikaa juu ya kiti chake, kama kawaida kwenye kiti karibu na ukuta. Yonathani alisimama wima, na Abneri alikaa ubavuni mwa Sauli. Lakini nafasi ya Daudi ilikuwa wazi.
Y el rey se sentó en su silla, como solía, en el asiento junto a la pared, y Jonatán se levantó, y se sentó Abner al lado de Saúl, y el lugar de David estaba vacío.
26 Hata hivyo Sauli hakusema kitu siku hiyo, kwa sababu alifikiri, “Kuna jambo limempata Daudi. Hayuko safi; hakika hayuko safi.”
Mas aquel día Saúl no dijo nada, porque se decía: Le habrá acontecido algo, por ventura no está limpio; no estará purificado.
27 Lakini siku ya pili, siku moja baada ya mwandamo wa mwezi, bado nafasi ya Daudi ilikuwa tupu. Ndipo Sauli akamuuliza Yonathani mwanaye, “Kwa nini mwana wa Yese hakuja kwenye chakula, jana na hata leo?”
El día siguiente, el segundo día de la nueva luna, aconteció también que el asiento de David estaba vacío. Y Saúl dijo a Jonatán su hijo: ¿Por qué no ha venido a comer el hijo de Isaí hoy ni ayer?
28 Yonathani akamjibu Sauli, “Daudi aliomba kwangu ruhusa kwa dhati ili aende Bethlehemu.
Y Jonatán respondió a Saúl: David me pidió encarecidamente le dejase ir hasta Belén.
29 Alisema, 'Tafadhali niruhusu niende. Maana familia yetu wanayo dhabihu huko mjini, na kaka yangu ameniagiza niwe huko. Basi kama nimepata kibali machoni pako, tafadhali niruhusu niende nikawaone kaka zangu.' Hakuja kwenye meza ya mfalme kwa sababu hii.”
Y dijo: Te ruego que me dejes ir, porque tenemos sacrificio los de nuestro linaje en la ciudad, y mi hermano mismo me lo ha mandado; por tanto, si he hallado gracia en tus ojos, haré una escapada ahora, y visitaré a mis hermanos. Por esto, pues, no ha venido a la mesa del rey.
30 Ndipo hasira ya Sauli iliwaka juu ya Yonathani, na akamwambia, “Wee mwana wa mwanamke mkaidi na muasi! Wadhani kwamba sijui kuwa umemchagua Mwana wa Yese kwa ajili ya aibu yako, na kwa aibu ya uchi wa mama yako?
Entonces Saúl se enardeció contra Jonatán, y le dijo: Hijo de la perversa y rebelde, ¿no sé yo que tú has elegido al hijo de Isaí para confusión tuya, y para confusión de la vergüenza de tu madre?
31 Kwa kuwa mwana wa Yese anaishi duniani, siyo wewe wala ufalme wako utakaoimarika. Sasa basi, tuma watu wamlete kwangu, kwa sababu inampasa kufa.”
Porque todo el tiempo que el hijo de Isaí viviere sobre la tierra, ni tú serás firme, ni tu reino. Envía pues ahora, y tráemelo, porque ha de morir.
32 Yonathani akamjibu Sauli baba yake, “Kwa sababu gani inampasa kuuwawa? Amefanya nini?”
Y Jonatán respondió a su padre Saúl, y le dijo: ¿Por qué morirá? ¿Qué ha hecho?
33 Ndipo Sauli akamtupia mkuki apate kumuua. Kwa hiyo Yonatani akatambua kwamba baba yake alinuia kumuua Daudi.
Entonces Saúl le arrojó una lanza para herirlo; de donde entendió Jonatán que su padre estaba determinado a matar a David.
34 Yonathani alitoka mezani akiwa na hasira kali bila kula chakula siku ya pili ya mwezi, kwa sababu alimhuzunikia Daudi, na kwa sababu baba yake amemwaibisha.
Y se levantó Jonatán de la mesa con exaltada ira, y no comió pan el segundo día de la nueva luna; porque tenía dolor a causa de David; y porque su padre le había afrentado.
35 Ikawa asubuhi, Yonathani akaenda huko shambani kama walivyoahidiana na Daudi, akiwa pamoja na kijana wake.
Al otro día de mañana, salió Jonatán al campo, al tiempo aplazado con David, y un criado pequeño con él.
36 Akamwambia yule kijana wake, “Kimbia utafute ile mishale niliyoitupa.” Na kijana alikimbia, akatupa mshale mwingine mbele yake.
Y dijo a su criado: Corre y busca las saetas que yo tirare. Y cuando el criado iba corriendo, él tiraba la saeta que pasara más allá de él.
37 Kijana alipofika katika eneo ambapo mshale ulitua, ule alioutuma Yonathani, akamwita tena kijana, na kusema, “Huo mshale hauko mbele yako?”
Y llegando el criado adonde estaba la saeta que Jonatán había tirado, Jonatán dio voces tras el muchacho, diciendo: ¿No está la saeta más allá de ti?
38 Kisha Yonathani akamwita yule kijana, “Upesi, harakisha, usikawie!” Hivyo kijana wa Yonathani akaikusanya mishale na kurudi kwa bwana wake.
Y volvió a gritar Jonatán tras el muchacho: Date prisa, aligera, no te pares. Y el criado de Jonatán cogió las saetas, y se vino a su señor.
39 Lakini huyo kijana hakujua lolote. Ni Yonathani na Daudi tu ndio walijua habari yenyewe.
Pero ninguna cosa entendió el criado; solamente Jonatán y David entendían el asunto.
40 Yonathani akampa kijana wake silaha na kumwambia, “Nenda, uzipeleke mjini.”
Luego dio Jonatán sus armas a su criado, y le dijo: Vete y llévalas a la ciudad.
41 Punde tu kijana alipoondoka, Daudi akasimama kutokea upande wa kusini, akiwa amelala kifudifudi, akainama mara tatu. Walibusiana wao kwa wao na wote wakalia kwa pamoja, Daudi akilia zaidi.
Y luego que el muchacho se hubo ido, se levantó David de la parte del mediodía, y se inclinó tres veces postrándose hasta la tierra; y besándose el uno al otro, lloraron el uno con el otro, aunque David lloró más.
42 Yonathani akamwambia Daudi, “Nenda kwa amani, kwa sababu wote tumeapa kwa jina la BWANA na tulisema, 'BWANA awe kati yangu na wewe, na awe kati ya uzao wangu na uzao wako, milele.'” Kisha Daudi alisimama na akaondoka, na Yonathani akarudi mjini.
Y Jonatán dijo a David: Vete en paz, que ambos hemos jurado por el nombre del SEÑOR, diciendo: El SEÑOR sea entre mí y ti, entre tu simiente y la mía, para siempre. Y él se levantó y se fue; y Jonatán se entró en la ciudad.

< 1 Samweli 20 >