< 1 Wakorintho 8 >

1 Sasa kuhusu vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu: tunajua ya kwamba “sisi sote tuna maarifa.” Maarifa huleta majivuno, bali upendo hujenga. 2 Ikiwa mtu yeyote anadhani kwamba anajua jambo fulani, mtu huyo bado hajui kama impasavyo kujua. 3 Lakini ikiwa mmoja wapo akimpenda Mungu, mtu huyo anajulikana naye. 4 Basi kuhusu kula vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu: twajua kuwa “sanamu si kitu katika dunia hii,” na ya kuwa hakuna Mungu ila mmoja tu.” 5 Kwa maana kuna wengi waitwao miungu ikiwa ni mbinguni au duniani, kama vile walivyo “miungu na mabwana wengi.” 6 “Ijapokuwa kwetu kuna Mungu mmoja tu ambaye ni Baba, vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake, na Bwana mmoja Yesu Kristo, ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo, na kwa yeye sisi tupo.” 7 Hata hivyo, ujuzi huu haupo ndani ya kila mmoja. Badala yake, wengine walishiriki ibada za sanamu hapo zamani, na hata sasa wanakula vyakula hivi kana kwamba ni kitu kilichotolewa sadaka kwa sanamu. Dhamiri zao zimepotoshwa kwa kuwa ni dhaifu. 8 Lakini chakula hakitatuthibitisha sisi kwa Mungu. Sisi sio wabaya sana kama tusipo kula, wala wema sana ikiwa tutakula. 9 Lakini iweni makini ya kwamba uhuru wenu usiwe sababu ya kumkwaza aliye dhaifu katika imani. 10 Hebu fikiri kwamba mtu amekuona, wewe uliye na ujuzi, unakula chakula katika hekalu la sanamu. Dhamiri yake mtu huyo haitathibitika hata yeye naye ale vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu? 11 Kwa hiyo kwa sababu ya ufahamu wako wa ukweli juu ya asili ya sanamu, kaka au dada yako aliye dhaifu, ambaye pia Kristo alikufa kwa ajili yake, anaangamizwa. 12 Hivyo, unapofanya dhambi dhidi ya kaka na dada zako na kuzijeruhi dhamiri zao zilizo dhaifu, mnatenda dhambi dhidi ya Kristo. 13 Kwa hiyo, ikiwa chakula kinasababisha kumkwaza kaka au dada, sitakula nyama kamwe, ili nisimsababishe kaka au dada yangu kuanguka. (aiōn g165)

< 1 Wakorintho 8 >