< Zaburi 99 >

1 Bwana anatawala, mataifa na yatetemeke; anakalia kiti cha enzi katikati ya makerubi, dunia na itikisike. 2 Bwana ni mkuu katika Sayuni; ametukuzwa juu ya mataifa yote. 3 Wanalisifu jina lako ambalo ni kuu na la kuogopwa: yeye ni mtakatifu! 4 Mfalme ni mwenye nguvu na hupenda haki, wewe umethibitisha adili; katika Yakobo umefanya yaliyo haki na sawa. 5 Mtukuzeni Bwana Mungu wetu, na mkaabudu katika mahali pa kuwekea miguu yake; yeye ni mtakatifu. 6 Mose na Aroni walikuwa miongoni mwa makuhani wake, Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake; walimwita Bwana, naye aliwajibu. 7 Alizungumza nao kutoka nguzo ya wingu; walizishika sheria zake na amri alizowapa. 8 Ee Bwana, wetu, ndiwe uliyewajibu, kwa Israeli ulikuwa Mungu mwenye kusamehe, ingawa uliadhibu matendo yao mabaya. 9 Mtukuzeni Bwana Mungu wetu, mwabuduni kwenye mlima wake mtakatifu, kwa maana Bwana Mungu wetu ni mtakatifu.

< Zaburi 99 >