< Zaburi 87 >

1 Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo. Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu; 2 Bwana anayapenda malango ya Sayuni kuliko makao yote ya Yakobo. 3 Mambo matukufu yanasemwa juu yako, ee mji wa Mungu: 4 “Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu na Babeli miongoni mwa wale wanaonikubali mimi: Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi, nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’” 5 Kuhusu Sayuni itasemwa hivi, “Huyu na yule walizaliwa humo, naye Aliye Juu Sana mwenyewe atamwimarisha.” 6 Bwana ataandika katika orodha ya mataifa: “Huyu alizaliwa Sayuni.” 7 Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba, “Chemchemi zangu zote ziko kwako.”

< Zaburi 87 >