< Zaburi 74 >

1 Utenzi wa Asafu. Ee Mungu, mbona umetukataa milele? Mbona hasira yako inatoka moshi juu ya kondoo wa malisho yako?
משכיל לאסף למה אלהים זנחת לנצח יעשן אפך בצאן מרעיתך
2 Kumbuka watu uliowanunua zamani, kabila la urithi wako, ambao uliwakomboa: Mlima Sayuni, ambamo uliishi.
זכר עדתך קנית קדם-- גאלת שבט נחלתך הר-ציון זה שכנת בו
3 Geuza hatua zako kuelekea magofu haya ya kudumu, uharibifu wote huu ambao adui ameuleta pale patakatifu.
הרימה פעמיך למשאות נצח כל-הרע אויב בקדש
4 Adui zako wamenguruma pale ulipokutana nasi, wanaweka bendera zao kama alama.
שאגו צרריך בקרב מועדך שמו אותתם אתות
5 Walifanya kama watu wanaotumia mashoka kukata kichaka cha miti.
יודע כמביא למעלה בסבך-עץ קרדמות
6 Walivunjavunja milango yote iliyonakshiwa kwa mashoka na vishoka vyao.
ועת (ועתה) פתוחיה יחד-- בכשיל וכילפות יהלמון
7 Waliteketeza kabisa mahali pako patakatifu, wakayanajisi makao ya Jina lako.
שלחו באש מקדשך לארץ חללו משכן-שמך
8 Walisema mioyoni mwao, “Tutawaponda kabisa!” Walichoma kila mahali ambapo Mungu aliabudiwa katika nchi.
אמרו בלבם נינם יחד שרפו כל-מועדי-אל בארץ
9 Hatukupewa ishara za miujiza; hakuna manabii waliobaki, hakuna yeyote kati yetu ajuaye hali hii itachukua muda gani.
אותתינו לא ראינו אין-עוד נביא ולא-אתנו ידע עד-מה
10 Ee Mungu, mtesi atakudhihaki mpaka lini? Je, adui watalitukana jina lako milele?
עד-מתי אלהים יחרף צר ינאץ אויב שמך לנצח
11 Kwa nini unazuia mkono wako, mkono wako wa kuume? Uutoe kutoka makunjo ya vazi lako na uwaangamize!
למה תשיב ידך וימינך מקרב חוקך (חיקך) כלה
12 Lakini wewe, Ee Mungu, ni mfalme wangu tangu zamani, unaleta wokovu duniani.
ואלהים מלכי מקדם פעל ישועות בקרב הארץ
13 Ni wewe uliyeigawanya bahari kwa uweza wako; ulivunja vichwa vya wanyama wakubwa wa kutisha katika maji.
אתה פוררת בעזך ים שברת ראשי תנינים על-המים
14 Ni wewe uliyeponda vichwa vya Lewiathani nawe ukamtoa kama chakula kwa viumbe vya jangwani.
אתה רצצת ראשי לויתן תתננו מאכל לעם לציים
15 Ni wewe uliyefungua chemchemi na vijito, ulikausha mito ambayo ilikuwa ikitiririka daima.
אתה בקעת מעין ונחל אתה הובשת נהרות איתן
16 Mchana ni wako, nao usiku ni wako pia, uliziweka jua na mwezi.
לך יום אף-לך לילה אתה הכינות מאור ושמש
17 Ni wewe uliyeiweka mipaka yote ya dunia, ulifanya kiangazi na masika.
אתה הצבת כל-גבולות ארץ קיץ וחרף אתה יצרתם
18 Ee Bwana, kumbuka jinsi mtesi alivyokudhihaki, jinsi watu wapumbavu walivyolitukana jina lako.
זכר-זאת--אויב חרף יהוה ועם נבל נאצו שמך
19 Usiukabidhi uhai wa njiwa wako kwa wanyama wakali wa mwitu; usisahau kabisa uhai wa watu wako wanaoteseka milele.
אל-תתן לחית נפש תורך חית ענייך אל-תשכח לנצח
20 Likumbuke agano lako, maana mara kwa mara mambo ya jeuri yamejaa katika sehemu za giza nchini.
הבט לברית כי מלאו מחשכי-ארץ נאות חמס
21 Usiruhusu walioonewa warudi nyuma kwa aibu; maskini na wahitaji hebu walisifu jina lako.
אל-ישב דך נכלם עני ואביון יהללו שמך
22 Inuka, Ee Mungu, ujitetee; kumbuka jinsi wapumbavu wanavyokudhihaki mchana kutwa.
קומה אלהים ריבה ריבך זכר חרפתך מני-נבל כל-היום
23 Usipuuze makelele ya watesi wako, ghasia za adui zako, zinazoinuka mfululizo.
אל-תשכח קול צרריך שאון קמיך עלה תמיד

< Zaburi 74 >