< Zaburi 60 >

1 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Shushani Eduthi.” Utenzi wa Daudi wa kufundisha. Wakati alipopigana na Waaramu kutoka Aramu-Naharaimu na Aramu-Soba, naye Yoabu akarudi nyuma na kuwaua Waedomu 12,000 katika Bonde la Chumvi. Ee Mungu, umetukataa na kutokea ghafula juu yetu, umekasirika: sasa turejeshe upya!
To the chief Musician upon Shushan-eduth, Michtam of David, to teach; when he strove with Aram-naharaim and with Aram-zobah, when Joab returned, and smote of Edom in the valley of salt twelve thousand. O God, thou hast cast us off, thou hast scattered us, thou hast been displeased; O turn thyself to us again.
2 Umetetemesha nchi na kuipasua; uiponye mavunjiko yake, kwa maana inatetemeka.
Thou hast made the earth to tremble; thou hast broken it: heal its breaches; for it shaketh.
3 Umewaonyesha watu wako nyakati za kukata tamaa; umetunywesha mvinyo unaotuyumbisha.
Thou hast shown thy people hard things: thou hast made us to drink the wine of astonishment.
4 Kwa wale wanaokucha wewe, umewainulia bendera, ili iweze kutwekwa dhidi ya upinde.
Thou hast given a banner to them that fear thee, that it may be displayed because of the truth. (Selah)
5 Tuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume, ili wale uwapendao wapate kuokolewa.
That thy beloved may be delivered; save [with] thy right hand, and hear me.
6 Mungu amenena kutoka patakatifu pake: “Nitaigawa Shekemu kwa ushindi na kulipima Bonde la Sukothi.
God hath spoken in his holiness; I will rejoice, I will divide Shechem, and measure out the valley of Succoth.
7 Gileadi ni yangu na Manase ni yangu; Efraimu ni kofia yangu ya chuma, nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala.
Gilead [is] mine, and Manasseh [is] mine; Ephraim also [is] the strength of my head; Judah [is] my lawgiver;
8 Moabu ni sinia langu la kunawia, juu ya Edomu natupa kiatu changu; nashangilia kwa kushindwa kwa Ufilisti.”
Moab [is] my washpot; over Edom will I cast out my shoe: Philistia, triumph thou because of me.
9 Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome? Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu?
Who will bring me [into] the strong city? who will lead me into Edom?
10 Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi, na hutoki tena na majeshi yetu?
[Wilt] thou not, O God, [who] hadst cast us off? and [thou], O God, [who] didst not go out with our armies?
11 Tuletee msaada dhidi ya adui, kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu.
Give us help from trouble: for vain [is] the help of man.
12 Kwa msaada wa Mungu tutapata ushindi, naye atawaponda adui zetu.
Through God we shall do valiantly: for he will tread down our enemies.

< Zaburi 60 >