< Zaburi 47 >

1 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. Pigeni makofi, enyi mataifa yote, mpigieni Mungu kelele za shangwe! 2 Jinsi gani alivyo wa kutisha, Bwana Aliye Juu Sana, Mfalme mkuu juu ya dunia yote! 3 Ametiisha mataifa chini yetu watu wengi chini ya miguu yetu. 4 Alituchagulia urithi wetu, fahari ya Yakobo, aliyempenda. 5 Mungu amepaa kwa kelele za shangwe, Bwana kwa sauti za tarumbeta. 6 Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa, mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa. 7 Kwa kuwa Mungu ni mfalme wa dunia yote, mwimbieni zaburi za sifa. 8 Mungu anatawala juu ya mataifa, Mungu ameketi juu ya kiti chake cha enzi kitakatifu. 9 Wakuu wa mataifa wanakusanyika kama watu wa Mungu wa Abrahamu, kwa kuwa wafalme wa dunia ni mali ya Mungu; yeye ametukuka sana.

< Zaburi 47 >