< Zaburi 128 >

1 Wimbo wa kwenda juu. Heri ni wale wote wamchao Bwana, waendao katika njia zake. 2 Utakula matunda ya kazi yako; baraka na mafanikio vitakuwa vyako. 3 Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao ndani ya nyumba yako; wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni kuizunguka meza yako. 4 Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa mtu amchaye Bwana. 5 Bwana na akubariki kutoka Sayuni siku zote za maisha yako, na uone mafanikio ya Yerusalemu, 6 nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako. Amani iwe juu ya Israeli.

< Zaburi 128 >