< Zaburi 126 >

1 Wimbo wa kwenda juu. Bwana alipowarejeza mateka Sayuni, tulikuwa kama watu walioota ndoto. 2 Vinywa vyetu vilijaa kicheko, ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe. Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa, “Bwana amewatendea mambo makuu.” 3 Bwana ametutendea mambo makuu, nasi tumejaa furaha. 4 Ee Bwana, turejeshee watu wetu waliotekwa, kama vijito katika Negebu. 5 Wapandao kwa machozi watavuna kwa nyimbo za shangwe. 6 Yeye azichukuaye mbegu zake kwenda kupanda, huku akilia, atarudi kwa nyimbo za shangwe, akichukua miganda ya mavuno yake.

< Zaburi 126 >