< Zaburi 124 >

1 Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. Kama Bwana asingalikuwa upande wetu; Israeli na aseme sasa: 2 kama Bwana asingalikuwa upande wetu, wakati watu walipotushambulia, 3 wakati hasira yao ilipowaka dhidi yetu, wangalitumeza tungali hai, 4 mafuriko yangalitugharikisha, maji mengi yangalitufunika, 5 maji yaendayo kasi yangalituchukua. 6 Bwana asifiwe, yeye ambaye hakuruhusu turaruliwe kwa meno yao. 7 Tumeponyoka kama ndege kutoka mtego wa mwindaji; mtego umevunjika, nasi tukaokoka. 8 Msaada wetu ni katika jina la Bwana, Muumba wa mbingu na dunia.

< Zaburi 124 >