< Zaburi 114 >

1 Wakati Israeli walipotoka Misri, nyumba ya Yakobo kutoka kwa watu wa lugha ngeni, 2 Yuda alifanywa makao matakatifu ya Mungu, Israeli akawa milki yake. 3 Bahari ilitazama ikakimbia, Yordani ulirudi nyuma, 4 milima ilirukaruka kama kondoo dume, vilima kama wana-kondoo. 5 Ee bahari, ni nini kilichokufanya ukakimbia, nawe, ee Yordani, ukarudi nyuma, 6 enyi milima mkarukaruka kama kondoo dume, enyi vilima, kama wana-kondoo? 7 Ee dunia, tetemeka mbele za Bwana, mbele za Mungu wa Yakobo, 8 aliyegeuza mwamba kuwa dimbwi la maji, mwamba mgumu kuwa chemchemi za maji.

< Zaburi 114 >