< Zaburi 110 >

1 Zaburi ya Daudi. Bwana amwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume, mpaka nitakapowafanya adui zako kuwa mahali pa kuweka miguu yako.” 2 Bwana ataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni; utatawala katikati ya adui zako. 3 Askari wako watajitolea kwa hiari katika siku yako ya vita. Ukiwa umevikwa fahari takatifu, kutoka tumbo la mapambazuko utapokea umande wa ujana wako. 4 Bwana ameapa, naye hatabadilisha mawazo yake: “Wewe ni kuhani milele, kwa mfano wa Melkizedeki.” 5 Bwana yuko mkono wako wa kuume, atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake. 6 Atawahukumu mataifa, akilundika mizoga na kuwaponda watawala wa dunia nzima. 7 Atakunywa maji katika kijito kando ya njia, kwa hiyo atainua kichwa chake juu.

< Zaburi 110 >