< Mika 5 >

1 Panga majeshi yako, ee mji wa majeshi, kwa kuwa kuzingirwa kumepangwa dhidi yetu. Watampiga mtawala wa Israeli shavuni kwa fimbo.
Now you shall gather yourself in troops, daughter of troops. He has laid siege against us. They will strike the judge of Israel with a rod on the cheek.
2 “Lakini wewe, Bethlehemu Efrathi, ingawa u mdogo miongoni mwa koo za Yuda, kutoka kwako atatokea kwa ajili yangu yeye atakayekuwa mtawala katika Israeli, ambaye asili yake ni kutoka zamani, kutoka milele.”
But you, Bethlehem Ephrathah, being small among the clans of Judah, out of you one will come forth to me that is to be ruler in Israel; whose goings forth are from of old, from everlasting.
3 Kwa hiyo Israeli utaachwa mpaka wakati mwanamke aliye na utungu atakapozaa na ndugu zake wengine warudi kujiunga na Waisraeli.
Therefore he will abandon them until the time that she who is in labor gives birth. Then the rest of his brothers will return to the children of Israel.
4 Atasimama na kulichunga kundi lake katika nguvu ya Bwana, katika utukufu wa jina la Bwana Mungu wake. Nao wataishi kwa usalama, kwa kuwa wakati huo ukuu wake utaenea hadi miisho ya dunia.
He shall stand, and shall shepherd in the strength of Jehovah, in the majesty of the name of Jehovah his God: and they will live, for then he will be great to the farthest parts of the earth.
5 Naye atakuwa amani yao. Wakati Mwashuru atakapovamia nchi yetu na kupita katika ngome zetu, tutawainua wachungaji saba dhidi yake, hata viongozi wanane wa watu.
He will be our peace when Assyria invades our land, and when he marches through our fortresses, then we will raise against him seven shepherds, and eight leaders of men.
6 Wataitawala nchi ya Ashuru kwa upanga, nchi ya Nimrodi kwa upanga. Atatuokoa kutoka kwa Mwashuru atakapoivamia nchi yetu na kuingia katika mipaka yetu.
They will rule the land of Assyria with the sword, and the land of Nimrod with the drawn sword. He will deliver us from the Assyrian, when he invades our land, and when he marches within our border.
7 Mabaki ya Yakobo yatakuwa katikati ya mataifa mengi kama umande kutoka kwa Bwana, kama manyunyu juu ya majani, ambayo hayamngoji mtu wala kukawia kwa mwanadamu.
The remnant of Jacob will be in the midst of many peoples, like dew from Jehovah, like showers on the grass, that do not wait for man, nor wait for the sons of men.
8 Mabaki ya Yakobo yatakuwa miongoni mwa mataifa, katikati ya mataifa mengi, kama simba miongoni mwa wanyama wa msituni, kama mwana simba miongoni mwa makundi ya kondoo, ambaye anaumiza vibaya na kuwararua kila anapopita katikati yao, wala hakuna awezaye kuokoa.
The remnant of Jacob will be among the nations, in the midst of many peoples, like a lion among the animals of the forest, like a young lion among the flocks of sheep; who, if he goes through, treads down and tears in pieces, and there is no one to deliver.
9 Mkono wako utainuliwa juu kwa ushindi juu ya watesi wako, nao adui zako wote wataangamizwa.
Let your hand be lifted up above your adversaries, and let all of your enemies be cut off.
10 “Katika siku ile,” asema Bwana, “nitaangamiza farasi zenu katikati yenu na kubomoa magari yenu ya vita.
"It will happen in that day," says Jehovah, "That I will cut off your horses out of the midst of you, and will destroy your chariots.
11 Nitaiangamiza miji ya nchi yenu na kuziangusha chini ngome zenu zote.
I will cut off the cities of your land, and will tear down all your strongholds.
12 Nitaangamiza uchawi wenu na hamtapiga tena ramli.
I will destroy witchcraft from your hand; and you shall have no soothsayers.
13 Nitaangamiza vinyago vyenu vya kuchonga na mawe yenu ya ibada yatoke katikati yenu; hamtasujudia tena kazi ya mikono yenu.
I will cut off your engraved images and your pillars out of your midst; and you shall no more worship the work of your hands.
14 Nitangʼoa nguzo za Ashera katikati yenu na kubomoa miji yenu.
I will uproot your Asherim out of your midst; and I will destroy your cities.
15 Nitalipiza kisasi kwa hasira na ghadhabu juu ya mataifa ambayo hayajanitii.”
I will execute vengeance in anger, and wrath on the nations that did not listen."

< Mika 5 >