< Mambo ya Walawi 18 >

1 Bwana akamwambia Mose,
וידבר יהוה אל משה לאמר
2 “Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.
דבר אל בני ישראל ואמרת אלהם אני יהוה אלהיכם
3 Msifanye kama wafanyavyo huko Misri, mahali mlipokuwa mnaishi, wala msifanye kama wanavyofanya katika nchi ya Kanaani, mahali ninapowapeleka. Msifuate matendo yao.
כמעשה ארץ מצרים אשר ישבתם בה לא תעשו וכמעשה ארץ כנען אשר אני מביא אתכם שמה לא תעשו ובחקתיהם לא תלכו
4 Ni lazima mzitii sheria zangu, na mwe waangalifu kuzifuata amri zangu. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.
את משפטי תעשו ואת חקתי תשמרו ללכת בהם אני יהוה אלהיכם
5 Zishikeni amri zangu na sheria zangu, kwa maana mtu anayezitii ataishi kwa hizo. Mimi ndimi Bwana.
ושמרתם את חקתי ואת משפטי אשר יעשה אתם האדם וחי בהם אני יהוה
6 “‘Hakuna mtu awaye yote atakayemsogelea ndugu wa karibu ili kukutana naye kimwili. Mimi ndimi Bwana.
איש איש אל כל שאר בשרו לא תקרבו לגלות ערוה אני יהוה
7 “‘Usimvunjie heshima baba yako kwa kukutana kimwili na mama yako. Yeye ni mama yako; usiwe na mahusiano kama hayo naye.
ערות אביך וערות אמך לא תגלה אמך הוא לא תגלה ערותה
8 “‘Usikutane kimwili na mke wa baba yako; hiyo itamvunjia heshima baba yako.
ערות אשת אביך לא תגלה ערות אביך הוא
9 “‘Usikutane kimwili na dada yako, wala binti wa baba yako, au binti wa mama yako, awe amezaliwa katika nyumba hiyo au mahali pengine.
ערות אחותך בת אביך או בת אמך מולדת בית או מולדת חוץ--לא תגלה ערותן
10 “‘Usikutane kimwili na binti wa mwanao ama binti wa binti yako; utajivunjia heshima.
ערות בת בנך או בת בתך לא תגלה ערותן כי ערותך הנה
11 “‘Usikutane kimwili na binti wa mke wa baba yako, aliyezaliwa na baba yako; huyo ni dada yako.
ערות בת אשת אביך מולדת אביך אחותך הוא--לא תגלה ערותה
12 “‘Usikutane kimwili na dada wa baba yako; ni ndugu wa karibu wa baba yako.
ערות אחות אביך לא תגלה שאר אביך הוא
13 “‘Usikutane kimwili na dada wa mama yako, kwa sababu ni ndugu wa mama yako wa karibu.
ערות אחות אמך לא תגלה כי שאר אמך הוא
14 “‘Usimvunjie heshima ndugu wa baba yako, kwa kukutana kimwili na mke wake; yeye ni shangazi yako.
ערות אחי אביך לא תגלה אל אשתו לא תקרב דדתך הוא
15 “‘Usikutane kimwili na mkwe wako, yeye ni mke wa mwanao; usiwe na mahusiano kama hayo naye.
ערות כלתך לא תגלה אשת בנך הוא לא תגלה ערותה
16 “‘Usikutane kimwili na mke wa kaka yako; utamvunjia heshima kaka yako.
ערות אשת אחיך לא תגלה ערות אחיך הוא
17 “‘Usikutane kimwili na mwanamke kisha na binti yake. Usikutane kimwili na binti wa mwanawe au binti wa binti yake; hao ni ndugu zake wa karibu. Huo ni uovu.
ערות אשה ובתה לא תגלה את בת בנה ואת בת בתה לא תקח לגלות ערותה--שארה הנה זמה הוא
18 “‘Usimchukue dada wa mke wako kuwa mke mwenza, na kukutana naye kimwili wakati bado mke wako anaishi.
ואשה אל אחתה לא תקח לצרר לגלות ערותה עליה--בחייה
19 “‘Usimsogelee mwanamke ili kukutana naye kimwili wakati wa unajisi wa siku zake za mwezi.
ואל אשה בנדת טמאתה--לא תקרב לגלות ערותה
20 “‘Usikutane kimwili na mke wa jirani yako na kujitia naye unajisi.
ואל אשת עמיתך--לא תתן שכבתך לזרע לטמאה בה
21 “‘Usimtoe mtoto wako yeyote awe kafara kwa mungu Moleki, kwani hutalinajisi kamwe jina la Mungu wako. Mimi ndimi Bwana.
ומזרעך לא תתן להעביר למלך ולא תחלל את שם אלהיך אני יהוה
22 “‘Usikutane kimwili na mwanaume kama mtu akutanaye na mwanamke; hilo ni chukizo.
ואת זכר--לא תשכב משכבי אשה תועבה הוא
23 “‘Usikutane kimwili na mnyama na kujitia unajisi kwake. Mwanamke asijipeleke kwa mnyama ili kukutana naye kimwili; huo ni upotovu.
ובכל בהמה לא תתן שכבתך לטמאה בה ואשה לא תעמד לפני בהמה לרבעה--תבל הוא
24 “‘Msijitie unajisi kwa njia yoyote katika hizi, kwa sababu hivi ndivyo mataifa nitakayoyafukuza mbele yenu yalivyojitia unajisi.
אל תטמאו בכל אלה כי בכל אלה נטמאו הגוים אשר אני משלח מפניכם
25 Hata nchi ilitiwa unajisi, hivyo nikaiadhibu kwa dhambi zake, nayo nchi ikawatapika wakazi wake.
ותטמא הארץ ואפקד עונה עליה ותקא הארץ את ישביה
26 Lakini ni lazima uzitunze amri zangu na sheria zangu. Mzawa na wageni waishio miongoni mwenu kamwe wasifanye mambo yoyote ya machukizo haya,
ושמרתם אתם את חקתי ואת משפטי ולא תעשו מכל התועבת האלה האזרח והגר הגר בתוככם
27 kwa kuwa mambo haya yote yalifanywa na watu walioishi katika nchi hii kabla yenu, na nchi ikawa najisi.
כי את כל התועבת האל עשו אנשי הארץ אשר לפניכם ותטמא הארץ
28 Kama mkiinajisi nchi, itawatapika kama ilivyowatapika mataifa yaliyowatangulia.
ולא תקיא הארץ אתכם בטמאכם אתה כאשר קאה את הגוי אשר לפניכם
29 “‘Kila mtu atakayefanya mojawapo ya machukizo haya, watu hao ni lazima wakatiliwe mbali na watu wao.
כי כל אשר יעשה מכל התועבת האלה--ונכרתו הנפשות העשת מקרב עמם
30 Shikeni maagizo yangu, wala msifuate desturi za machukizo yoyote yaliyofanywa kabla hamjafika katika nchi hii, na kujitia unajisi kwa hayo. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.’”
ושמרתם את משמרתי לבלתי עשות מחקות התועבת אשר נעשו לפניכם ולא תטמאו בהם אני יהוה אלהיכם

< Mambo ya Walawi 18 >