< Mambo ya Walawi 15 >

1 Bwana akawaambia Mose na Aroni,
And the LORD spoke to Moses and to Aaron, saying,
2 “Semeni na Waisraeli mwaambie: ‘Wakati mtu yeyote anapotokwa na usaha mwilini, usaha huo ni najisi.
Speak to the children of Israel, and say to them, When any man hath a running issue out of his flesh, [because of] his issue he [is] unclean.
3 Iwe unaendelea kutiririka kutoka mwilini mwake au umeziba, utamfanya kuwa najisi. Hivi ndivyo usaha wake utakavyomletea unajisi:
And this shall be his uncleanness in his issue: whether his flesh shall run with his issue, or his flesh be stopped from his issue, it [is] his uncleanness.
4 “‘Kitanda chochote atakacholalia mtu mwenye kutokwa na usaha kitakuwa najisi, na chochote atakachokalia kitakuwa najisi.
Every bed on which he lieth that hath the issue, is unclean: and every thing on which he sitteth, shall be unclean.
5 Yeyote atakayegusa kitanda chake ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.
And whoever toucheth his bed, shall wash his clothes, and bathe [himself] in water, and be unclean until the evening.
6 Yeyote atakayeketi juu ya kitu chochote alichokalia mwenye kutokwa na usaha, ni lazima afue nguo zake, na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.
And he that sitteth on [any] thing on which he sat that hath the issue, shall wash his clothes, and bathe [himself] in water, and be unclean until the evening.
7 “‘Yeyote atakayemgusa mtu mwenye kutokwa na usaha, ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.
And he that toucheth the flesh of him that hath the issue, shall wash his clothes, and bathe [himself] in water, and be unclean until the evening.
8 “‘Ikiwa mtu mwenye kutokwa na usaha atamtemea mate mtu yeyote ambaye ni safi, mtu huyo ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.
And if he that hath the issue shall spit upon him that is clean; then he shall wash his clothes, and bathe [himself] in water, and be unclean until the evening.
9 “‘Kila tandiko ambalo mtu huyo atalikalia wakati wa kupanda mnyama litakuwa najisi,
And whatever saddle he rideth upon that hath the issue, shall be unclean.
10 na yeyote atakayegusa kitu chochote alichokuwa amekalia atakuwa najisi mpaka jioni. Yeyote atakayeinua vitu hivyo ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.
And whoever toucheth any thing that was under him shall be unclean until the evening; and he that beareth [any of] those things, shall wash his clothes, and bathe [himself] in water, and be unclean until the evening.
11 “‘Yeyote atakayeguswa na mtu anayetokwa na usaha bila kunawa mikono yake kwa maji, ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.
And whomsoever he toucheth that hath the issue (and hath not rinsed his hands in water) he shall wash his clothes, and bathe [himself] in water, and be unclean until the evening.
12 “‘Chungu cha udongo kitakachoguswa na mtu huyo ni lazima kivunjwe, na kifaa chochote cha mbao kitaoshwa kwa maji.
And the vessel of earth that he toucheth who hath the issue, shall be broken: and every vessel of wood shall be rinsed in water.
13 “‘Wakati mtu atakapotakasika kutoka usaha wake, anapaswa kuhesabu siku saba kwa utakaso wake. Ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji safi, naye atatakasika.
And when he that hath an issue is cleansed of his issue; then he shall number to himself seven days for his cleansing, and wash his clothes, and bathe his flesh in running water, and shall be clean.
14 Siku ya nane, atachukua hua wawili au makinda mawili ya njiwa, aje mbele za Bwana kwenye ingilio la Hema la Kukutania, na kumpa kuhani.
And on the eighth day he shall take to him two turtle-doves, or two young pigeons, and come before the LORD to the door of the tabernacle of the congregation, and give them to the priest:
15 Kuhani atavitoa dhabihu, mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi na huyo mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Kwa njia hii atafanya upatanisho mbele za Bwana kwa ajili ya huyo mtu kwa sababu ya kutokwa usaha kwake.
And the priest shall offer them, the one [for] a sin-offering, and the other [for] a burnt-offering; and the priest shall make an atonement for him before the LORD for his issue.
16 “‘Wakati mtu akitokwa na shahawa, ni lazima aoge mwili mzima kwa maji, na atakuwa najisi mpaka jioni.
And if any man's seed of copulation shall go from him, then he shall wash all his flesh in water, and be unclean until the evening.
17 Vazi lolote ama ngozi yoyote yenye shahawa juu yake ni lazima ioshwe kwa maji, na itakuwa najisi mpaka jioni.
And every garment, and every skin on which is the seed of copulation, shall be washed with water, and be unclean until the evening.
18 Ikiwa mtu atalala na mwanamke, na kukawa na kutoka kwa shahawa, ni lazima wote waoge kwa maji, nao watakuwa najisi mpaka jioni.
The woman also with whom man shall lie [with] seed of copulation, they shall [both] bathe [themselves] in water, and be unclean until the evening.
19 “‘Ikiwa mwanamke atatokwa na damu ya kawaida ya mwezi, atakuwa najisi kwa siku saba, na yeyote atakayemgusa atakuwa najisi mpaka jioni.
And if a woman shall have an issue, [and] her issue in her flesh be blood, she shall be put apart seven days: and whoever toucheth her shall be unclean until the evening.
20 “‘Chochote atakacholalia wakati wake wa hedhi kitakuwa najisi, na chochote atakachokikalia kitakuwa najisi.
And every thing that she lieth upon in her separation shall be unclean: every thing also that she sitteth upon shall be unclean.
21 Yeyote atakayegusa kitanda chake ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.
And whoever toucheth her bed shall wash his clothes, and bathe [himself] in water, and be unclean until the evening.
22 Yeyote atakayegusa chochote atakachokalia ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.
And whoever toucheth any thing that she sat upon shall wash his clothes, and bathe [himself] in water, and be unclean until the evening.
23 Kiwe ni kitanda ama chochote alichokuwa amekikalia, ikiwa mtu yeyote atakigusa, atakuwa najisi mpaka jioni.
And if it [be] on [her] bed, or on any thing on which she sitteth, when he toucheth it, he shall be unclean until the evening.
24 “‘Ikiwa mwanaume atalala naye na ile damu ya mwezi ikamgusa, atakuwa najisi kwa siku saba; kitanda chochote atakachokilalia huyo mwanaume kitakuwa najisi.
And if any man shall lie with her at all, and her flowers be upon him, he shall be unclean seven days: and all the bed on which he lieth shall be unclean.
25 “‘Ikiwa mwanamke atatokwa na damu kwa siku nyingi zaidi ya siku zake za mwezi, au amekuwa na damu inayoendelea zaidi ya kipindi chake, atakuwa najisi kwa kipindi chote cha shida hiyo, kama ilivyokuwa katika siku za hedhi yake.
And if a woman shall have an issue of her blood many days out of the time of her separation, or if it shall run beyond the time of her separation; all the days of the issue of her uncleanness shall be as the days of her separation: she [shall be] unclean.
26 Kitanda chochote atakachokilalia huyo mwanamke wakati anaendelea kutokwa na damu kitakuwa najisi, kama kilivyokuwa kitanda chake wakati wa siku zake za hedhi, na chochote atakachokalia kitakuwa najisi, kama wakati wake wa hedhi.
Every bed on which she lieth all the days of her issue shall be to her as the bed of her separation: and whatever she sitteth upon shall be unclean as the uncleanness of her separation.
27 Yeyote agusaye vitu hivyo atakuwa najisi; ni lazima afue nguo zake na kuoga kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.
And whoever toucheth those things shall be unclean, and shall wash his clothes, and bathe [himself] in water, and be unclean until the evening.
28 “‘Wakati atakapotakasika kutoka hedhi yake, ni lazima ahesabu siku saba, na baada ya hapo atakuwa safi kwa kawaida ya ibada.
But if she shall be cleansed of her issue, then she shall number to herself seven days, and after that she shall be clean.
29 Siku ya nane ni lazima achukue hua wawili au makinda mawili ya njiwa, na kumletea kuhani kwenye mlango wa Hema la Kukutania.
And on the eighth day she shall take to her two turtles, or two young pigeons, and bring them to the priest, to the door of the tabernacle of the congregation.
30 Kuhani atatoa dhabihu, mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na huyo mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Kwa njia hii, atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Bwana kwa sababu ya unajisi wa kutokwa damu kwake.
And the priest shall offer the one [for] a sin-offering, and the other [for] a burnt-offering; and the priest shall make an atonement for her before the LORD for the issue of her uncleanness.
31 “‘Ni lazima uwatenge Waisraeli kutokana na vitu ambavyo vinawafanya najisi, ili wasife katika unajisi wao kwa kunajisi makao yangu, ambayo yapo katikati yao.’”
Thus shall ye separate the children of Israel from their uncleanness: that they die not in their uncleanness, when they defile my tabernacle that [is] among them.
32 Haya ni masharti kwa ajili ya mtu mwenye kutokwa na usaha, kwa ajili ya yeyote atakayetokwa na shahawa,
This [is] the law of him that hath an issue, and [of him] whose seed goeth from him, and [he] is defiled therewith.
33 kwa ajili ya mwanamke katika siku zake za hedhi, kwa ajili ya mwanaume au mwanamke atokwaye na usaha, na kwa ajili ya mwanaume alalaye na mwanamke ambaye ni najisi kwa kawaida ya ibada.
And of her that is sick of her flowers, and of him that hath an issue, of the man and of the woman, and of him that lieth with her that is unclean.

< Mambo ya Walawi 15 >