< Yoshua 12 >

1 Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kuitwaa nchi yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba: 2 Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni. Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi. 3 Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya materemko ya Pisga. 4 Nayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei. 5 Naye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa watu wa Geshuri, na watu wa Maaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni. 6 Mose, mtumishi wa Bwana, na Waisraeli wakawashinda. Naye Mose mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao. 7 Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda upande wa magharibi mwa Yordani, kuanzia Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni hadi kufikia Mlima Halaki, unaoinuka ukielekea Seiri. (Yoshua alitoa nchi zao kwa makabila ya Israeli iwe urithi wao sawasawa na mgawanyiko wa makabila yao: 8 nchi ya vilima, shefela, upande wa magharibi, Araba, materemko ya milima, jangwa, na Negebu; nchi za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi): 9 mfalme wa Yeriko mmoja mfalme wa Ai (karibu na Betheli) mmoja 10 mfalme wa Yerusalemu mmoja mfalme wa Hebroni mmoja 11 mfalme wa Yarmuthi mmoja mfalme wa Lakishi mmoja 12 mfalme wa Egloni mmoja mfalme wa Gezeri mmoja 13 mfalme wa Debiri mmoja mfalme wa Gederi mmoja 14 mfalme wa Horma mmoja mfalme wa Aradi mmoja 15 mfalme wa Libna mmoja mfalme wa Adulamu mmoja 16 mfalme wa Makeda mmoja mfalme wa Betheli mmoja 17 mfalme wa Tapua mmoja mfalme wa Heferi mmoja 18 mfalme wa Afeki mmoja mfalme wa Lasharoni mmoja 19 mfalme wa Madoni mmoja mfalme wa Hazori mmoja 20 mfalme wa Shimron-Meroni mmoja mfalme wa Akishafu mmoja 21 mfalme wa Taanaki mmoja mfalme wa Megido mmoja 22 mfalme wa Kedeshi mmoja mfalme wa Yokneamu katika Karmeli mmoja 23 mfalme wa Dori (katika Nafoth-Dori) mmoja mfalme wa Goimu katika Gilgali mmoja 24 mfalme wa Tirsa mmoja wafalme jumla yao ilikuwa thelathini na mmoja.

< Yoshua 12 >