< Ayubu 25 >

1 Ndipo Bildadi Mshuhi akajibu: 2 “Mamlaka na kuheshimiwa ni vyake Mungu; yeye huthibitisha amani katika mbingu juu. 3 Je, majeshi yake yaweza kuhesabika? Ni nani asiyeangaziwa na nuru yake? 4 Mtu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu? Awezaje mtu aliyezaliwa na mwanamke kuwa safi? 5 Ikiwa hata mwezi sio mwangavu nazo nyota si safi machoni pake, 6 sembuse mtu ambaye ni funza: mwanadamu ambaye ni buu tu!”

< Ayubu 25 >