< Yeremia 46 >

1 Hili ni neno la Bwana lililomjia nabii Yeremia kuhusu mataifa:
This is the word of Yahweh that came to Jeremiah the prophet concerning the nations.
2 Kuhusu Misri: Huu ni ujumbe dhidi ya jeshi la Farao Neko mfalme wa Misri, lililoshindwa huko Karkemishi kwenye Mto Frati na Nebukadneza mfalme wa Babeli, katika mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda:
For Egypt: “This is about the army of Pharaoh Necho, king of Egypt that was at Carchemish by the Euphrates river. This was the army that Nebuchadnezzar king of Babylon defeated in the fourth year of Jehoiakim son of Josiah, king of Judah:
3 “Wekeni tayari ngao zenu, kubwa na ndogo, mtoke kwa ajili ya vita!
Get the small shields and the large shields ready, and go forward to fight.
4 Fungieni farasi lijamu, pandeni farasi! Shikeni nafasi zenu mkiwa mmevaa chapeo! Isugueni mikuki yenu, vaeni dirii vifuani!
Put the harness on the horses; mount up on the horses and take your stand with your helmets on; polish the spears and put on your armor.
5 Je, ninaona nini? Wametiwa hofu, wanarudi nyuma, askari wao wameshindwa. Wanakimbia kwa haraka pasipo kutazama nyuma, tena kuna hofu kuu kila upande,” asema Bwana.
What am I seeing here? They are filled with terror and are running away, for their soldiers are defeated. They are running for safety and are not looking back. Terror is all around—this is Yahweh's declaration—
6 Walio wepesi na wenye mbio hawawezi kukimbia, wala wenye nguvu hawawezi kutoroka. Kaskazini, kando ya Mto Frati, wanajikwaa na kuanguka.
the swift cannot run away, and the soldiers cannot escape. They stumble in the north and fall beside the Euphrates River.
7 “Ni nani huyu ajiinuaye kama Mto Naili, kama mito yenye maji yanayofanya mawimbi?
Who is this who rises like the Nile, whose waters toss up and down like the rivers?
8 Misri hujiinua kama Mto Naili, kama mito yenye maji yanayofanya mawimbi. Husema, ‘Nitainuka na kufunika dunia, nitaiangamiza miji na watu wake.’
Egypt rises like the Nile, like rivers of water that rise and fall. Egypt says, 'I will go up and I will cover the earth. I will destroy cities and their inhabitants.
9 Songeni mbele, enyi farasi! Endesheni kwa ukali, enyi magari ya farasi, Endeleeni mbele, enyi mashujaa: watu wa Kushi na Putu wachukuao ngao, watu wa Ludi wavutao upinde.
Go up, horses. Be angry, you chariots. Let the soldiers go out, Cush and Put, men skillful with a shield, and Ludim, men skillful at bending their bows.'
10 Lakini ile siku ni ya Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, siku ya kulipiza kisasi, kisasi juu ya adui zake. Upanga utakula hata utakapotosheka, hadi utakapozima kiu yake kwa damu. Kwa maana Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, atatoa dhabihu kwenye nchi ya kaskazini, kando ya Mto Frati.
That day will be the day of vengeance for the Lord Yahweh of hosts, and he will avenge himself on his foes. The sword will devour and be satisfied. It will drink its fill of their blood. For there will be a sacrifice to the Yahweh Lord of hosts in the northern land by the Euphrates River.
11 “Panda hadi Gileadi ukapate zeri, ee Bikira Binti wa Misri. Lakini umetumia dawa nyingi bila mafanikio; huwezi kupona.
Go up to Gilead and obtain medicine, virgin daughter of Egypt. It is useless that you put much medicine on yourself. There is no cure for you.
12 Mataifa yatasikia juu ya aibu yako, kilio chako kitaijaza dunia. Shujaa mmoja atajikwaa juu ya mwingine, nao wataanguka chini pamoja.”
The nations have heard of your disgrace. The earth is filled with your laments, for soldier stumbles against soldier; both of them fall together.”
13 Huu ndio ujumbe Bwana aliomwambia nabii Yeremia kuhusu kuja kwa Nebukadneza mfalme wa Babeli ili kuishambulia Misri:
This is the word that Yahweh told Jeremiah the prophet when Nebuchadnezzar king of Babylon came and attacked the land of Egypt:
14 “Tangaza hili katika Misri, nawe ulihubiri katika Migdoli, hubiri pia katika Memfisi na Tahpanhesi: ‘Shikeni nafasi zenu na mwe tayari, kwa kuwa upanga unawala wale wanaokuzunguka.’
“Announce in Egypt, and proclaim it in Migdol, Memphis, and Tahpanhes. 'Take your station and prepare yourself, for the sword will devour those around you.'
15 Kwa nini mashujaa wako wamesombwa na kupelekwa mbali? Hawawezi kusimama, kwa maana Bwana atawasukuma awaangushe chini.
Why are your mighty ones face-down on the ground? They will not stand, because I, Yahweh, have pushed them to the ground.
16 Watajikwaa mara kwa mara, wataangukiana wao kwa wao. Watasema, ‘Amka, turudi kwa watu wetu na nchi yetu, mbali na upanga wa mtesi.’
He increases the numbers of those who stumble. Each soldier falls against the next one. They are saying, 'Get up. Let us go home. Let us go back to our own people, to our native land. Let us leave this sword that is beating us down.'
17 Huko watatangaza, ‘Farao mfalme wa Misri ni makelele tu, amekosa wasaa wake.’
They proclaimed there, 'Pharaoh the king of Egypt is only a noise, one who has let his opportunity slip away.'
18 “Kwa hakika kama niishivyo,” asema Mfalme, ambaye jina lake ni Bwana Mwenye Nguvu Zote, “mmoja atakuja ambaye ni kama Tabori miongoni mwa milima, kama Karmeli kando ya bahari.
As I live—declares the King, whose name is Yahweh of hosts— someone will come like Mount Tabor and Mount Carmel by the sea.
19 Funga mizigo yako kwenda uhamishoni, wewe ukaaye Misri, kwa kuwa Memfisi utaangamizwa na kuwa magofu pasipo mkazi.
Pack for yourselves baggage to carry into exile, you who live in Egypt. For Memphis will become a waste, it will lie in ruins and no one will live there.
20 “Misri ni mtamba mzuri, lakini kipanga anakuja dhidi yake kutoka kaskazini.
Egypt is a very beautiful young cow, but a stinging insect is coming from the north. It is coming.
21 Askari wake waliokodiwa katika safu zake wako kama ndama walionenepeshwa. Wao pia watageuka na kukimbia pamoja, hawataweza kuhimili vita, kwa maana siku ya msiba inakuja juu yao, wakati wao wa kuadhibiwa.
The hired soldiers in her midst are like a fattened bull, but they will also turn away and run away. They will not stand together, for the day of their disaster is coming against them, the time of their punishment.
22 Misri atatoa sauti kama ya nyoka anayekimbia kadiri adui anavyowasogelea na majeshi, watakuja dhidi yake wakiwa na mashoka, kama watu wakatao miti.
Egypt hisses like a snake and crawls away, for her enemies are marching against her. They are going toward her like woodcutters with axes.
23 Wataufyeka msitu wake,” asema Bwana, “hata kama umesongamana kiasi gani. Ni wengi kuliko nzige, hawawezi kuhesabika.
They will cut down the forests—this is Yahweh's declaration—although it is very dense. For the enemies will be more numerous than locusts, unable to be counted.
24 Binti wa Misri ataaibishwa, atatiwa mikononi mwa watu wa kaskazini.”
The daughter of Egypt will be made ashamed. She will be given into the hand of people from the north.”
25 Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asema: “Nakaribia kuleta adhabu juu ya Amoni mungu wa Thebesi, na juu ya Farao, Misri na miungu yake, na wafalme wake, pamoja na wale wanaomtegemea Farao.
Yahweh of hosts, the God of Israel, says, “See, I am about to punish Amon of Thebes, Pharaoh, Egypt and her gods, her kings the Pharaohs, and those who trust in them.
26 Nitawatia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wao, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na maafisa wake. Hatimaye, hata hivyo, Misri itakaliwa kama nyakati zilizopita,” asema Bwana.
I am giving them into the hand of the ones seeking their lives, and into the hand of Nebuchadnezzar king of Babylon and his servants. Then after this Egypt will be inhabited as in previous days—this is Yahweh's declaration.
27 “Usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu, usifadhaike, ee Israeli. Hakika nitakuokoa kutoka nchi za mbali, uzao wako kutoka nchi ya uhamisho wao. Yakobo atakuwa tena na amani na salama, wala hakuna hata mmoja atakayewatia hofu.
But you, my servant Jacob, do not fear. Do not be dismayed, Israel, for see, I am about to bring you back from far away, and your offspring from the land of their captivity. Then Jacob will return, find peace, and be secure, and there will be no one to terrify him.
28 Usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu, kwa maana mimi niko pamoja nawe,” asema Bwana. “Ingawa nitayaangamiza kabisa mataifa yote ambayo miongoni mwake nimekutawanya, sitakuangamiza wewe kabisa. Nitakurudi, lakini kwa haki tu, wala sitakuacha kabisa bila kukuadhibu.”
You, my servant Jacob, do not fear—this is Yahweh's declaration—for I am with you, so I will bring complete destruction against all the nations where I scattered you. But I will not destroy you completely. Yet I will discipline you justly and will certainly not leave you unpunished.”

< Yeremia 46 >