< Isaya 10 >

1 Ole wao wawekao sheria zisizo za haki, kwa wale watoao amri za kuonea,
Woe to those who decree unrighteous decrees, and to the writers who write oppressive decrees;
2 kuwanyima maskini haki zao na kuzuilia haki za watu wangu walioonewa, kuwafanya wajane mawindo yao na kuwanyangʼanya yatima.
to deprive the needy from justice, and to rob the poor among my people of their rights, that widows may be their spoil, and that they may make the fatherless their prey.
3 Mtafanya nini siku ya kutoa hesabu, wakati maafa yatakapokuja kutoka mbali? Mtamkimbilia nani awape msaada? Mtaacha wapi mali zenu?
What will you do in the day of visitation, and in the desolation which will come from afar? To whom will you flee for help? Where will you leave your wealth,
4 Hakutasalia kitu chochote, isipokuwa kujikunyata miongoni mwa mateka, au kuanguka miongoni mwa waliouawa. Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali, mkono wake bado umeinuliwa juu.
so as not to kneel with the prisoners, or fall among the slain? For all this his anger is not turned away, but his hand is stretched out still.
5 “Ole kwa Ashuru, fimbo ya hasira yangu, ambaye mkononi mwake ana rungu ya ghadhabu yangu!
Alas Assyrian, the rod of my anger, the staff in whose hand is my indignation.
6 Ninamtuma dhidi ya taifa lisilomjua Mungu, ninamtuma dhidi ya taifa linalonikasirisha, kukamata mateka na kunyakua nyara, pia kuwakanyaga chini kama matope ya barabarani.
I will send him against a profane nation, and against the people who anger me will I give him a command to take the spoil and to take the prey, and to tread them down like the mire of the streets.
7 Lakini hili silo analokusudia, hili silo alilo nalo akilini; kusudi lake ni kuangamiza, kuyakomesha mataifa mengi.
However he doesn't mean so, neither does his heart think so; but it is in his heart to destroy, and to cut off not a few nations.
8 Maana asema, ‘Je, wafalme wote si majemadari wangu?
For he says, "Aren't all of my officials kings?
9 Je, Kalno hakutendwa kama Karkemishi? Hamathi si kama Arpadi, nayo Samaria si kama Dameski?
Isn't Calno like Carchemish? Isn't Hamath like Arpad? Isn't Samaria like Damascus?
10 Kama vile mkono wangu ulivyotwaa falme za sanamu, falme ambazo vinyago vyao vilizidi vile vya Yerusalemu na Samaria:
As my hand has found the kingdoms of the idols, whose engraved images exceeded those of Jerusalem and of Samaria;
11 je, nisiishughulikie Yerusalemu na sanamu zake kama nilivyoshughulikia Samaria na vinyago vyake?’”
shall I not, as I have done to Samaria and her idols, so do to Jerusalem and her idols?"
12 Bwana atakapokuwa amemaliza kazi yake yote dhidi ya Mlima Sayuni na Yerusalemu, atasema, “Nitamwadhibu mfalme wa Ashuru kwa ajili ya majivuno ya ukaidi wa moyo wake na kutazama kwa macho yenye dharau.”
Therefore it will happen that, when the LORD has performed his whole work on Mount Zion and on Jerusalem, he will punish the fruit of the willful proud heart of the king of Assyria, and the insolence of his haughty looks.
13 Kwa kuwa anasema: “‘Kwa nguvu za mkono wangu nimefanya hili, kwa hekima yangu, kwa sababu nina ufahamu. Niliondoa mipaka ya mataifa, niliteka nyara hazina zao, kama yeye aliye shujaa niliwatiisha wafalme wao.
For he has said, "By the strength of my hand I have done it, and by my wisdom; for I have understanding: and I have removed the boundaries of the peoples, and have robbed their treasures. Like a valiant man I have brought down their rulers.
14 Kama mtu atiavyo mkono kwenye kiota, ndivyo mkono wangu ulivyochukua utajiri wa mataifa; kama watu wakusanyavyo mayai yaliyoachwa, ndivyo nilivyokusanya nchi zote; wala hakuna hata mmoja aliyepiga bawa au kufungua kinywa chake kutoa mlio.’”
My hand has found the riches of the peoples like a nest, and like one gathers eggs that are abandoned, have I gathered all the earth. There was no one who moved their wing, or that opened their mouth, or chirped."
15 Je, shoka laweza kujigamba kuwa na nguvu zaidi kuliko yule anayelitumia, au msumeno kujisifu dhidi ya yule anayeutumia? Ni kana kwamba fimbo ingeweza kumwinua yeye aichukuaye, au mkongojo ungemwinua mwenye kuutumia!
Should an axe brag against him who chops with it? Should a saw exalt itself above him who saws with it? As if a rod should lift those who lift it up, or as if a staff should lift up someone who is not wood.
16 Kwa hiyo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, atatuma ugonjwa wa kudhoofisha kwa askari wake walio hodari, katika fahari yake moto utawaka kama mwali wa moto.
Therefore the LORD of hosts, will send among his fat ones leanness; and under his glory a burning will be kindled like the burning of fire.
17 Nuru ya Israeli itakuwa moto, Aliye Mtakatifu wao mwali wa moto; katika siku moja utaunguza na kuteketeza miiba na michongoma yake.
The light of Israel will be for a fire, and his Holy One for a flame; and it will burn and devour his thorns and his briers in one day.
18 Fahari ya misitu yake na mashamba yenye rutuba utateketeza kabisa, kama vile mtu mgonjwa adhoofikavyo.
He will consume the glory of his forest, and of his fruitful field, both soul and body. It will be as when a standard bearer faints.
19 Nayo miti inayobaki katika misitu yake itakuwa michache sana hata mtoto mdogo angeweza kuihesabu.
The remnant of the trees of his forest shall be few, so that a child could write their number.
20 Katika siku ile, mabaki ya Israeli, walionusurika wa nyumba ya Yakobo, hawatamtegemea tena yeye aliyewapiga, lakini watamtegemea kwa kweli Bwana Aliye Mtakatifu wa Israeli.
It will come to pass in that day that the remnant of Israel, and those who have escaped from the house of Jacob will no more again lean on him who struck them, but shall lean on the LORD, the Holy One of Israel, in truth.
21 Mabaki watarudi, mabaki wa Yakobo watamrudia Mungu Mwenye Nguvu.
A remnant will return, even the remnant of Jacob, to the mighty God.
22 Ingawa watu wako, ee Israeli, ni wengi kama mchanga wa pwani, ni mabaki yao tu watakaorudi. Maangamizi yamekwisha amriwa, ni mengi tena ni haki.
For though your people, Israel, are as the sand of the sea, a remnant will be kept safe. For he will fulfill the word and decisively, overflowing in righteousness;
23 Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, atatekeleza maangamizi yaliyoamriwa juu ya nchi yote.
because the Lord will carry out the word decisively in the midst of the earth.
24 Kwa hiyo, hili ndilo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: “Enyi watu wangu mkaao Sayuni, msiwaogope Waashuru, wanaowapiga ninyi kwa fimbo na kuinua rungu dhidi yenu, kama Misri ilivyofanya.
Therefore the LORD of hosts says: "My people who dwell in Zion, do not be afraid of the Assyrian, though he strike you with the rod, and lift up his staff against you, as Egypt did.
25 Bado kitambo kidogo sana hasira yangu dhidi yenu itakoma, na ghadhabu yangu itaelekezwa kwenye maangamizi yao.”
For yet a very little while, and the indignation against you will be accomplished, and my anger will be directed to his destruction."
26 Bwana Mwenye Nguvu Zote atawachapa kwa mjeledi, kama alivyowapiga Wamidiani katika mwamba wa Orebu, naye atainua fimbo yake juu ya maji, kama alivyofanya huko Misri.
The LORD of hosts will stir up a scourge against him, as in the slaughter of Midian at the rock of Oreb. His rod will be over the sea, and he will lift it up like he did against Egypt.
27 Katika siku hiyo mzigo wao utainuliwa kutoka mabegani mwenu, na nira yao kutoka shingoni mwenu; nira itavunjwa kwa sababu ya kutiwa mafuta.
It will happen in that day, that his burden will depart from off your shoulder, and his yoke from off your neck, and the yoke shall be destroyed because of the anointing.
28 Wanaingia Ayathi, wanapita katikati ya Migroni, wanahifadhi mahitaji huko Mikmashi.
He has come to Aiath. He has passed through Migron. At Michmash he stores his baggage.
29 Wanavuka kivukoni, nao wanasema, “Tutapiga kambi huko Geba usiku kucha.” Rama inatetemeka; Gibea ya Sauli inakimbia.
He went through the pass. He has lodged at Geba. Ramah trembles. Gibeah of Saul has fled.
30 Piga kelele, ee Binti Galimu! Sikiliza, ee Laisha! Maskini Anathothi!
Cry aloud with your voice, daughter of Gallim. Listen, Laishah. You poor Anathoth.
31 Madmena inakimbia; watu wa Gebimu wanajificha.
Madmenah is a fugitive. The inhabitants of Gebim flee for safety.
32 Siku hii ya leo watasimama Nobu; watatikisa ngumi zao kwa mlima wa Binti Sayuni, kwa kilima cha Yerusalemu.
This very day he will halt at Nob. He shakes his hand at the mountain of the daughter of Zion, the hill of Jerusalem.
33 Tazama, Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, atayakata matawi kwa nguvu kuu. Miti mirefu sana itaangushwa, ile mirefu itashushwa chini.
Look, the Lord, the LORD of hosts, will lop the boughs with terror. The tall will be cut down, and the lofty will be brought low.
34 Atakata vichaka vya msitu kwa shoka; Lebanoni itaanguka mbele zake yeye Mwenye Nguvu.
He will cut down the thickets of the forest with iron, and Lebanon will fall by the Mighty One.

< Isaya 10 >